Uchaguzi 2020 Wana Arusha tumrudishieni Dkt. John Magufuli asante ya kufikisha usafiri wa treni Arusha, kwa kuifuta CHADEMA hapa mjini

Lema ajiandaye kisaikoloji kuachia jimbo la Arusha mjini.
 
Acha wongo, hivi unaweza kulinganisha Arusha na mikoa maskini Kama Dodoma au Mwanza?

Nianze na Dodoma. Hivi umewahi kupita majimbo kama Mtera,Mpwapwa. Kuona kulivyo na ukame na Shida ya maji?.

Tuache utani bwana.

Nenda Mwanza na Shinyanga mikoa iliyokaribu na Ziwa lakini hakuna maji.

Watu wanakunywa maji pamoja na mifugo. Siku nyingine Leta hoja zinazoeleweka Tajiri Tanzanite
 
Kama wewe hautaki treni, sisi wengine tunataka na tunaona umuhimu wake.
 
Mawazo yangu Naona Tungefufua Viwanda na Mashamba ya Kahawa na Ngano Kwanza tuanze Uzalishaji. Kama ni kusafirsha Watu Usafiri wa Barabara hausumbui. Ndege pia Kwa Wanaojiweza zipo daily.
 
UNA degedege wewe, ingekuwa ni hivyo basi Shemeji yako angepewa nyumba kwa kumtoa BIKRA dada yako
 
Hiyo Chadema katika majimbo yake imejenga treni ya kisasa?kama imeahajenga huko basi ndio utoe kauli kama hizi.

Kwani reli inajengwa na chama au kodi za kila mmoja hata asiye CCM. Kwa taarifa yako - kupotea kwa mikutano ni swala la mahusiano zaidi ya nchi yetu na wengine. Nchi jirani mikutano imejaa tele!! Hapa kwetu hatuendi hata mikutano ya mataifa makubwa, tunategemea kuwa na ushawishi gani wa kuwaleta hapa??

Vurugu unazozungumzia za mwaka 2015?? Mbona unazungumza kama kwamba zinatokea mpaka sasa?? Acha fitna na uzandiki. Watu wa arusha wanajitambua - ukweli ni kuwa jitihada zinazofanyika ni CCM kupunguza nguvu za wapinzani majasiri - Lema, Lissu, Esther Bulaya, Matiko na Sugu. Sema CCM inaitaka Arusha kwa sababu inahitaji Lema asiwe mbunge.

Kama CCM inaleta maendeleo sehemu yoyote - sasa achaneni na Arusha. Pelekeni maendeleo mikoa ya Dodoma, Singida, Tabora, Shinyanga, Simiyu.
 
Arusha siyo maboya. Hatupangiwi
Watu wengi mnaopiga kelele humu sio watu wa Arusha..nikukifanyisha tu..ila mngejua Arusha palivyopaya mngefikiria mara 2 mbili.Lema sio kiongozi ni mwanaharakati.
 
Miaka 30 ilipita baada ya MAFISADI PAPA kuiua reli...at last IMERUDI,hureeee!!
 
Ndio type ya makada wa CCM hii😂😂 unaisifu serikali kwa kutimiza jukumu lake la msingi.

Isifu kwakuboresha maisha ya watu. Inaonekana swala/somo zima la maendeleo hulijui.

Tikija kwenye hoja yako sasa: Ni Cjadema ndio walizuia hiyo reli isifanye kazi kipindi chote hiko? Chama gani kilichokuwa madarakani muda wote huu?
Ni Chadema ndio inayopanga hazina itoe kiasi gani kwaajili ya maendeleo ya koa na vitongoji vyake?

Yaelekea hata maana ya uwepo wa vyama vya upinzani katika sera za nchi hujui!
Kiufupi huna hoja
 
Kwa kurudisha Treni ya mkoloni??? Wewe una akili au? Yaani karne hii ya 21 unasifia treni ya Mwaka 1900 huko inayotumia masaaa zaidi ya 20 kufika Arusha tu hapo?

Kweli CCM vilaza sana!!!
Mtakula Treni?
Mkakati wa Kuuhujumu Mkoa wa Arusha ulianza baada ya Uhuru sio leo wala Jana .
Ni ukweli usiopingika hata Azimio la Arusha la kuwafilisi matajiri halikuanza kwa bahati Mbaya.

Ni mkakati wa CCM kuwafilisi Matajiri binafsi na kuhakikisha uchumi na Kodi za nchi zinawanufaisha wanasiasa na Makada wa CCM wanaoshika madaraka.

Arusha ndio Mkoa Pekee wenye Matajiri ambao sio Viongozi wa serikali. Ni watu wanaojituma wenyewe kwa kazi na biashara binafsi.
Tajiri nje ya siasa wanaiumiza sana CCM jambo linalowapa mashaka na kuwanyima usingizi ni kuwaona watu wanatajirika bila kuwalamba miguu viongozi wa CCM na serikali yake.

Kutokana na hofu hiyo ya kutokea Matajiri nje ya mfumo wa kiutawala ndio maana CCM na serikali yake haikubaliki Arusha ,Mara ,Mbeya ,Dar es salaam, Mwanza, Kagera, Morogoro Vijijini ikiwemo,Mikumi,Kilombero, Mahenge ,Pemba, Singida vijijini na maeneo yote yenye wafanyabiashara wasiotaka kuhusika kwenye siasa Chafu za CCM. Matokeo yake ni Serikali kuamua kuwakomesha kwa kuwanyima miundo Mbinu na kutumia vikundi vya Kisabaya kuwapora Mali zao na kuwabambika makesi na hata kuwabambika kodi kubwa.

