Uchaguzi 2020 Wana JF, nipeni Pole. Msinicheke wala msinibeze; nimegombea ubunge Kawe kupitia CCM nimeambulia kura 1. Ama kweli CCM ina wenyewe!

Pole sana kaka na hongera pia kwa kuonyesha uthubutu.Amini kuwa Mungu amekufungulia njia. Kwa wakati wake utaona utukufu wake ukijitukuza kupitia wewe.Uwe na siku njema.
 
Sita kupa pole sababu naamini ulistahiki ulichopata
Lakini pia sitakubeza sababu umetumia haki yako

Mwisho natamani sana kumuona the old Pasco.........yule Pasco wa kujenga hoja kwa maslahi mapana ya taifa na si Mayala wa sasa wa kuimba mapambio ya kusifu na kuabudu
 
Napinga hoja mimi niko JF mwaka wa 11 huu. Huyu "njaa" simjui
 
Ukome kujipendekeza pendekeza, yale mashetani ya kijani ulitegemea yakupe kura ???
 
Mayalla, nilidhani 2020 sintaipigia CCM kura kwa sababu nilifikiri akina Musiba na mtu kama wewe ambao kazi yenu ni kuwasema vibaya wapinzani, kuwachonganisha na serikali, kuwakejeli na kuwazushia mambo mazito nilifikiri CCM itawachagua.
Kwa kitendo cha wewe na Musiba na wale waliohama vyama vya upinzani na kwenda CCM kukataliwa kwenye kura za maoni, nimeanza kurudisha imani kwa CCM.
HONGERA CCM KWA KUWAKATAA MTU KAMA WEWE.
 
Pamoja na Mapambio yote yale mkuu kweli pole sana ndio maana hata teuzi hupati ila mkuu Malipo ya mapambio ndio hayo
 
Asante kauli yako imesaidia kuonyesha uhalisia wako. Nyie ndio wapiga pesa na wenye uchu wa madaraka, yan kushindwa tu umekimbilia kusema ccm inawenyewe kama vile sio yule uliekuwa unaisifia kila.siku.
 
Mbona mchakato bado haujakwisha ,unaweza pata maaana baada ya hao kutangazwa majina yataoutia mchakato mwngn,so usishangae mtu amepita kura za maoni na Bado hasipate nafasi ya kupeperusha bendera ya kijani.
This is CCM bwana,chama kubwa.
 
Mbona mchakato bado haujakwisha ,unaweza pata maaana baada ya hao kutangazwa majina yataoutia mchakato mwngn,so usishangae mtu amepita kura za maoni na Bado hasipate nafasi ya kupeperusha bendera ya kijani.
This is CCM bwana,chama kubwa.
Sio kwa kupata kura moko na akaachwa mwenye kura 300
 
Kwani ulikuwa hujui CCM inaanzia mashinani,kama hushiriki community task ngazi za mashina,hujawahi kukusanyika kwenye michezo ya kata,usitegemee kuchaguliwa labda kuteuliwa.
 
Kuna jambo ulikuwa hulijui au ulilijua ila hukuwa serious.
Kwanza ilikupasa kujua ni nani mpiga kura.
Wajumbe wengi wako matawini na si humu Jf. Wengine hata TV hawana, so they don't know you .
Ungeutaka ubunge ungetafuta nafasi yoyote ndani ya CCM ambayo ingekufanya utambulike kwanza na wajumbe . ungepita kiulaini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…