Wamisionari waliofika Tanganyika walikuta watu wamestaarabika na wanajua kusoma na kuandika

Wamisionari waliofika Tanganyika walikuta watu wamestaarabika na wanajua kusoma na kuandika

Longo longo na Ujanja Mwingi! Anafikiri humu kuna mamuma wa kuwaongopea aweke link tuzione
Chipukizi,
Kama kuna kitu unakitaka kutoka kwangu nifahamishe kiungwana nitakupatia.

Hapana haja ya kunivunjia heshima.

Unataka link ya makala niliyoandika miaka 20 iliyopita?

Ingia YouTube Fanya name search.

Fanya hivyo ikiwa hujapata ukitakacho nifahamishe.

Ingia: mohamedsaidsalum.blogspot.com.

Fanya search.

Ikiwa hujapata ukitakacho In Shaa Allah nifahamishe.
PUBLICATIONS/RESEARCH PAPERS/ARTICLES

The Life and Times of Abdulwahid Sykes 1924 –1968 The Untold Story of the Muslim Struggle against British Colonialism in Tanganyika, Minerva Press London, 1998 translated into Kiswahili as Maisha na Nyakati za Abdulwahid Sykes 1924-1968 Historia Iliyofichwa Kuhusu Harakati za Waislam Dhidi ya Ukoloni wa Waingereza, Phoenix Publishers, Nairobi, 2002.

The Torch on Kilimanjaro, Oxford University Press, Nairobi, 2006

Contributing author for an African anthology: The Mermaid of Msambweni and Other Stories, Oxford University Press 2007, Nairobi.

Contributing author Dictionary of African Biography (DAB), Oxford University Press 2011, New York.

Uamuzi wa Busara, Abantu Publications 2008, Dar es Salaam.

Watu Mashuhuri Katika Uhuru wa Tanganyika No. 1, Ibn Hazm Media Centre, 2018, Dar es Salaam.

Watu Mashuhuri Katika Uhuru wa Tanganyika No.2, Ibn Hazm Media Centre 2018, Dar es Salaam

Dar es Salaam na Wazalendo Wake Mashujaa Katika Kupigani Uhuru wa Tanganyika Ibn Hazm Media Centre 2018, Dar es Salaaam

Watu Mashuhuri Katika Kuulingania Uislam Tanzania, Sheikh Ilunga, Ibn Hazm Media Centre 2018, Dar es Salaam

Dola, Kanisa na Tatizo la Udini Tanzania, Ibn Hazm Media Centre, 2018, Dar es Salaam

The School Trip to Zanzibar, Africa Proper Education Network 2020, Dar es Salaam

Rajabu Ibrahim Kirama, Jemadari wa Vita Kuwa Jemadari wa Uislam, Readit, 2020, Dar es Salaam

Sal Davis, An Autobiography, Readit/Amazon, 2023, Dar es Salaam

In Praise of Ancestors (1987) Africa Events (London).

Abdulwahid Sykes: Founder of Political Movement (1988) Africa Events (London).

Islam and Politics in Tanzania (1989) Al Haq International (Karachi)

The Plight of Tanzanian Muslim (1993) Change (Dar es Salaam).

Tanzania - The "Secular" Unsecular State (1995) Change (Dar es Salaam).

The Question of Muslim Stagnation in Education in Tanzania - A Muslim Riddle (Paper presented at the Conference of the Global World of the Swahili Intercultural Dialogue on the Indian Ocean Zanzibar, February 20 - 23, 2003).

Islamic Education and Intellectualism in Eastern Africa ‘Themes from the Pulpit in Tanganyika (Tanzania Mainland) 1800 – 2000’ (Paper presented at International Symposium on Islamic Civilisation in Eastern Africa Kampala, Uganda organised by the Islamic Conference Research Centre for Islamic History, Art and Culture (IRCICA), Istanbul and the Islamic University in Uganda, Mbale December 15th – 17th 2003).

Sheikh Hassan bin Ameir - The Moving Spirit of Muslim Emancipation in Tanganyika (1950 – 1968) (Paper presented at Youth Camp Organised by Zanzibar University, World Assembly of Muslim Youth (WAMY) and Tanzania Muslim Students Association (TAMSA) 27th February – 4th March 2004).

Islamic Movement and the Christian Lobby in Tanzania - the Experience of the late Prof. Kighoma Ali Malima (1938 – 1995) (Paper Presented to Tanzania Muslim Students Association (TAMSA) Sokoine University of Agriculture (SUA) Morogoro 11th April 2004).

Terrorism in East Africa the Tanzanian Experience (Paper Presented at the Conference on Islam, Terrorism and African Development University of Ibadan, Nigeria 8th - 10th February 2006).

