Dah, mkuu pole sana. Sio kwamba CCM ina wenyewe bali hukujipanga vizuri na wananchi wengi wapiga kura upande wa CCM hawakufahamu. Wewe ni mwandishi wa habari lakini wanaokufahamu zaidi ni members wengi wa JF na wanaofuatilia nchi inavyokwenda kwenye vyombo vya habari na magazeti. Lazima ufahamu kuingia kwenye siasa sio lelemama kama kujiunga na JF na kuanza kutoa matusi na mipasho. (Sio wewe binafsi lakini kuna wengi tu wameingia sio kwa nia ya dhati ya kuona haki inatendeka bali kutoka maslahi ya watu flani flani).
Mkuu usikate tamaa jipange ila fahamu kuingia siasa ni mbinu lazima ujipange, bado 2025 ipo njiani jitafakari kwa kina then ujitose. Usione DJ Mbowe anakula ruzuku ya Bill 8 ukafikiri wapiga zumari wengi waliomo humu wanafanya bure, there is a price sisi wengine ni mapenzi tu ya nchi yetu kuona haki inatendeka wala hatutaki vyeo.
BTW hiyo kura moja ulijipigia mwenyewe, vipi marafiki zako n.k.