Wamisionari waliofika Tanganyika walikuta watu wamestaarabika na wanajua kusoma na kuandika

Wamisionari waliofika Tanganyika walikuta watu wamestaarabika na wanajua kusoma na kuandika

Ingekuwa Uislamu unakumbatia elimu ya kisasa au Kikoloni, leo hii ungekuta karibu kila msikiti una taasisi rasmi ya kutoa elimu dunia, kuanzia chekechea mpaka chuo kikuu.
 
Tuambiane ukweli, kimsingi madrasa zote zipo kupandikiza imani, tamaduni na mila za kiislamu kwa watoto. Hazina mchango wowote wa maana kwa mtoto kwenye kumfanya akawa bora kwenye elimu dunia. Hilo limekuwa hivyo miaka yote.
 
Mzee Said analazimisha sana Uislamu uwe ndio alama ya Uhuru wa Tanganyika, wakati kiuhalisia uhuru wa Tanganyika ni matokeo ya siasa za hapa na pale na utashi wa muingereza. Waambie watu ukweli, muingereza alishapoteza interest za kuendelea kuitawala Tanganyika directly hivyo akaamua kuitawala indirectly kwa kutuachia Uhuru bandia.
 
Hapo utamkosha mzee MS🤣
Ins...
Hapana siwezi kufurahishwa na kejeli.
Mimi niko JF toka 2008.

Kilichonivuta hapa ni historia ya kupigania uhuru wa Tanganyika.

Nilianza kwa kueleza kuwa historia inayosomeshwa kuanzia shule ya msingi hadi Chuo Kikuu ina upungufu mkubwa.

Historia hii imeacha wazalendo wengi wengi wao wakiwa Waislam na imekuwa ikieleza historia ya Julius Nyerere peke yake.

Kwa kusema hivi ikawa nimegusa hisia za wengi na hapa ndipo mjadala huu ulipoanza.

Kwanza wasomaji wengi hawakuamini nilichokuwa naandika na baadhi walighadhibika na kuanza "name calling," kuniita majina kama "sheikh," "ustaadh," "mufti" na kadhalika.

Walikuwa wanajaribu kunifanya kichekesho kwa kejeli hizi.

Wengine wakawa wanajadiliana na mimi na kutia Kiingereza katika maandishi yao.

Nikafahamu kuwa wasomaji wangu wengi wanataabishwa na kule kutojua historia ya kweli na kutonifahamu.

Ikawa sasa nina kazi mbili.

Kazi ya kwanza kujieleza nifahamike na kazi ya pili kuleta ushahidi kuwa historia ya uhuru ilikuwa haijaandikwa na mimi ndiye mtu wa kwanza kuandika historia ya kweli ya uhuru wa Tanganyika na historia ya TANU.

Hapo ndipo nilipojiambia kuwa nimepata darasa kubwa sana lenye wanafunzi wanaohitaji kusomeshwa historia ya kweli.

Nikawa sasa nafundisha historia ya uhuru nikisaidiwa na picha na rejea.

Hili darasa bado ninalo na wanafunzi wamekuwa wakiongezeka siku baada ya siku.

Hakuna katika ninayoeleza suala la mimi kusomesha Uislam au kutaka Tanzania iwe nchi ya Kiislam.

JF Jukwaa la Historia kwa uandishi huu wangu wakanipa tuzo ya Mwandishi Bora wa historia kwa miaka miwili mfululizo 2021 na 2022.

1707971503466.png
 
1707968547987.png
Mzee Said analazimisha sana Uislamu uwe ndio alama ya Uhuru wa Tanganyika, wakati kiuhalisia uhuru wa Tanganyika ni matokeo ya siasa za hapa na pale na utashi wa muingereza. Waambie watu ukweli, muingereza alishapoteza interest za kuendelea kuitawala Tanganyika directly hivyo akaamua kuitawala indirectly kwa kutuachia Uhuru bandia.​
Zan...
Unasema nalazimisha Uislam uwe ndiyo alama ya uhuru wa Tanganyika.
Vipi nilazimishe?

Nachukulia wewe hutaki Uislam kujitokeza katika historia ya uhuru wa Tanganyika.

