Wamisionari waliofika Tanganyika walikuta watu wamestaarabika na wanajua kusoma na kuandika

Wamisionari waliofika Tanganyika walikuta watu wamestaarabika na wanajua kusoma na kuandika

Mzee Mohammed ameanza kuandika historia ya Tanganyika mda. Na ametoa vitabu vingi ila kuna jambo linanitatiza
1. Anatumia nguvu kubwa kuiandika historia ya Tanganyika, lakini mwamko wa watanganyika kutala kujua historia ni mdogo sana, kwa nini? Je kujua historia hii kunaweza kubadilisha hali duni na kuleta maendeleo kwa watanzania?

2. Historia za mzee Mohammed zinalenga kuonyesha nguvu za waislam katika uhuru na Tanganyika. Ila mzee wetu anasahau mchango mkubwa uliofabywa na watu wengine ikiwemo machief, wasomi nk. Ila historia hii imejikita kwa waislamu na wazee wa Dar es Salaam. Je historia ya Tanganyika na uhuru wake unaletwa na waislam pekee?

Ila nataka kumpongeza sana mzee wetu Mohammed Said. Kwa kuandika historia yake kuhusu Tanganyika imeonekana kabisa kuna mapungufu makubwa kwenye historia iliyokuwepo, pia siku zote uongo hujitenga pale penye ukweli. .
 
Kwako unaona ni kitu cha kawaida Ila kwao ni endorsement moja kubwa sana,
Stow...
Kughitilafiana ni katika silka za binadamu.

Ulionavyo jambo wewe si sawa nilionavyo mimi.
Tupe link za English mzee , tusibitoshe kama kweli wewe ni msomi na Wakaloni walikukuta unajua soma na kuandika English na kijerumani
 
Mr Q,
Zipo nyingi.
Kwa nini unataka kuzisikiliza hizi za Kiingereza ilhali zipo za Kiswahili?
Interviewer wa kizungu huwa wanamaswali ya msingi unlike wa huku kwetu. Pia nataka kujifunza jambo kutoka kwenye mahojiano hayo. Naomba links
 
Mzee Mohammed ameanza kuandika historia ya Tanganyika mda. Na ametoa vitabu vingi ila kuna jambo linanitatiza
1. Anatumia nguvu kubwa kuiandika historia ya Tanganyika, lakini mwamko wa watanganyika kutala kujua historia ni mdogo sana, kwa nini? Je kujua historia hii kunaweza kubadilisha hali duni na kuleta maendeleo kwa watanzania?

2. Historia za mzee Mohammed zinalenga kuonyesha nguvu za waislam katika uhuru na Tanganyika. Ila mzee wetu anasahau mchango mkubwa uliofabywa na watu wengine ikiwemo machief, wasomi nk. Ila historia hii imejikita kwa waislamu na wazee wa Dar es Salaam. Je historia ya Tanganyika na uhuru wake unaletwa na waislam pekee?

Ila nataka kumpongeza sana mzee wetu Mohammed Said. Kwa kuandika historia yake kuhusu Tanganyika imeonekana kabisa kuna mapungufu makubwa kwenye historia iliyokuwepo, pia siku zote uongo hujitenga pale penye ukweli. .
Mnafiq sana huyo mzee na udini mwingi
 
Tupe link za English mzee , tusibitoshe kama kweli wewe ni msomi na Wakaloni walikukuta unajua soma na kuandika English na kijerumani
Chi...
Kama kweli mimi ni msomi.
Unaniuliza.

Wamishionari ndiyo waliokunikuta mimi najua kusoma na kuandika.

Wakoloni walikuja baadae.

Huyo aliyekuwa anajua kusoma na kuandika ni Chief Kimweri.

Unataka kuipima elimu yangu kutokana na ujuzi wa lugha ya Kiingereza?

Mbona hicho si kipimo?
 
Interviewer wa kizungu huwa wanamaswali ya msingi unlike wa huku kwetu. Pia nataka kujifunza jambo kutoka kwenye mahojiano hayo. Naomba links
Mr. Q,
Mimi nimezungumza Vyuo Vikuu.
Hapo unaalikwa utoe mada kisha maswali na majibu.

Vyuo Vikuu haviwafanyii watu mahojiano wao hualika wasomi kuja kuzungumza na walimu na wanafunzi.
 
Mzee mzushi na mnafiki mtaalamu wa kupindisha historia,pasina kujia hata hii elimu aliipata kwenye shule za kanisa,hii vita mzee huiwezi utakufa na life litaendelea huku ukristo ukiendelea kutamalaki pole sana kwa kupoteza muda wako kupigania kisicho na faida

Kila goti litapigwa mbele ya kanisa.
 
Unahitajika ufafanuzi kuhusu kiapo na kuhusu kile kitabu chenye blue cover.

Hii ni kama imemhusu Mheshimiwa na Pope tu.

Wajumbe walikuwa huko wakishangaa mabomba yanayotoa mvinyo badala ya maji.
 
Mr. Q,
Mimi nimezungumza Vyuo Vikuu.
Hapo unaalikwa utoe mada kisha maswali na majibu.

