Kwa kurudisha Treni ya mkoloni??? Wewe una akili au? Yaani karne hii ya 21 unasifia treni ya Mwaka 1900 huko inayotumia masaaa zaidi ya 20 kufika Arusha tu hapo?
Kweli CCM vilaza sana!!!
Hapo vipi!
Ni kwa muda mrefu Arusha imezorota kimaendeleo,mpaka vimikoa vidogo vinakua kasi ukilinganisha na Arusha yenye fursa nyingi za kiuchumi.
WanaArusha nyie ni mashaidi juu ya kupwaya na kulala kwa fursa mbalimbali zilizopo katika mkoa wa Arusha.
Arusha kama miaka kumia imegeuzwa na wapinzani kama ndio kitovu cha harakati na sehemu ya kuanza kumwaga damu eti kwa lengo la ukombozi.Arusha imekuawa na historia mbaya ya machafuko ya kisiasa, maana yake, wapinzani wamebadilisha image ya kutoka mji wa kistaarabu na tulivu na kuwa kitovu cha machafuko ya kisiasa.
Tunakumbuka Arusha kwa miaka ya nyumba ilikuwa ni mji ambao serikali ilipendekeza kufanyia mikutano yake ya kimataifa kwasababu ni mji ambao una hali ya hewa nzuri na hotel za kutosha za zenye hadhi ya kimataifa.
Ila baada ya machafuko haya ya kisiasa, imefuta kabisa mambo kama haya ambayo pia ilikuwa inasababishs mzunguko wa pesa hapa mjini.
Pia sekta ya utalii imepwaya sana,watalii ambao ni wazungu wanaogopa sana kufanya utalii maeneo ambayo yanamachafuko ya kisiasa,hivyo hali hii imesababisha watalii kupungua sana katika mkoa wa Arusha, mikutano ya East Afrika mara nyingi huwa inafanyia Dar..badala ya Arusha ambayo ndio ilikuwa makao makuu ya East Afrika. Hizi nilizotaja ni fursa chache tu kati ya fursa nyingi zilizopotea katika mkoa wa Arusha.
Kitendo cha Rais Magufuli kufufua Reli na kufikisha Arusha,tafsiri yake ana imani na fursa zilizopo katika mkao huu,Hivyo tukiifuta hichi chama chenye kuleta machafuko hapa mjini itakuwa tumemrudishia asante Rais Maghufuli na serikali yake itaanza kuipa Arusha hadhi yake kama jiji la kiamataifa Tanzania.
Hawa wapinzani hawajawahi kuleta maendeleo yeyote hapa Arusha, zaidi ya kusababisha mkoa huu udumae kama Kilimanjaro. Kwa anayebisha ataje maendeleo yaliyoletwa na Lema na chama chake.
Hizo barabara zilizojengwa ndani ya mji wa Arusha ambayo chadema inatumia kama ngao,ya kuwadanganyia hao wafuasi wake ni project ya World Bank iliyoanza kipindi cha Kikwete.
Ni YEYE Magufuli2020#
Mkakati wa Kuuhujumu Mkoa wa Arusha ulianza baada ya Uhuru sio leo wala Jana .
Ni ukweli usiopingika hata Azimio la Arusha la kuwafilisi matajiri halikuanza kwa bahati Mbaya.
Ni mkakati wa CCM kuwafilisi Matajiri binafsi na kuhakikisha uchumi na Kodi za nchi zinawanufaisha wanasiasa na Makada wa CCM wanaoshika madaraka.
Arusha ndio Mkoa Pekee wenye Matajiri ambao sio Viongozi wa serikali. Ni watu wanaojituma wenyewe kwa kazi na biashara binafsi.
Tajiri nje ya siasa wanaiumiza sana CCM jambo linalowapa mashaka na kuwanyima usingizi ni kuwaona watu wanatajirika bila kuwalamba miguu viongozi wa CCM na serikali yake.
Kutokana na hofu hiyo ya kutokea Matajiri nje ya mfumo wa kiutawala ndio maana CCM na serikali yake haikubaliki Arusha ,Mara ,Mbeya ,Dar es salaam, Mwanza, Kagera, Morogoro Vijijini ikiwemo,Mikumi,Kilombero, Mahenge ,Pemba, Singida vijijini na maeneo yote yenye wafanyabiashara wasiotaka kuhusika kwenye siasa Chafu za CCM. Matokeo yake ni Serikali kuamua kuwakomesha kwa kuwanyima miundo Mbinu na kutumia vikundi vya Kisabaya kuwapora Mali zao na kuwabambika makesi na hata kuwabambika kodi kubwa.
