Uchaguzi 2020 Wana JF, nipeni Pole. Msinicheke wala msinibeze; nimegombea ubunge Kawe kupitia CCM nimeambulia kura 1. Ama kweli CCM ina wenyewe!

Uchaguzi 2020 Wana JF, nipeni Pole. Msinicheke wala msinibeze; nimegombea ubunge Kawe kupitia CCM nimeambulia kura 1. Ama kweli CCM ina wenyewe!

Pole sana Kaka jipange 2025 endelea kuwa mwanachama hai shiriki miradi ya chama katika Jimbo lako Kama mwanachama wakawaida na pia una jina kubwa sana hapa jamii forum ukubwa huo huo wa jina ukaonekane katika kata zote za Jimbo la kawe kwa wazee na vijana..2025 sio mbali

Kura hazipigwi JF mlamu!
 
Siku zote nilikuwa nakuona opportunist mkuu na kuegemea CCM haswa wakati huu ambapo mwenye nchi na viongozi wake washakujua ni hesabu nzuri.

Mungu akubariki ili tuone Paskali wa kabla na baada ya 2020 watakuwa sawa kiitikadi na kimaono [emoji120][emoji120]
 
Hongera umejitahidi ila uliingia sehemu siyo waombaji 170 wapiga kura 400 hapo ulitegemea kitu kweli,

Jitahidi usipate stree, ni mambo madogo madogo ila yanafikirisha.

Anyways kupotea njia ndio kujua njia au utapotea kwenda tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimekuona tu upon bize na simu hapa CCM ina wenyewe mnakuja Leo kesho etu mnataka uongozi nampongeza sana mh rais kwa kuweka wazi mghakato mzima hakuna cha kuchakachua wala nini
 
Pascal Mayalla,

Mwana kuyatafuta mwana kuyapata! Sikubezi kaka, ila kumbuka ni wapi ulipoanguka ukatubu. Musa hakuona shida kuteseka na watu wa Mungu kuliko furaha ya kitambo kwa farao.

Kwani ungekuwa mbunge ungeifanyia nini nchi yako kwa mfumo wa CCM zaidi ya kutumikia tumbo na kupongeza?
 
Mkuu inamana kujiajiri hutaki mpaka unaenda kugombea Ubunge?

Hizo nguvu unazotaka kuziweka katika ubunge basi jikite kwenye kampuni yako hakika Njaa itapoa

Ila CV yaako si imeshaingia kwenye kanzi data ya CCM-uteuzi kwahyo subiri wilaya yako tu Pascal Mayalla
 
Back
Top Bottom