Wamisionari waliofika Tanganyika walikuta watu wamestaarabika na wanajua kusoma na kuandika

Wamisionari waliofika Tanganyika walikuta watu wamestaarabika na wanajua kusoma na kuandika

Uhuru wa Tanganyika
Vishu...
Mwaka wa 1950 uongozi wa TAA uliunda TAA Political Subcommittee na wajumbe wake walikuwa hawa: Dr. Vedasto Kyaruzi (President), Abdulwahid Sykes (Secretary), Hamza Mwapachu, Mufti Sheikh Hassan bin Ameir, Sheikh Said Chaurembo, Steven Mhando na John Rupia.

Mshauri wa mambo ya Mandate Territories alikuwa Earle Seaton.

Kamati hii ndiyo iliyoongoza TAA hadi kufikia kuunda TANU 1954.
 
Mpw...
Kwani nini chanzo cha matatizo ya NECTA?
Waislam ndio walikuwa wanasema wana matatizo na NECTA, sasa unashangaza kuniuliza mimi?

Ndalichako alitoka, bado wewe ukasema hata aliyebaki ni wale wale (Msonde).

Ndio maana kwasasa nimekuuliza, bado Kuna tatizo au limekwisha?
 
Waislam ndio walikuwa wanasema wana matatizo na NECTA, sasa unashangaza kuniuliza mimi?

Ndalichako alitoka, bado wewe ukasema hata aliyebaki ni wale wale (Msonde).

Ndio maana kwasasa nimekuuliza, bado Kuna tatizo au limekwisha?
Mpwi...
Ningependa kuona nilikosema maneno hayo.
 

Attachments

  • Screenshot_20240217-073202.png
    Screenshot_20240217-073202.png
    177.6 KB · Views: 6
👇👇👇
Wewe Mpimbwe wa Kibaoni,Use ya, Majimoto, Kasansa au wapi? Mbona mtata hivyo wakati sisi wapimbwe sio watata hivyo? Umemvua nguo mzee wa watu. Atajaa upepo kwa maana huwa anajaa sana upepo. Nilimuona Azam TV kwenye mahojiano kuhusu Uhuru. Alitokota.
 
Ingekua amri yako Wakristo wasingekwepo nchi hii. Ila ndio hivyo Mungu sio Athumani.
 
Wewe Mpimbwe wa Kibaoni,Use ya, Majimoto, Kasansa au wapi? Mbona mtata hivyo wakati sisi wapimbwe sio watata hivyo? Umemvua nguo mzee wa watu. Atajaa upepo kwa maana huwa anajaa sana upepo. Nilimuona Azam TV kwenye mahojiano kuhusu Uhuru. Alitokota.
Jimm...
Husemi kweli na unajua husemi kweli.

Nina nafasi yangu katika uandishi na mijadala.

Hapa nina tuzo za Uandishi Bora.

Nisingetunukiwa heshima hiyo ningekuwa kama hivyo usemavyo nilivyo.

Wala sijapata aibu ya kuvuliwa nguo na yeyote si hapa wala si katika majukwaa mengine duniani niliposimama kuzungumza.
 
Ingekua amri yako Wakristo wasingekwepo nchi hii. Ila ndio hivyo Mungu sio Athumani.
Mag...
Unasema haya kwa kuwa nimeandika historia ya kweli ya uhuru wa Tanganyika na kuonyesha mchango wa Waislam?
 
Yaani hili zee ni jinga sana, ila ni wakati wao acha awajaze wenzie upepo waingie kingi
Nan...
Sikutegemea utaghadhibika kiasi hiki cha kunitukana.

Mimi sichukii kuitwa mzee kwani hakika mimi si kijana tena.

Namshukuru Mwenyezi Mungu kwa kunifikisha umri huu.

Na hakika nilikuwa kijana khasa kwa kila kitu kuanzia mavazi hadi uwezo Mungu alinipendelea si wengi aliwapa nema aliyonipa mimi.

Niko Piccadilly Circus London, Niko Edinburgh Castle Glasgow, niko Tahrir Square Cairo, Eiffel Tower Paris, Soweto Johannesburg kwingi sana Central Park New York kwingi...

Machava Stadium Maputo, United Nations Geneva, Kalakuta Republic Lagos...

Montaza Palace Alexandria.
Ulipokuwa ukuta wa Berlin.

Makka na Madina.

Nasingepata haya kama Allah asingenipa umri hadi kufikia uzee miaka 72 juma lijalo In Shaa Allah.

Nasikitika kuwa unanitukana, "hili lizee."

Ungeweza hata kusema huyu mzee.

Sijui kutukana wala sijazoea kutukanwa.

Kwetu ni fedheha.

Lakini naamini mama yako ni umri wangu na kakufunza adabu.

Angalia usimtukanishe baba yako.
 
Kweli


Wajerumani walipofika Tanganyika waliwakuta Waislam wanafahamu kuandika, kusoma na walikuwa wameelimika katika hesabu.

Mmishionari Ludwig Krapf alipofika kwa Chifu Kimweri wa Usambaa mwaka 1848 alimkuta yeye na wanae wote wanajua kusoma na kuandika.

