Uchaguzi 2020 Wana JF, nipeni Pole. Msinicheke wala msinibeze; nimegombea ubunge Kawe kupitia CCM nimeambulia kura 1. Ama kweli CCM ina wenyewe!

Uchaguzi 2020 Wana JF, nipeni Pole. Msinicheke wala msinibeze; nimegombea ubunge Kawe kupitia CCM nimeambulia kura 1. Ama kweli CCM ina wenyewe!

Ubahili umekuponza. Kama unaweza kuwapa milioni 10 kila kata umeshindwa nini kuwahonga wajumbe elfu kumi kumi????

Wajumbe 400 ukiwapa elfu 10 kila mmoja ni milioni 4 tu. Ndio maana wamekuona haupo serious!

Hii aibu ni ya wana jf wote, hadi Mashinji na Mwijaku wamekuzidi kura!

Inabidi upigwe ban kama ya mwezi hivi ili akili ikae sawa.
 
Mkuu Pascal Mayalla pole kwa matokeo na hongera kwa kujaribu. Juzi Jumamosi katika kipindi cha jicho letu katika Habari cha Star Tv ulitangaza kustaafu uandishi wa habari. hata hivyo nakuomba ubadili nia yako na kurejea katika kipindi husika. Nitafurahi kama utatushirikisha uzoefu ulioupata kwa kushiriki katika huu uchaguzi.

Ahsante
 
Kaka Pascal kwanza nikupe hongera kwa uthubutu.

Pili nikupe hongera kwa kupata kura hizo 11 zinamaanisha kuwa kuna watu wana imani nawe zaidi ya walivo na imani na Nabii. Hilo ni jambo la kujipongeza.

Tatu ni kuwa huo ni mwanzo tu wa mchakato na sio mwisho wake. Huenda jina lako likapitishwa na kamati kuu ama ukakumbukwa kwenye nafasi za uteuzi.

Ni kweli CCM ina webyewe na wenyewe ni wanachama wake kama wewe mwenyewe.

La muhumu zaidi ni kuwa sasa ushaonesha rangi zako za kweli baada ya kufunuwa nikab yako na wana JF wenzako tumeshakujuwa.
 
Kwanza nikupongeza kwa ujasiri wa kuchukua fomu na kugombea. Kugombea sio jambo rahisi sana na unapopata kura 1 haina maana hoja zako hazikuwa na mashiko, huenda jina lako limekuwa jipya sana kwa wajumbe wa mkutano mkuu wa jimbo.

Nimefanya siasa kidogo za vyama, inahitaji kuwaivisha wapiga kura kwa muda wa kutosha na kuna wakati unaweza kupata au kukosa vilevile.

Nikupongeze tena kwa ujasiri hasa kwenye muda kama huu.

2025 unaweza kuja kivingine.
 
Tunakupongeza kwa uthubutu wako wa kugombea jimbo hilo kwa tiketi ya CCM. Na pia kwa kututhibitishia ukweli kwamba CCM ina wenyewe. Ukweli ndio huo, waliomo ndani wamo na wasingependa wasiokuwamo wapenyeze kiurahisi.
 
Back
Top Bottom