Wamisionari waliofika Tanganyika walikuta watu wamestaarabika na wanajua kusoma na kuandika

Wivu wa nini? Walijua kukariri Quran. Anyway baada ya hapo? Ni Mikoa gani ambayo ipo Duni kielimu? Tuache kujifariji. Wamisionari waliwekeza kwenye Elimu. Kila walipojenga Kanisa walijenga na Shule na Hospital. Ndo umekuwa mfumo wao mpaka leo. Shule nyingi ni za Kanisa na Vyuo. Waislamu hata walicho nacho walipewa na Serikali. Tuache kuongea uongo wa kujifariji. Na kukaa kulalamika lalamika miaka yote
 


PATA ZAWADI YAKO YA PASAKA MAPEMA HII



View: https://www.youtube.com/watch?v=XfEBl66mYAE
 
Chizi...
Wivu na hasad ilisababishwa na kukuta ustaarabu kinyume na walivyokuwa wakiamini kuwa wanakwenda kukutana na washenzi.

Pwani yote ya Afrika ya Mashariki Uislam ulikuwa umeenea na watu wakijua kusoma na kuandika.

Kubwa walijua hadi kanuni za afya.
Wanawaona Waislam wakiwa nadhifu na wasafi kwa nguo na miili yao.

Wakioga na kutumia maji wanapokwenda haja na kabla ya kusali wakitawadha.

Wanawake wao wakijua kujipara na kutumia utuli.

Na mengine mengi.
Haya yaliwashangaza.

Afrika waliofika hawa wamishionari haikuwa "Dark Continent."

Sasa hilo la ujenzi wa shule na hospitali nimelieleza mara nyingi kuwa Waislam walijenga shule katika ukoloni na wakoloni wakishirikiana na wamishionari walijenga shule lakini elimu ilitolewa kwa kuwabagua Waislam.

Baada ya ukoloni kuondoka na Tanganyika kuwa huru EAMWS iliendelea kujenga shule na kuazimia kujenga Chuo Kikuu.

EAMWS ikapigwa marufuku ikaundwa BAKWATA na huu ndiyo ukawa mwisho wa miradi yote ya elimu ya Waislam.
 
Wenzetu wanawekeza kwenye mambo ya msingi....ila kuna sisi watz tupo bize na porojo za ukoloni😂
Very sad....nadhani mzee Mohamad said angetumia pia muda wake kuelezea historia hiyo itusaidieje kwa huu mkwamo wa kimaendeleo katika jamii hasa ya kiislam.....kwa sababu tumelalamika muda mrefu, hata lengo la maandishi ya mzee huwa halieleweki kwa kweli nimesoma muda mrefu sana ila hata sielewagi. As a Muslim sometimes let our society ikubali tu kuwa tulipoacha misingi ya uislam adui zetu walituponda ponda na kutusambaratisha sasa kubaki kulilia historia hata haitusaidii, manaake kila mara utasikia mfumo kristo na blah blah za hapa na pale lakini hakuna viongozi wa kiislam ambao wapo tayari kuipambania jamii ya kiislam kwa dhati.......sasa hilo ni kosa la adui au letu....???? historia ambayo inaiongelea juu ya ustawi na ustaarabu wa jamii ya kiislam kwa ushahidi wa miji na athari nyengine hasa kwa pwani ya Afrika Mashariki ni very insignificant kwa hivi sasa........kwani maeneo mengi ambayo yananasibishwa na uislam yana changamoto nyingi sana za kijamii....japo kwa nchi kama Tanzania relative poverty ipo dispersed kulingana na eneo hivyo kwa kusema hivyo pia hatuwezi sema jamii ambao si waislam basi ni matajiri....kilichopo ni kuwa as Muslim community we are crying so much na wakatinwe have so much potentials na historia inatubeba.
 

Kiongozi ni mtu kama wewe , ingalipendeza zaidi wewe ukaanza kuwa kama kiongozi ukaanza hizo jitihada , usisubiri watu
 
Ustaarabu ni very subjective. Bahati nzuri mimi nimekulia Kibiti (Kanyenye) nmesoma pale pia. Naufahamu kiasi Uislamu. Siwezi jisifu sheikh. Ndo maana nasema kiasi. Ila nashukuru Mungu nimefunguka nilifanikiwa kupata ilimu ya kunifungua ufahamu. Since then i have been so free. Like a bird on a tree.
 
Mzee unajua unachoteteaga hata hakijulikaniki, KINDLY hebu elezea historia hii ambayo wewe umeiandika inasaidia nini jamii ya kiislam kwa sasa. Mufti aliwahi ongea kuwa sisi karibia kila kitu tumepewa na serikali, please it will be worthy to explain how Muslim can re write the History.....bora hata akina Sheikh Illunga walikuwa wanaelekeza nini cha kufanya.....your history explanation is based more on lamentations......ndiyo maana licha ya kuwa imekupatia tuzo mbali mbali lakini haijawa na athari katika jamii......na ukumbuke waliothiriwa na athari za ukoloni au mifumo dhalimu si Waislamu pekee ni jamii kwa ujumla, ukiangalia Mtume S.A.W alileta ukombozi kwa jamii yote.....hata wasiokuwa Waislamu walineemeka kutokana na mfumo wa kiislam, sasa hizi stori za akina Sykes n.k perhaps hata wao hawakuwa smart kama waliacha kila walichokipigania kikapotea from know where....walipokuwa wanaanzisha project ya uhuru wa nchi hii what was their mission.....??? mostly ukiangalia historia ambayo waislamu huwa tunaelezea ni kuwa tu how smart we were before colonialism na historia huwa inajirudia mbona still today we have many flaws.....ina maana katika ramani ya kutafuta uhuru wetu akina Sykes walikuwa hawana options mbalimbali based on situation changes mpaka waikristo kupitia Nyerere wakachukua kila kitu ilhali waanzilishi walikuwa waislam....???
 

Yaani mzungu akujengee shule , wewe nani kwake ??

Slaves for God's Glory




"Never let them get above themselves. It should be their aim to be better slaves, for the glory of God ...


And they are NOT to set their hearts on gaining their liberty at the church's expense, for then they only become slaves to their own longings."


– St Ignatius Letter. to Polycarp, 4.
 
Kiongozi ni mtu kama wewe , ingalipendeza zaidi wewe ukaanza kuwa kama kiongozi ukaanza hizo jitihada , usisubiri watu
Hapana mkuu, mimi ni kiongozi katika level ndogo sana.....level ya familia yangu, na katika misingi ya kiislamu bado sijafikia level ya kuongoza kundi la watu.....uislam una miiko yake katika uongozi. Hoja yangu kubwa ni kuwa historia hii aliyoandika na kuitangaza mzee wetu Mohamed Said lengo lake hasa ni nini...?? both kwa ustawi wa iman yetu na jamii kwa ujumla, kwa sababu kusema tu Waislamu walianzisha harakati za uhuru na blah blah nyengine then what.....by the way ni fault ya wazee wake.....ina maana hawakujipanga vizuri kiasi ambacho waandika historia wakawazidi maarifa.
 
Je sultani alikuwa ni Mkoloni?
 
Ooooh... Walijenga waarabu... Nimekumbuka.
 

hakuna level ndogo , ndio ujitahidi ufike level kubwa kama wewe kweli unalo lengo la kuuinua uislamu. Histoaria hiyo kwako kwa vile level yako ni ndogo ndiyo maana ukawa na mawazo finyu sana kuhusu uislamu na waislamu tanganyika na inaelekea huvijui vita tunavyopigwa na makafiri
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…