Lakini kweli hili linawezekana?
Wamejaribu watu huko nyuma kulitekeleza hili.

Imeshindikana baada ya mimi kuandika kitabu cha Abdul Sykes.

Kila aliyekisoma kitabu hiki alipigwa na butwaa kubwa na sababu yake ni kuwa alikuwa anasoma historia mpya.

Nakupa mfano mmoja kwa kukuwekea moja ya Nyaraka za Sykes kisha In Shaa Allah nitakupa maelezo chini ya picha:

1707967913343.png

Kutokana na nyaraka hiyo hapo juu nimeandika maneno haya katika kitabu cha Abdul Sykes:
''Nakala ya barua isiyokuwa na tarehe kutoka TAA kwenda kwa Malkia Elizabeth iliyotiwa saini na viongozi wote wa TAA: Rais Julius Nyerere, Makamu wa Rais Abdulwahid Sykes, Katibu Mkuu Dome Okochi, Naibu Katibu Dossa Aziz, Mweka Hazina John Rupia, Naibu Mweka Hazina Ally Sykes ikimpongeza Malkia kwa kutawazwa.''

Huu ulikuwa mwaka wa 1953 na uongozi wa TAA ulikuwa ndiyo huo.

Ulikuwa unaijua historia hii au umepata kuisoma popote pale?

Dome Okochi Budohi ni huyo hapo chini:

1707968376295.png

Picha hii ipo katika kitabu cha Abdul Sykes
niko na Dome Budohi Ruiru, Nairobi 1972​
1707968541890.png

 
Ingekuwa Uislamu unakumbatia elimu ya kisasa au Kikoloni, leo hii ungekuta karibu kila msikiti una taasisi rasmi ya kutoa elimu dunia, kuanzia chekechea mpaka chuo kikuu.
Zan...
Sikulaumu.
Huijui historia ya Waislam na juhudi yao katika elimu.

Soma hapo chini niliyoandika katika kitabu cha Abdul Sykes kuhusu suala la elimu:

Mkutano wa Kwanza wa Waislam (Muslim Congress), 1962

Baada ya uhuru kupatikana mwaka 1961 Waislam waliamini kuwa hali yao ya baadae katika serikali huru itakuwa nzuri.

Mwaka 1962 ukaitishwa mkutano wa Waislam wa nchi nzima kujadili nafasi ya Uislam katika Tanganyika huru.

Taasisi zifuatazo zilihudhuria mkutano huo: East African Muslim Welfare Society (EAMWS), Daawat Islamiyya, Jamiatul Islamiya fi Tanganyika, Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika na Muslim Education Union.

Mkutano huu ulikubaliana pamoja na mambo mengine, umuhimu wa kuanzisha idara ya elimu chini ya EAMWS.

Waislam hawakusubiri serikali itimize ahadi yake ya kurekebisha upogo uliokuwepo wa elimu kati ya Waislam na Wakristo.

Waislam walianzisha mipango yao wenyewe ili isaidiane na juhudi ya serikali.

Mipango ikatayarishwa ya kujenga shule Tanganyika nzima na mwishowe kujenga Chuo Kikuu cha kwanza kwa Waislam katika Afrika ya Mashariki.

Mkutano ukamchagua Tewa Said Tewa waziri wa serikali, mwanasiasa wa TAA na mmoja wa wale wazalendo 17 walioanzisha TANU kuwa mwenyekiti wa EAMWS kwa upande wa Tanganyika.

Huu ndiyo ukawa mwanzo wa uadui kati ya Waislam na serikali.

Uelewano uliodumu wakati wa kudai uhuru ukaanza kutoweka na siasa zikachukua sura mpya ya uhasama, kutoaminiana na kutafutana.

Kisa cha hali hii mpya ikiwa ni sababu ya Waislam kutaka kuondoa hali ya kikoloni iliyowakandamiza kwa miaka mingi.

Waislam waliona kuwa hili lilikuwa ni jambo lisilokuwa na pingamizi kufanyika.

Uhuru ili uwe na maana ni lazima Waislam wajitoe ndani ya unyonge waliogubikwa na wakoloni.

