Wana JF narudia tena, haribu kabisa tiketi au karatasi yenye taarifa zako kamili

Sijui tiketi yangu siku ile niliichana au laa! Tena niliitupa pale getini,akili iliniambia niichane kabla ya kuitupa,je mikono ilitekeleza?

Hatar sana!

Halafu somo lingine andika majina yako halisi gesti,kuna faida ya utetezi unaweza kuipata kama yakitokea majanga,mfano majanga yametokea dar ukahusishwa lkn kumbe ulikuwa namtumbo so inakuwa ize wakifuatilia uko katika guest list

Huwa tunaingia pia kwenye maofisi,huwa tunasaini tukiingia ila tukitoka hatusaini mda tuliotoka,haya yanatokea ya kutokea umeonekana ukiingia ila haukusomeka wakati wa kutoka hapo vipi?

Usidharau mambo
 
Pole sana kwake. Mimi hata nikiweka vocha ya kukwangua huwa nachana. Nilielekezwaga na Afisa Upelelezi mmoja kwamba kukitokea tukio lolote kwenye kutafuta taarifa sahihi wanakusanya chochote kilichopo eneo hilo. So kwa mfano uhalifu umetokea and wakakuta vocha imekwanguliwa ndani ya eneo husika watafanya walichofanya kwa rafiki yako. Cha msingi tu awape ushirikiano watajua if he is guilty or not
 
Anasema kesho yake anashangaa kuona police wako nyumbani kwake na wakamuweka chini ya ulinzi kwa kosa la uhalifu uliotokea maeneo ya Kimara bucha.

Tiketi ya basi inahusiana vipi na uhalifu hata kama imekutwa eneo la uhalifu??

Anyway, tiketi za electronics huwa zinaacha footprint kwenye database husika iliyotumika kukata tiketi, mtandao wa simu nao hubaki na kumbukumbu...

Simu yake kama alisafiri inaacha alama za mahali alipotembelea kwenye database za mitandao ya simu...

Hakuna kesi hapo unless hii iwe togwa mixer alkasusu...
 
Ametuhumiwa kutenda kosa gani kwanza...
 
Usichoelewa ni nini?
Hebu pitia post za niliowajibu ndipo uje kuuliza maswali yako hapa.

Tatizo unasoma post kuu na kujibu wakati nilishatoa ufafanuzi kwenye baadhi ya comments
 
Hoja yako ni ya muhimu sana ila binadamu wanabadilika na wana mambo yao ya chini chini ambayo ni siri yao na Mungu wao.

Kuna watu ni wastaarabu na wema sana ila ukijasikia balaa lao baada ya kukamatwa ndipo utaamini binadam ni kiumbe hatari sana.
 
Nakumbushia na kusaini vitabu vya mahudhurio iwe kazin au sehem yoyote utakayoingia ambayo inahitaj kusaini
 
Usichane wala kuharibu hifadhi vema nyumbani mpaka ipite walau wiki hivi.. Unaweza kuihitaji pia kama ushahidi katika mazingira kama hayohayo na mengineyo
 
Du! Hawa mutual friends ni nyoko kabisa
 
Hiyo ya kuandika jina sahihi guest aisee imewahi kutokea Nairobi early 2000s sitasahau kuna raia walibebwa na kupewa kesi kubwa ya robbery sijui kama walikuja kuachiwa wale.
Tupe mkasa kidogo
 
Usichoelewa ni nini?
Hebu pitia post za niliowajibu ndipo uje kuuliza maswali yako hapa.

Tatizo unasoma post kuu na kujibu wakati nilishatoa ufafanuzi kwenye baadhi ya comments

Tatizo ni kwamba you're not a logical thinker kama hao polisi tu, naona umeshindwa kuelewa comment yangu kwamba polisi hawajawaza nje ya boksi wametumia shortcut kama kawaida yao...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…