Al Marhum Sheikh Kassim bin Juma bin Khamis (1940 – 1994) and the Pork Riots of 1993. (Paper Presented at the Regional Conference on Islam in Eastern Africa: Islam Encounter with the Challenges of the 21st Century 1st - 3rd August 2006, Kenyatta University, Nairobi.

Muslim Bible Scholars of Tanzania – The Legacy of Sheikh Ahmed Deedat (1918 – 2005) Paper Presented at the International Symposium on Islamic Civilisation in Southern Africa Organised by The Organisation of Islamic Conference Research Centre for Islamic History, Art and Culture (IRCICA) The National AWQAF Foundation of South Africa (AWQAF SA 1 – 3 September 2006 University of Johannesburg.

Tanzania: A Nation Without Heroes Seminar Organised by IFRA French Institute for Research in Africa and BIEA British Institute in East Africa 23rd and 24th September 2013 at IFRA Nairobi.

Awards: Several Awards

Visiting Scholar: (2011)

University of Iowa, Iowa City, USA

Northwestern University, Chicago, Illinois, USA

Zentrum Moderner Orient (ZMO), Berlin.

OTHER COUNTRIES VISITED

Zambia, Ethiopia, Great Britain, Swaziland, Msumbiji, Zimbabwe, Zambia, Sudan, Egypt, Saudi Arabia, United Arab Emirates, Oman, Yemen, Uganda, Switzerland, Iran, France, Netherlands, Turkey and Abu Dhabi.​
 
Mr. Q,
Inakisiwa nina makala zipatazo 10,000.

Hizi zipo JF, FB na You Tube.

Nina makala nyingine hapa: mohamedsaidsalum.blogspot.com.

Nina makala nyingine hizi ndizo za mwanzo miaka ya 1980s Library of Congress, Washington DC.

Nilipoanza kuandika nilikuwa naandika kwa Kiingereza.

Baadae nikabadili nikaanza kuandika kwa Kiswahili.

Nina makala nyingi wala sijui idadi yake katika magazeti haya: Annur, Rai, Mwananchi, Raia Mwema, Mtanzania na The East African.

Makala nyingine zipo Uingereza: Africa Events na New African (London).

Ninazo papers muhimu za mada nilizozungumza Vyuo Vikuu Tanzania na nje ya mipaka yake, Kenya, Afrika Kusini, Nigeria, Ujerumani na Marekani.
Link ya youtube itapendeza mkuu wamgu au maneno ya kutumia basi nika search mwenyewe huko youtube
 
Uzalendo,
Walikuwa wanajua kusoma na kuandika Kiswahili, Kijerumani na Kiarabu.
Mbona uzushi huu..
Kwamba Wajerumani walipokuja enzi hizo walikuta wafuasi wa mudi tayari wanajua kusoma na kuandika kiswahili, kijerumani na kiarabu kupitia kusoma madrasa.

Hicho kijerumani ni nani alikuwa amewafunza humo madrasa kabla ya ujio wa Wajerumani?
Bora ungesema walikuwa wanajua kiarabu na lugha za kienyeji..

Mwisho, hapo umeongelea Zanzibar na Tanga tu. Je, huko kwingine kama Mbeya, Ruvuma, Mtwara, Rukwa, Mwanza, Mara, Arusha, nk kulikuwa na Elimu gani?
 
Ant...
Nakuomba kitu kimoja tufanye mjadala wa kuheshimiana.
Maneno kama, ''wafuasi wa Mudi,'' hayapendezi na yataharibu hadhi ya mjadala wetu.

Mimi niko hapa kusomesha historia ambayo wengi hawaifahamu.
Tufanye mjadala wa adabu ili yule atakae kusoma anufaike na mjadala wetu.

Kuhusu elimu ya madrasa kuna paper ya Ishumi Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam Department of Education ambayo alizungumzia kuhusu Waislam kuwa watu wa kwanza kuelimika katika Pwani ya Afrika ya Mashariki.

Bahati mbaya sikumbuki ''citation,'' yake lakini mtu akifika Maktaba ya Chuo Kikuu anaweza akaipata.

Wajerumani walifungua shule Ocean Raod na ndilo waliposoma Kleist Sykes, Schneider Plantan, Thomas Plantan, Mashado Plantan na watoto wengi wa Dar es Salaam wakati wa utawala wa Wajerumani.

Hapo ndipo walipofundishwa Kijerumani.

Kijeruamani kilifundishwa baada ya Wajerumani kuingia baada ya Berlin Conference 1842.

Haya unaweza ukayasoma katika, Seminar Paper ya DA Sykes, ''The Life of Kleist Sykes,'' Ref. No. JAN/HIST/143/15 Maktaba ya Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam, East Africana, Department of History (1968).