Kwa upande wa serikali hali hii ilisababisha hofu kubwa.''
(Kutoka kitabu cha Abdul Sykes)

Ukitaka kusoma zaidi kuhusu tatizo hili ingia:
 
Huu ni Uongo uliokubuu😂 Katika nchi zote za Kiislam Madrasa ni kwa ajili ya kufundisha Quran na Kiarabu. Katika tembea yangu kiasi Duniani hapa sijaona Madrasa inafundisha zaidi ya hivi viti viwili. Madrasa zilianzishwa miaka kadhaa baada ya Kuanzishwa Dini ya Kiislam. Muhamad akusoma Madrasa. Asili ya Kufundisha Watoto ilianzia Misri enzi za Falao na ata ukisoma maandiko .Musa alisoma katk shule za Misri,,Elimu ambayo ilimwezesha kufanya vikao na majadiliano na Farao mpaka akawapa rukhusa Waisrael watoke Misri, Pia Elimu hiyo hiyo Ilimsaidia Musa Kuwaongoza Kuhukumu na kuwatawala wana Israel Jangwani wakiwa wanaelekea Jerusalem kwenye nchi yao. (Hapa unaona kuwa Musa alikuwa na Elimu zaidi ya moja ikiwemo Sheria, Uongozi etc)Israel waliendeleza utamaduni wa Kusomesha watoto wao.... na ata Yesu Aliweza Soma katika shule hizo na Yeye kujua kusoma na Kuandika pamoja na mambo mengine kama Sheria n.k,,,(Bibilia ina ushaidi wa Yesu kujua kusoma na kuandika na pia kuwa na Elimu tosha ya Dini na pia Siasa- Kitu ambacho kilimwezesha kuhubiri na kufanya kazi zake Kisomi na umakini wa hali ya juu) Warabu wakakopy ila wao ikiwa ni mafundisho ya kitabu kimoja tu... hu ndo ukweli
Mkuu:
Jaribu kufanya utafiti kidogo tu kuhusu University of Timbuktu Kuanzia karne ya 13-18 halafu linganisha na andiko lako.
 
Mas...
Napenda kusomesha.
Haya ni mambo muhimu sana ambayo yanataka watu waelezwe kwa kina.

Umemsikia Rais Samia Hassan akimkabidhi Pope zawadi ya mfano wa mlango wa Kizanzibari anamwambia Zanzibar ilifungua mlango kwa Ukristo kuingia Germany Ostafrika.

Johann Krapf alipofika katika Barza ya Chief Kimweri anahukumu kesi huku anaandika. na kavaa kama alivyomkuta Sultan Barghash wa Zanzibar alivyovaa na anapeperusha bendera ya Sultan.

View attachment 2902155
Chief Kimweri​
Kwahiyo alikuwa chini ya sultan?
 
Mimi nikionaga andiko la huyu Mohamed Saidi ... Najua haendi mbali na udini, na hawezi kutoka humo kamwe.... Kunakuwa hakuna jipya
 
Naam alikuwa chini ya Sultan.
Mimi nikionaga andiko la huyu Mohamed Saidi ... Najua haendi mbali na udini, na hawezi kutoka humo kamwe.... Kunakuwa hakuna jipya
Newazz,
Bahati mbaya wewe unaona udini.

Wako wengi sana katika vyombo vya habari ndani na nje ya mipaka yetu hawanioni hivyo.

Ushahidi ni mialiko niliyopokea kutoka kwao nizungumze vyuoni kwao na kuzungumza na vyombo vyao.

Haya nimeeleza mara nyingi hapa.
 
The past serves no purpose; its useles!
Use...
Inaelekea hujui kilichitokea baada ya kitabu cha Abdul Sykes kuchapwa.

Kiliandikiwa book review tatu: John Iliffe, James Brennan na Jonathon Glassman na kuchapwa katika Cambridge Journal of African History.

Nikaalikwa University of Iowa na Northwestern University, Marekani.

Jiulize.
 
Ni upi mchango wa ukristo/wakristo kwa chochote hapa nchini?
Kama upo basi naomba hata michango yao 3 tu.
 
Back
Top Bottom