Huu unyama na dhulama sasa basi.
Tunataka serikali itakayoweka mazingira ya haki kwa wote ,tajiri na maskini bila kupora Mali ya MTU wala kumfurahisha binadam mmoja kwa kumuumiza mwingine asiye na hatia kwa sababu tu ya kutaka kupata Kura na madaraka.
CCM kwa miaka mingi wamepata uongozi kwa dhulma.
Arusha Kwa miaka mingi CCM na serikali yake wamekua wakilazimisha ushindi kwenye Udiwani,serikali za mitaa,Ubunge na hata Urais ili tu waendelee kugawana mapesa waliyokuwa wanakusanya kwenye halmashauri na udanganyifu mkubwa waliokuwa wanaufanya Tangu Uhuru na kuzoea kuwatumia madiwani wa chama kimoja kuvuruga mopango ya kweli na endelevu ya miji.
Baada ya kuona kuwa Chadema imeweza kudhibiti mapato ya halmashauri ya miji na majiji kitumiaka vibaya kama CCM ilivuozoea kula ndio maana wakaamua kudhibiti tena mapato ya halmashauri ili yakusanywe Arusha halafu yakatumike kununua Kuku au yatumike anapotaka MTU mmoja kwa manufaa yake ya kupata kura na kuteua watu wa nyumbani kwake na marafiki zake huku Arusha na mikoa niliyoitaja yenye watanzania waliojiajiri na wanaolipa kodi wakibaki kuomba na kupiga magoti na kusujudu ili wapewe maendeleo hata ya kuchimba mitaro.
Cha ajabu jakuna hata nafasi na sheria inayowafanya Matajiri kujenga hata dispensary kwa manufaa yao bila kusujudu tena na kupata ruhusa kwa hao hao wanaowanyima maendeleo ya kodi zao.
Ni mzunguko wa dhulma na mateso na uhuni na unyanyasaji mkubwa ili mwisho walazimishe kuchagua CCM eti watawapa hisani ya maendeleo.
Ninaichukia CCM kwenye hii tabia ya kujikweza kuliko Mungu muumba wa utajiri wote wa asili uliopo Tanzania.
Utafikiri waliumba mlima Kilimanjaro au Mbuga za Manyara na Serengeti ,utafikiri madini ya Tanzanite yameletwa na CCM.
Vurugu zote za kisiasa nchini na kokote Duniani hua zinasababishwa na vyama vinavyotawala.
Hivi Arusha wapinzani wanaletaje vurugu kama uchaguzi unafanyika kwa haki, wazi , na kwa huru bila kuleta mambo ya kihuni huni ya kujaribu kubadili matokeo. Kuchelewa kutangaza matokeo ambayo yapo wazi aliyeeshinda ni mpinzani.
Kwa nini Tume ilazimishe kumfurahisha MTU mmoja na kuacha huzuni na chuki kwa Malaki na maelfu kama sio mamilioni ya watu?
CCM ndiyo Mara zote inalazimisha kushinda kwenye nafasi za umeya kwenye miji na majiji bila kujali kuwa patatokea vurugu.
Chaajabu wanafanya hayo kwa sababu tu ya kulenga maslahi.
Haki hii inatuonyesha wazi kuwa CCM ni kikundi cha watu wabinafsi wanaojiona kuwa Rasilimali za nchi hii zipo kwa ajili ya kujipatia fedha na madaraka ya nchi hii wao na familia zao na marafiki zao .
CCM wanakua tayari kufanya vurugu kama alivyosema yule mwenyekiti wa UVCCM alimradi tu wapate maslahi na madaraka ambayo yanawapa fursa ya kula kodi za watanzania kwa mishahara minono.
Ndio maana wakishashinda wanawatoa marafiki zao waliokuwa Wanafanya kazi kwenye taasisi kama vyuo vikuu na kuwapa nafasi za uteuzi wa kisiasa mana ndiko walikojiwekea maslahi mazuri kwa ubinafsi wao.