Hayo mengine hapa kwa sasa si mahali pake ndiyo maana nimeyanyamazia.

Msikilize Thomas Plantan hapo chini akizunumza Kijerumani:
 
Kama mlikuwa mmeendelea kiasi hiki kielimu ilikuwaje wakristu wakawazidi?
 
Wajerumani walipofika Tanganyika waliwakuta Waislam wanafahamu kuandika, kusoma na walikuwa wameelimika katika hesabu.

Mmishionari Ludwig Krapf alipofika kwa Chifu Kimweri wa Usambaa mwaka 1848 alimkuta yeye na wanae wote wanajua kusoma na kuandika.

Krapf alikuwa na barua mkononi kutoka Zanzibar kwa Sultan Barghash ikimuomba Chief Kimweri amsaidie Krapf kwani ni "mtu wa Mungu."

Herufi walizokuwa wakitumia zilikuwa za Kiarabu.

Wajerumani kwa ajili hii basi waliwaajiri Waislam kama walimu, wakalimani na makarani serikalini.

Wamisionari na wakoloni waliona wivu kwa maendeleo haya waliyoyakuta kwa Waislam.

Kubwa zaidi ni kuwa walikuwa wamekuja kustaarabisha watu "washenzi'' badala yake wamewakuta watu walistaarabika na wanye utamaduni wa kupendeza.

Elimu hii yote na utamaduni huu wa hali ya juu ulikuwa unatokana na Uislam na elimu iliyokuwa imetolewa na madras.

Hapo ndipo zilipoaanza mbinu ya kuvunja maendeleo haya yote.

Herufi za Kiarabu zikapigwa marufuku kutumika na badala yake watu wakalazimishwa kujifunza herufi za Kirumi.

Muislam ambae jana alipoingia kulala alikuwa anaitwa ameelimika akaamka asubuhi yake mjinga, hana elimu, hajui kusoma wala kuandika.

Njama hizi zote dhidi ya Uislam ilikuwa sehemu ya makubaliano kama ilivyoandikwa katika kifungu IV cha Mkutano wa Berlin wa mwaka 1884.

Kifungu hicho kilikuwa kinasema kuwa Ukristo ni lazima ulindwe dhidi ya Uislam.

Kati ya mwaka 1888 -1892 katika kutekeleza kifungu hicho kama ilivyokubalika katia Mkutano wa Berlin, Imperial British East Africa Company ilitumia nguvu za kisiasa na kijeshi kuulinda Ukristo na taasisi zake zote katika Afrika ya Mashariki.

Ombwe lililoachwa na madrsa ikajazwa na shule zilizojengwa na Serikali na Kanisa chini ya usimamizi wa wakoloni.

Historia iliyoandikwa inasema kuwa Kanisa ndilo lililoweka msingi wa kwanza wa elimu Tanganyika.

Ukweli ni kuwa Wamisionari walifuata nyayo za madras na walimu wa kwanza katika shule za misheni walikuwa Waislam ambao hawakusoma katika shule za kanisa bali katika madras.

(Kutoka kitabu cha Abdul Sykes 1998).

Baada ya karne mbili Rais wa Tanzania kutoka Zanzibar anampa zawadi ya mlango wa Kizanzibari Kiongozi Mkuu wa Kanisa Katoliki Duniani ndani ya Vatican na kumweleza maneno haya:

"This is the door... " - Sultan opened for Christianity..."

Huu ndiyo mlango uliofunguliwa kwa Ukristo kuingia Zanzibar na Afrika ya Mashariki.

Kwa uongo hujambo umeeleza kuwa waislamu ndio Walikuwa wa kwanza kuelimika wakijua kusoma na kuandika Kwa herufi za kiarabu
Halafu eti walimu wa kwanza wa shule za misionari Walikuwa waislamu waliosoma madarasa.Sijawahi ona shule yeyote Wala kusikia ya Kanisa iliyowahi fundisha kiarabu darasani Cha kusoma Wala kuandika Wala kuongea
Pili kama elimu yenu Iko juu Mbona Sasa hivi madrasa Bado zipo mnaendelea nazo hiyo elimu ya juu ya madrasa ilipotelea wapi Serikali mtasingizia kuwa ilikuja misikitini kubadilisha syllabus au?
 
Unatatizo gani na dini yako ww ungekuwa Iran ungekuwa mfia dini kabisa toka nakujua jukwaa la historia unaendekeza sana ushujaa wa dini yako kuna mahi hauko sawa Ila huwezi kujua,
 
Kama mlikuwa mmeendelea kiasi hiki kielimu ilikuwaje wakristu wakawazidi?
Nan...
Nimeandika paper kadhaa kuhusu hili.
Ukoloni uliukandamiza Uislam.

