Mwongozo wangu upo hivi...
Ukisoma vizuri thread ya watu wa Arusha utagundua wameshatoa gharama na utaratibu mzima wa safari.
Sasa kuna vitu kwanza inabidi watupe mwangaza kabla ya kuendelea na hatua yoyote inayofuata.
Mosi, Je magari watakayotoka nayo Arusha ndio hayo hayo watayatumia kufanya mizunguko wakifika TANGA?
Kama jibu ni NDIO basi inabidi na sisi tufuate utaratibu kama huo.
Kama ni HAPANA watueleze kule TANGA utatumika utaratibu (haswa gharama) upi kwenye suala la USAFIRI.
ZINGATIA:Tukifika TANGA wote misele itakua ni ile ile, hivyo utofauti wetu upo tu kwenye namna ya kufika huko TANGA.
Pili, gharama za MALAZI hizi zitakuwa sawa kama wao walivyopanga, hili sio la kujadili
Tatu, kwa habari ya CHAKULA sina uhakika ni utaratibu gani utafuatwa ila pia sioni kama kutakuwa na shida hapo.