Huu unyama na dhulama sasa basi.
Tunataka serikali itakayoweka mazingira ya haki kwa wote ,tajiri na maskini bila kupora Mali ya MTU wala kumfurahisha binadam mmoja kwa kumuumiza mwingine asiye na hatia kwa sababu tu ya kutaka kupata Kura na madaraka.

CCM kwa miaka mingi wamepata uongozi kwa dhulma.
Arusha Kwa miaka mingi CCM na serikali yake wamekua wakilazimisha ushindi kwenye Udiwani,serikali za mitaa,Ubunge na hata Urais ili tu waendelee kugawana mapesa waliyokuwa wanakusanya kwenye halmashauri na udanganyifu mkubwa waliokuwa wanaufanya Tangu Uhuru na kuzoea kuwatumia madiwani wa chama kimoja kuvuruga mopango ya kweli na endelevu ya miji.

Baada ya kuona kuwa Chadema imeweza kudhibiti mapato ya halmashauri ya miji na majiji kitumiaka vibaya kama CCM ilivuozoea kula ndio maana wakaamua kudhibiti tena mapato ya halmashauri ili yakusanywe Arusha halafu yakatumike kununua Kuku au yatumike anapotaka MTU mmoja kwa manufaa yake ya kupata kura na kuteua watu wa nyumbani kwake na marafiki zake huku Arusha na mikoa niliyoitaja yenye watanzania waliojiajiri na wanaolipa kodi wakibaki kuomba na kupiga magoti na kusujudu ili wapewe maendeleo hata ya kuchimba mitaro.
Cha ajabu jakuna hata nafasi na sheria inayowafanya Matajiri kujenga hata dispensary kwa manufaa yao bila kusujudu tena na kupata ruhusa kwa hao hao wanaowanyima maendeleo ya kodi zao.
Ni mzunguko wa dhulma na mateso na uhuni na unyanyasaji mkubwa ili mwisho walazimishe kuchagua CCM eti watawapa hisani ya maendeleo.

Ninaichukia CCM kwenye hii tabia ya kujikweza kuliko Mungu muumba wa utajiri wote wa asili uliopo Tanzania.
Utafikiri waliumba mlima Kilimanjaro au Mbuga za Manyara na Serengeti ,utafikiri madini ya Tanzanite yameletwa na CCM.

Vurugu zote za kisiasa nchini na kokote Duniani hua zinasababishwa na vyama vinavyotawala.

Hivi Arusha wapinzani wanaletaje vurugu kama uchaguzi unafanyika kwa haki, wazi , na kwa huru bila kuleta mambo ya kihuni huni ya kujaribu kubadili matokeo. Kuchelewa kutangaza matokeo ambayo yapo wazi aliyeeshinda ni mpinzani.
Kwa nini Tume ilazimishe kumfurahisha MTU mmoja na kuacha huzuni na chuki kwa Malaki na maelfu kama sio mamilioni ya watu?

CCM ndiyo Mara zote inalazimisha kushinda kwenye nafasi za umeya kwenye miji na majiji bila kujali kuwa patatokea vurugu.
Chaajabu wanafanya hayo kwa sababu tu ya kulenga maslahi.
Haki hii inatuonyesha wazi kuwa CCM ni kikundi cha watu wabinafsi wanaojiona kuwa Rasilimali za nchi hii zipo kwa ajili ya kujipatia fedha na madaraka ya nchi hii wao na familia zao na marafiki zao .
CCM wanakua tayari kufanya vurugu kama alivyosema yule mwenyekiti wa UVCCM alimradi tu wapate maslahi na madaraka ambayo yanawapa fursa ya kula kodi za watanzania kwa mishahara minono.

Ndio maana wakishashinda wanawatoa marafiki zao waliokuwa Wanafanya kazi kwenye taasisi kama vyuo vikuu na kuwapa nafasi za uteuzi wa kisiasa mana ndiko walikojiwekea maslahi mazuri kwa ubinafsi wao.
 
Hivi unaweza kuishukuru ATM kwa kukupatia pesa uliyoitoa? Wana Arusha Rais yeyote atayengoza TZ ni jukumu lake kujenga miundombinu kwa kodi zetu na hapaswi kushukuriwa, pesa hatoi mfukoni mwake, zinatoka kwenye kodi zetu.

SISI NDIO MABOSI TUNAMUAGIZA ANUNUE AU LAH.
 
Waniletee maji huku kwangu ninapoishi kabla ya October la sivyo kura yangu itaenda kwa HASHIM RUNGWE
 
Huu ujinga utaisha lini? Magufuli hajengi miundombinu kwa fedha zake na mkewe. Ni kodi zetu na ni wajibu wake. Kiongozi bora hapimwi kwa kigezo hicho. Amka Lumumba
Tunamrudisha madarakani kwa kuweza kutekeleza majukumu yake ipasavyo. Amefanikisha kwa zaidi ya 75%, bado tunaimani nae.
 
Mpinzani kutoka chama gani?
 
Nchi za ulaya kama ujerumani na zingine bado zinatumia treni za zamani sana na ni nchi zilizoendelea. Acheni kukaririshwa na hao viongozi wachadema ambao hata jema kwao ni baya, alafu pia hii ni treni ya mizigo sio ya abiria.
Huwezi kulinganisha na huo mkweche watu una kutu kila mahali kwenye mabehewa .Sio kweli google uone.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…