Vyuo Vikuu haviwafanyii watu mahojiano wao hualika wasomi kuja kuzungumza na walimu na wanafunzi.
Mkuu yani mi nipo nje ya mada hii nacho omba ni hizo links za interview zako nipate kujifunza mawili matatu. Pia kama una documentaries speeches n.k ndio mambo nayo yataka kwa kujifunza tu and fir inspirations
 
Hiyo kumuona Papa yenyewe nasikia imezidi sana 30 - 45 minutes, ukitoka hapo unaenda kuongea na wasaidizi wake. Hiyo ni kama unaenda kumsalimia TU. Kukaa naye muda mrefu labda wakienda kina putin
 
Mkuu yani mi nipo nje ya mada hii nacho omba ni hizo links za interview zako nipate kujifunza mawili matatu. Pia kama una documentaries speeches n.k ndio mambo nayo yataka kwa kujifunza tu and fir inspirations
Mr. Q,
Inakisiwa nina makala zipatazo 10,000.

Hizi zipo JF, FB na You Tube.

Nina makala nyingine hapa: mohamedsaidsalum.blogspot.com.

Nina makala nyingine hizi ndizo za mwanzo miaka ya 1980s Library of Congress, Washington DC.

Nilipoanza kuandika nilikuwa naandika kwa Kiingereza.

Baadae nikabadili nikaanza kuandika kwa Kiswahili.

Nina makala nyingi wala sijui idadi yake katika magazeti haya: Annur, Rai, Mwananchi, Raia Mwema, Mtanzania na The East African.

Makala nyingine zipo Uingereza: Africa Events na New African (London).

Ninazo papers muhimu za mada nilizozungumza Vyuo Vikuu Tanzania na nje ya mipaka yake, Kenya, Afrika Kusini, Nigeria, Ujerumani na Marekani.
 
Hahaha
Unataka kusema nini?

Kuwa vitabu vyake vya kizungu kaandikiwa?

Au hajawahi kuhojiwa na VoA?

Sijajua mantiki ya hii.
Longo longo na Ujanja Mwingi! Anafikiri humu kuna mamuma wa kuwaongopea aweke link tuzione
 
Wajerumani walipofika Tanganyika waliwakuta Waislam wanafahamu kuandika, kusoma na walikuwa wameelimika katika hesabu.

Mmishionari Ludwig Krapf alipofika kwa Chifu Kimweri wa Usambaa mwaka 1848 alimkuta yeye na wanae wote wanajua kusoma na kuandika.

Krapf alikuwa na barua mkononi kutoka Zanzibar kwa Sultan Barghash ikimuomba Chief Kimweri amsaidie Krapf kwani ni "mtu wa Mungu."

Herufi walizokuwa wakitumia zilikuwa za Kiarabu.

Wajerumani kwa ajili hii basi waliwaajiri Waislam kama walimu, wakalimani na makarani serikalini.

Wamisionari na wakoloni waliona wivu kwa maendeleo haya waliyoyakuta kwa Waislam.

Kubwa zaidi ni kuwa walikuwa wamekuja kustaarabisha watu "washenzi'' badala yake wamewakuta watu walistaarabika na wanye utamaduni wa kupendeza.

Elimu hii yote na utamaduni huu wa hali ya juu ulikuwa unatokana na Uislam na elimu iliyokuwa imetolewa na madras.

Hapo ndipo zilipoaanza mbinu ya kuvunja maendeleo haya yote.

Herufi za Kiarabu zikapigwa marufuku kutumika na badala yake watu wakalazimishwa kujifunza herufi za Kirumi.

Muislam ambae jana alipoingia kulala alikuwa anaitwa ameelimika akaamka asubuhi yake mjinga, hana elimu, hajui kusoma wala kuandika.

Njama hizi zote dhidi ya Uislam ilikuwa sehemu ya makubaliano kama ilivyoandikwa katika kifungu IV cha Mkutano wa Berlin wa mwaka 1884.

Kifungu hicho kilikuwa kinasema kuwa Ukristo ni lazima ulindwe dhidi ya Uislam.

Kati ya mwaka 1888 -1892 katika kutekeleza kifungu hicho kama ilivyokubalika katia Mkutano wa Berlin, Imperial British East Africa Company ilitumia nguvu za kisiasa na kijeshi kuulinda Ukristo na taasisi zake zote katika Afrika ya Mashariki.

Ombwe lililoachwa na madrsa ikajazwa na shule zilizojengwa na Serikali na Kanisa chini ya usimamizi wa wakoloni.

Historia iliyoandikwa inasema kuwa Kanisa ndilo lililoweka msingi wa kwanza wa elimu Tanganyika.

Ukweli ni kuwa Wamisionari walifuata nyayo za madras na walimu wa kwanza katika shule za misheni walikuwa Waislam ambao hawakusoma katika shule za kanisa bali katika madras.

(Kutoka kitabu cha Abdul Sykes 1998).

Baada ya karne mbili Rais wa Tanzania kutoka Zanzibar anampa zawadi ya mlango wa Kizanzibari Kiongozi Mkuu wa Kanisa Katoliki Duniani ndani ya Vatican na kumweleza maneno haya:

"This is the door... " - Sultan opened for Christianity..."

Huu ndiyo mlango uliofunguliwa kwa Ukristo kuingia Zanzibar na Afrika ya Mashariki.

Cry me a river
 
Back
Top Bottom