Wanafamilia 5 waliokufa uwanja wa Uhuru kuzikwa leo. Mchungaji Mastah aongoza ibada

Laiti serikali ingekuwa ya watu kwa ajili ya watu, PM alitakiwa ajiuzulu kwa hiari au kwa lazima, baada tu ya mazishi Chato.
Ajiuzulu kwasababu ya huu uzembe hebu muache majaliwa ana mambo mengi kuwajibika, hilo hata viongozi wengine walishindwa kuandaa utaratibu wa kwenda kumuona hayati JPM bila kuwa na msukumano bali kwa mstari

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Poleni sana nasikia na mbunge wa ubungo ndo hivo tena hatunae.
Naomba niishie hapo tafadhali
 
Sio ujinga ndugu,hicho kifo sio cha kawaida kuna kitu kilikuwa kinamsukuma huyo mama aende huko tena na familia yote can u imagine?....muulize ndugu Mshana Jr sema hawez kuelezea hili anaogopa wanakijani watamvamiaa[emoji23]
[emoji3]kuna mengi tutajuzana hebu tuupe muda wakati
 
Yule MTU tangu Enzi na mama yake wanatuhumiwa ' Kujua mengi'. Watu WA lake zone wanajua .Ipo hata habari kuwa makazi wanayoishi SASA waliyapata toka kufukuzwa baada ya kujulikana wanajua mengi ya kidunia.
wanaruka na ungo??
 
Fidia? Binadamu aliyepotelewa na ndugu yake kwa kufariki huwa anafidiwa na kitu gani kinachozidi thamani ya roho iliyotoweka?
 
Kwa kweli ni majonzi makubwa kwa familia iliyopoteza watoto watano wakati wa kuuwaga mwili wa Dkt. Magufuli aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tano na hivyo basi kama itapendeza itoe kifuta jasho kwa ile familia iliyopoteza watoto watano.
 
Reactions: LGF
Kifo cha wengi ni sherehe 🤔
 
Kwa kweli ni majonzi makubwa kwa familia iliyopoteza watoto watano wakati wa kuuwaga mwili wa Dr. Magufuli aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tano na hivyo basi kama itapendeza itoe kifuta jasho kwa ile familia iliyopoteza watoto watano.
Ingekuwa serikali ya Magufuli, wazazi wangeozea jela kwa uzembe
 
Rais juzi kahutubia Dodoma wala hajaona umuhimu wa kuongelea unategemea watapewa chochote, labda?
 
Ni kweli, hata mimi naunga mkono hoja kwa 100%.
Ni muhimu sana kuwashika mkono waliopoteza familia zao katika Msiba wa Commando wetu JPM.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…