Wanachama wa Yanga na Simba ni mambumbu wa mpira. Wataazima viwanja mpaka dunia ina malizika

Wanachama wa Yanga na Simba ni mambumbu wa mpira. Wataazima viwanja mpaka dunia ina malizika

Malaria 2

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2023
Posts
6,846
Reaction score
10,288
Licha ya kuwa mpira ni haramu kwa mujibu wa mafundisho ya dini yangu lkn kama mimi kama msomi sinabudi kuchambua mchezo huo.
Tuanzie hapa.
Yanga na simba ni timu kongwe sana Tanzania, ni timu zenye washabiki wengi na ndio timu zinazotegemewa ktk Afrika kwa ujumla.
Yanga imevuma sana huko nyuma tangu enzi za Juma Mkambi ( General) , Makumbi Juma ( Homa ya jiji) Lauret Mwalosako, Athumani Juma Chama, Yussuf Bana, Godwin Aswile, Edubli Lunyamila- hini kizazi cha hivi karibuni kabla kizazi nyuma kabisa cha akina Sunday Manasara, Said Zimbwe nk
Huku simba ikiwa na Malota Soma, Edward Chumila na wengine wengi.

Kwanini hadi leo Simba Yanga hazina uwanja tofauti na Azam ambayo ni yajuzi juzi tu?
Mipango mibaya na ufisadi wa timu unaathiri maendeleo.
WANACHAMQ WA YANGA SIMBA NI MAMBUMBU

Wanachama wa Yanga na simba wao wanaangalia nani kamfunga nani lkn hawaangalii management imefanya nini
Management ilimuekea kikwazo FEI Toti wanachama walifurahia huku mijadala ya mtandao ya kijaamii ikishika kasi

1. Utawala unafanya nini ktk ujenzi wa uwanja? Au itakuwa inadandia viwanja vya timu ndogo ndogo?
2. Timu ina kipato gani na ina madeni gani?
3. Hipi long plan ya timu ambayo imewasilishwa katika mkutano wa wanachama?
4. Mapato na matumizi ya timu kwa mwaka imewasilishwa kwa wanachama? Au ndio akisajiliwa mchezaji wa kigeni na kusifiwa na uongozi wanachama wanaridhika?

3
.
 
Uwanja wa mpira Wala sio jambo kubwa la kuwatisha Simba na YANGA sema tu hawajaona tija kuwekeza huko, wameona bora wa outsource viwanja kuliko kujiongezea majukumu ya kumaintain uwanja, kama viwanja ni muhimu kwako basi tuwaambie pia wawe na hotels zao wasiwe wanakodi maana ni gharama pia.
 
Taja timu moja yenye maendeleo duniani ambao wana outsource ya uwanja
 
Usilolijua ni kwamba

hizo ni team za siasa ambazo zinatumiwa na serikali kuongeza mapato..hawawezi kuziachilia kirahisi..KUNA SIASA NDANI YAKE
 
Kuna watu wananufaika na huo mfumo mzee,kwa hilo wanachama hawana hatia,kwa namna hizi imani mbili zilivyo,akija kiongozi mwenye utashi kuwachangisha tu ili uwanja ujengwe na project ikaanza,watajenga tu......ila sasa kuna watu wananufaika sana kwa hizo hama hama
 
Kiwanja si 🍑 kusema kila timu iwe nacho. Na hizi ni kelele za msimu tu, kuhusu timu na viwanja. Yanga kuhama uwanja, mtakuja na kila nadharia. Mtasahau, hivi vilabu wakiona umuhimu, watajenga tu.
 
Kiwanja si 🍑 kusema kila timu iwe nacho. Na hizi ni kelele za msimu tu, kuhusu timu na viwanja. Yanga kuhama uwanja, mtakuja na kila nadharia. Mtasahau, hivi vilabu wakiona umuhimu, watajenga tu.
Kwa mashabiki weye ndio nyie management watakula pesa mpaka watapike
 
Unawafahamu AC milan na Inter milan? Km ulikuwa hujui sasa hao ndo Simba na Yanga wa pale Italy... Vp ulishawahi fuatilia wanatumia uwanja gani?

Andiko lako ni zuri sana, lakini kabla hujalilinganisha andiko lako na dunia jaribu kuperuzi kwanza ili usionekane mjinga
 
Hivi tawala za Yanga na simba wanavyohadaa wanachama wao
 
Back
Top Bottom