Wanachama UN wapiga kura mzozo wa Urusi - Ukraine

Wanachama UN wapiga kura mzozo wa Urusi - Ukraine

brazaj

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2016
Posts
31,698
Reaction score
41,733
Kumepigwa kura UN kuhusiana na nani ni nani kwenye uvamizi wa Ukraine.

Upande wa Russia kuna North Korea, Syria, Belarus na Eritrea.

IMG_20220303_093713_066.jpg


Kwa mujibu wa Tutu na bwana Martin Luther yumkini na sisi tumewakilisha:



IMG_20220201_083950_789.jpg


Source: NPR Cookie Consent and Choices
===

Nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa wamekutana kwa dharura na kupiga kura za misimamo yao juu ya mzozo wa Russia-Ukraine unaoendelea kutikisa dunia.

Kura hizo ni mahsusi na ni azimio la kukemea vikali mashambuliz ya kibabe yanayoendelea kufanywa na Urusi dhidi ya Taifa la Ukraine, ambapo licha ya jitihada za usuluhishi kuanzishwa, bado vita hivyo vimeonekana kushika hatamu.

Hatua hii ni shinikizo baada ya Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelenskyy kuomba msaada wa kimataifa zaidi ya maramoja kwa lengo la kudhibiti vita hivyo ambavyo nchi yake imeonekana kuathirika zaidi ya mbabe wake Urusi kadiri siku zinavyosogea.

Nchi 141 kati ya 193 za UN zilipiga kura ya kuilaani vikali Russia na kuridhia kuwekewa vikwazo mbalimbali vya kimaendeleo na uchumi wake duniani kote.

Nchi tano hazikukubaliana na uamuzi huu; wao waliisapoti Urusi. Kati ya nchi hizo ni washirika wa Urusi ambao ni Belarus, Korea ya Kaskazini, Eritrea na Syria.

Nchi 35 hazikufungamana na upande wowote. Miongoni mwao ni nchi ya China ambaye ni rafiki mkubwa wa Urusi pamoja na Uganda.
Nchi 11 hazikushiriki (kupiga kura) kabisa.

Rais Zelenskyy wa Ukraine alishukuru nchi wanachama kwa kushiriki katika kura hizo, hasa zile zilizopiga kura za kulaani Urusi.
 
Kama nchi hatufungamani na upande wowote, ila wananchi mmojammoja wana maoni yao

Mungu Ibariki Tanzania

Mungu wabadilishe viongozi wa Russia na Ukraine mioyo yao watafute Suluhu nje ya vita
 
TZ mnasema woga/wasaliti wakati nchi kubwa kama China haikupiga kura. Kwa mtazamo wangu (based na nchi zote 35 absent) ni wazi waliokuwa hawakupiga kura hawakutaka kuonesha wazi msimamo wao, lakini iko wazi wameunga mkono Russia kimya kimya.
 
TZ mnasema woga/wasaliti wakati nchi kubwa kama China haikupiga kura. Kwa mtazamo wangu (based na nchi zote 35 absent) ni wazi waliokuwa hawakupiga kura hawakutaka kuonesha wazi msimamo wao, lakini iko wazi wameunga mkono Russia kimya kimya.

IMG_20220201_084022_348.jpg
 
Hiyo kura amepiga nani? Ingekuwa enzi za ujamaa tungesimama na Russia

Enzi ya Nyerere ilikuwa ya ujamaa. Tusingesimama na Russia.

Usichanganye enzi ya ujamaa na enzi zenu matajiri mkikutana:

IMG_20220303_102530_977.jpg

Hiiiiii bagosha!
 
Back
Top Bottom