Wana JF narudia tena, haribu kabisa tiketi au karatasi yenye taarifa zako kamili

Kabisa, Mimi Hakuna namna nitaitwa Police nisiende, tena wakisema niende kesho wala sitalala, I want to get over issues haraka, na wala sina mtu wa kuniteka!

Kuna dogo Mmoja niliambiwa ameiba Milioni Tatu. Sasa Kwa jinsi Mimi ninavyomjua Yule dogo nikawa namtetea. Yule boss akaniambia "Robert wewe hujui. Mimi mtu mzima nimeona wezi wa aina nyingi. Huyu dogo sio wakwanza"
Dogo hataki kwenda kwa Boss, tumemuitia Polisi katoroka kwao.

Hapo ndio nikaanza kuwa na mashaka, wazazi wake Wanamtetea kuwa hakukimbia kwa sababu ya wizi Bali Sababu ya hofu ya Polisi.

Polisi wakaishia kucheka tuu. Siku mbili zilizofuata, dogo Akiwa na Wazazi wake wakaleta Milioni mbili na Laki Moja na nusu wakasema hizo zingine wataleta kidogokidogo. Kwani dogo amezitumia.

Yaani yule dogo alinifundisha Jambo Moja, usimpime mtu Kwa kumwangalia
 
Enzi hizo kama 20yrs ago niko nchi za watu nilinunua simu ya dili. Nina rafiki yangu alikuwa mwingi kidogo. Alikuwa na rafiki zake Wapakistan. Wale walikuwa wanaiba simu kutoka warehouse inayohifadhi handset za kampuni fulani wa simu. Moja ya hio simu,very latest and expensive nikauziwa mimi.
Siku moja nikapokea simu mtu akajitambulisha ni polisi kutoka investigation unit blah blah. Akanitaja kwa majina,akataja simu ninayotumia na akaniuliza umeipata wapi. Nikamwambia nimenunua lkwa mtu ambae nilikuwa introduced na rafiki yangu. Akasema sawa,hio simu ni ya wizi na ni sehemu ya uchunguzi wa uhalifu mkubwa. Kwasababu umetoa ushirikiano endelea kutumia. Akakata simu. Alipokata tu simu nikaachana na ile simu na hawakujitafuta tena. Baadae nilisikia wale vijana Wapakistan walikula miaka 7 jela.
Sasa hapa unaona polisi wanaojua kazi yao. Ingekuwa hapa Tz sijui ingekuwaje.
 
Tuseme hivi, kujiunga na jeshi la polisi kiwango cha chini kabisa ni degree kutoka chuo kinachotambuliwa.
Unafikiri wale wapelelezi ni wajinga hawakwenda shule? Ukiwa na kesi inayohitaji upelelezi utajua kuwa wanajua wanachofanya.
Polisi wana vitengo,kuna vitengo tofauti.
 
Hata vocha oliyotumika
 

Ninaelewa kwamba kila kinachokutwa kwenye crime scene kinaweza tumika kuanzisha mchakato wa upepelezi...

Sasa kwenye tukio la uvamizi na ujambazi kama ilivyoelezwa na mleta mada, kitu pekee kinachomuunganisha jamaa na huo uhalifuni ni uwepo tu wa karatasi "inayodhaniwa" kuwa ni tiketi ya basi...

Polisi walipaswa wajue kwanza uhalali wa hiyo tiketi,

1. Je ni halisi au imenakiliwa?

2. Huyu mtu alisafiri, je huko alipokwenda si alikutana na watu, hao watu wanaweza kuthibitisha uwepo wake huko?

3. Kwenye database za makampuni ya telecom, simu huwa zinaacha kumbukumbu ikiwemo periodic locations wakati inapohama mahali hadi mahali, polisi wangeweza kutumia hili pia...

Polisi inapokamata mtu inabaswa iwe na ushahidi wa kutosha usio na shaka, hatua ya ukamataji iwe ni ya mwisho.
Sasa Bongo unapata mtu anakamatwa, halafu unaambiwa upelelezi unaendelea ili mradi tu wamtie mtu lupango wamtese kulazimisha akiri makosa...
 
Ohh, kumbe.
Basi sisi tukajua hawa mutual wametumika kumlengesha
Kuna njia mbalimbali za kiuchunguzi za kuweza ku-trace na ku-track Watu au Wahalifu. Zipo njia nyingi sana,
 

Eboh! mbona una panic na kupangia watu vitu vya kuandika...

Wewe si ndiye uliyeleta kisa cha maisha ya mtu mwingine hapa tujadili tukio lake πŸ˜‚
 
Kuna kitu kinaitwa alibi. Na sio mara zote kisapotiwe na rafiki zako, siku hizi kuna smartphone ambayo inaweza kutumika kujua ulikuwa wapi na wakati gani.

Najua kwasababu sio kada atapata shida, lakini ni jambo dogo sana hilo, kama una alibi mzuri na kuna namna ya kuisupport either physically au digitallly unakwepa hizi mambo.

Mfano alienda nyumbani myda wa tukio alikuwa amewasha smartphone, laptop au smartTV hivi vitu vnaweza kukubebaba. Au bodaboda, mangi,jirani pia wanaweza kuhusika kukubeba hapa.

Mwamba arudi mtaani, mafisadi waingie ndani.
 

Kabisa, ni sahihi!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…