Krapf alikuwa na barua mkononi kutoka Zanzibar kwa Sultan Barghash ikimuomba Chief Kimweri amsaidie Krapf kwani ni "mtu wa Mungu."

Herufi walizokuwa wakitumia zilikuwa za Kiarabu.

Wajerumani kwa ajili hii basi waliwaajiri Waislam kama walimu, wakalimani na makarani serikalini.

Wamisionari na wakoloni waliona wivu kwa maendeleo haya waliyoyakuta kwa Waislam.

Kubwa zaidi ni kuwa walikuwa wamekuja kustaarabisha watu "washenzi'' badala yake wamewakuta watu walistaarabika na wanye utamaduni wa kupendeza.

Elimu hii yote na utamaduni huu wa hali ya juu ulikuwa unatokana na Uislam na elimu iliyokuwa imetolewa na madras.

Hapo ndipo zilipoaanza mbinu ya kuvunja maendeleo haya yote.

Herufi za Kiarabu zikapigwa marufuku kutumika na badala yake watu wakalazimishwa kujifunza herufi za Kirumi.

Muislam ambae jana alipoingia kulala alikuwa anaitwa ameelimika akaamka asubuhi yake mjinga, hana elimu, hajui kusoma wala kuandika.

Njama hizi zote dhidi ya Uislam ilikuwa sehemu ya makubaliano kama ilivyoandikwa katika kifungu IV cha Mkutano wa Berlin wa mwaka 1884.

Kifungu hicho kilikuwa kinasema kuwa Ukristo ni lazima ulindwe dhidi ya Uislam.

Kati ya mwaka 1888 -1892 katika kutekeleza kifungu hicho kama ilivyokubalika katia Mkutano wa Berlin, Imperial British East Africa Company ilitumia nguvu za kisiasa na kijeshi kuulinda Ukristo na taasisi zake zote katika Afrika ya Mashariki.

Ombwe lililoachwa na madrsa ikajazwa na shule zilizojengwa na Serikali na Kanisa chini ya usimamizi wa wakoloni.

Historia iliyoandikwa inasema kuwa Kanisa ndilo lililoweka msingi wa kwanza wa elimu Tanganyika.

Ukweli ni kuwa Wamisionari walifuata nyayo za madras na walimu wa kwanza katika shule za misheni walikuwa Waislam ambao hawakusoma katika shule za kanisa bali katika madras.

(Kutoka kitabu cha Abdul Sykes 1998).

Baada ya karne mbili Rais wa Tanzania kutoka Zanzibar anampa zawadi ya mlango wa Kizanzibari Kiongozi Mkuu wa Kanisa Katoliki Duniani ndani ya Vatican na kumweleza maneno haya:

"This is the door... " - Sultan opened for Christianity..."

Huu ndiyo mlango uliofunguliwa kwa Ukristo kuingia Zanzibar na Afrika ya Mashariki.

Mzee
Wanting said kweli uankaha na kuamua kuandika uongo HV unapata faida gani kuandika na kupotsha ukweli mm Nina hakika huyu sultani alikuwa hajui kusoma Wala kuandika na madrasa haijawai kufundusha watu kuandika na kusoma

Tunashukuru snaa wazungu kwa kutuleteaa elimu leo hi usinge andika chochote kitu
 
Nan...
Wamisionari mfano wa Johann Krapf wamekuja Afrika wakiita Dark Continent wakiamini wanakuja kuwastaarabisha watu waliokuwa washenzi hawana mila, desturi wala historia.

Krapf alipofika Zanzibar akapewa barua na Sultan Barghash ampelekee Chief Kimweri Vuga.

Anafika Vuga Chief Kimweri anaipokea barua na anaisoma.

Barua imeandikwa kwa Arabic Script.

Chief Kimweri yuko katika Barza yake anahukumu kesi na anajua kusoma na kuandika na ni Muislam anamuamini Mungu Mmoja.

Alikotoka kwao Ujerumani kaacha shule Vuga anakuta madrasa zinasomesha watoto zile 3Rs, yaani Reading, Writing na Arithmetic.

Liko wapi hilo Black Continent.

Haliko Zanzibar wala Vuga kote kakuta utawala unaoendesha serikali na raia wanatii hizo mamlaka.

Ikiwa hujaelewa usione tabu kuuliza.
[/QUOTEUongo on

Uongo huu
 
Kweli
Mzee
Wanting said kweli uankaha na kuamua kuandika uongo HV unapata faida gani kuandika na kupotsha ukweli mm Nina hakika huyu sultani alikuwa hajui kusoma Wala kuandika na madrasa haijawai kufundusha watu kuandika na kusoma

Tunashukuru snaa wazungu kwa kutuleteaa elimu leo hi usinge andika chochote kitu
Goroko,
Kimweri akijua kusoma na kuandika hili halina shaka soma paper ya Ushumi iko East Africana Maktaba ya Chuo Kikuu Cha Dar-es-Salaam.

Ishumi alikuwa mhadhiri Department of Education, Chuo Kikuu Cha Dar-es-Salaam.
 
Back
Top Bottom