Matumizi ya Arabic Script yalipigwq marufuku na badala yake matumizi ya Roman Script yakachukua nafasi.

Wamishionari na wakoloni wakawa wanatoa elimu kwa ubaguzi.

Hii ndiyo sababu Waislam wakawa mstari wa mbele katika kupambana kwanza na Wajerumani kwa silaha kisha na Waingereza kupitia vyama.

Nimeeleza haya yote katika kitabu cha Abdul Sykes.
 
Wajerumani walipofika Tanganyika waliwakuta Waislam wanafahamu kuandika, kusoma na walikuwa wameelimika katika hesabu.

Mmishionari Ludwig Krapf alipofika kwa Chifu Kimweri wa Usambaa mwaka 1848 alimkuta yeye na wanae wote wanajua kusoma na kuandika.

Krapf alikuwa na barua mkononi kutoka Zanzibar kwa Sultan Barghash ikimuomba Chief Kimweri amsaidie Krapf kwani ni "mtu wa Mungu."

Herufi walizokuwa wakitumia zilikuwa za Kiarabu.

Wajerumani kwa ajili hii basi waliwaajiri Waislam kama walimu, wakalimani na makarani serikalini.

Wamisionari na wakoloni waliona wivu kwa maendeleo haya waliyoyakuta kwa Waislam.

Kubwa zaidi ni kuwa walikuwa wamekuja kustaarabisha watu "washenzi'' badala yake wamewakuta watu walistaarabika na wanye utamaduni wa kupendeza.

Elimu hii yote na utamaduni huu wa hali ya juu ulikuwa unatokana na Uislam na elimu iliyokuwa imetolewa na madras.

Hapo ndipo zilipoaanza mbinu ya kuvunja maendeleo haya yote.

Herufi za Kiarabu zikapigwa marufuku kutumika na badala yake watu wakalazimishwa kujifunza herufi za Kirumi.

Muislam ambae jana alipoingia kulala alikuwa anaitwa ameelimika akaamka asubuhi yake mjinga, hana elimu, hajui kusoma wala kuandika.

Njama hizi zote dhidi ya Uislam ilikuwa sehemu ya makubaliano kama ilivyoandikwa katika kifungu IV cha Mkutano wa Berlin wa mwaka 1884.

Kifungu hicho kilikuwa kinasema kuwa Ukristo ni lazima ulindwe dhidi ya Uislam.

Kati ya mwaka 1888 -1892 katika kutekeleza kifungu hicho kama ilivyokubalika katia Mkutano wa Berlin, Imperial British East Africa Company ilitumia nguvu za kisiasa na kijeshi kuulinda Ukristo na taasisi zake zote katika Afrika ya Mashariki.

Ombwe lililoachwa na madrsa ikajazwa na shule zilizojengwa na Serikali na Kanisa chini ya usimamizi wa wakoloni.

Historia iliyoandikwa inasema kuwa Kanisa ndilo lililoweka msingi wa kwanza wa elimu Tanganyika.

Ukweli ni kuwa Wamisionari walifuata nyayo za madras na walimu wa kwanza katika shule za misheni walikuwa Waislam ambao hawakusoma katika shule za kanisa bali katika madras.

(Kutoka kitabu cha Abdul Sykes 1998).

Baada ya karne mbili Rais wa Tanzania kutoka Zanzibar anampa zawadi ya mlango wa Kizanzibari Kiongozi Mkuu wa Kanisa Katoliki Duniani ndani ya Vatican na kumweleza maneno haya:

"This is the door... " - Sultan opened for Christianity..."

Huu ndiyo mlango uliofunguliwa kwa Ukristo kuingia Zanzibar na Afrika ya Mashariki.

Kuna watu watakupinga tu na hawana backup evidence yoyote.
 
Unatatizo gani na dini yako ww ungekuwa Iran ungekuwa mfia dini kabisa toka nakujua jukwaa la historia unaendekeza sana ushujaa wa dini yako kuna mahi hauko sawa Ila huwezi kujua,
Git...
Sina tatizo.
Neno "kuendekeza," huwezi kulitumia kwa mtu anaetafiti na kuandika.

Haiwi kuushughulisha ubongo kuwe kuendekeza.

Wala haiwezi kuwa mtu anaeandika mada za kisomi na kuandika vitabu awe hayuko sawa.

Mtu aliyepungukiwa hana uwezo wa kufanya hayo.
 
Na Sasa hivi ajibu kwa Nini kijerumani hakifundishwi madrasa zao kama kilikuwa mojawapo ya lugha zilizofundishwa madrasa.

Mzee Mohamed Said ni Professional Liar
Sho...
Kijerumani kilifundishwa shule wakati wa utawala wa Wajerumani.
 
Back
Top Bottom