Wanafamilia 5 waliokufa uwanja wa Uhuru kuzikwa leo. Mchungaji Mastah aongoza ibada

Kuna umuhimu kwa familia za wahanga wote kulipwa fidia na serikali. Wangefuata taratibu sahihi za miaka yote za kuwaaga viongozi wa kitaifa, haya yote yasinge tokea.
Pamoja na lawama kwa serikali, nadhani watanzania tuna ushamba au ulimbukeni juu ya mambo, dunia kwa sasa ni kama kijiji, kuna matukio tunaweza kuyaangalia tukiwa majumba i mwetu lakini myu mwenye akili timamu anabeba watoto na kuwapeleka kwenye mazingira hatarishi kama yale
 
Huyu Mama alikua mjinga sana amesababisha watoto wafe kifo kibaya mno, na inaonekana walidondoka wote kwa pamoja na watu wakawalalia.
Mjinga zaidi ni mume, aliruhusu vipi familia yake kwenda kwenye porpulation kama ile, yaani mke wako anakurupuka tu anaondoka nyumbani na watoto wote eti anawapeleka msibani, unapoutwa kichwa cha familia ni pamoja na kuilinda familia yako, kuhakikisha kila wanapokwenda usalama wao ni 100%
 

Kuna hiyo nadharia huja baada ya jambo kutokea, kwanini hakufanya hivi, kwanini haikua vile, hivi ilikuaje akaenda njia hile ona mpaka umauti imemfika, lakini jambo lilojificha ni siku ikifika nahisi unakua kama umepumbazwa hata huwezi kung'amua mambo au kufanya maamuzi mengine tofauti
 
Kuna haja gani ya kwenda na watoto kuaga maiti, mnapojifanya kukengeuka maadili ndio yanatokea, poleni sana...watoto wa kiafrica huwa wanabaki nyumbani, kwani walikwama wapi hii familia???
 
Mume wangu amesafiri ila alivyojua ni zamu yetu Dom kuaga kapiga simu asubui asubui akasema asisikie mtu anaenda uwanjani au barabarani kuaga tuomboleze kupitia TV tuu.
 
Ni sawa ila sisi tuliobaki tupate somo
 
Kabisa nadhani huwa kuna nguvu fulani. Natamani hata kujua walikua wanajisikiaje but who to tell a tale
 
Sana huwezi amini picha za hao wtt zinajirudia kichwani mwangu naumiaaa naumia sana
Msiba juu ya msiba, yule baba wa hile familia nimekosa majibu, mtu kukumbwa na msiba wa kupoteza members of ur family [emoji128] ni jambo sio rahisi, ni ngumu kuubeba msiba huu na unahitaji kifua kwa kweli hasa muda kama huu usiku unapoingia kulala, pale unapobaki peke yako na mawazo yako na kutafakari yaliyokutokea
 
Halafu kuangalia tukio kwenye TV ni raha kuliko live,kwenye TV utaona angle zote maana wana camera nyingi.

Kwenye mikusanyiko ya watu wengi ni hatari sana,2015 kwenye kampeni ya lowassa jangwani nilishuhudia ,ni hatari ni hatari ni hatari.
 
Acha kabisa mkuu
 
Kabisa nadhani huwa kuna nguvu fulani. Natamani hata kujua walikua wanajisikiaje but who to tell a tale
Wapo waliokiona kifo kabisa na kurudi katika hali ya kujitambua wakikusimulia utaogopa
 
Mwanamke hakuwa mwerevu, uwezi kurupuka na watoto wadogo wakaangalie maiti, wengine ni watu wazima ila hatunaga shobo na maiti hata kidg, unaaga pakiwa na ulazima sasa yeye akili hana atakua mswahili huyo...
 
Sio ujinga ndugu,hicho kifo sio cha kawaida kuna kitu kilikuwa kinamsukuma huyo mama aende huko tena na familia yote can u imagine?....muulize ndugu Mshana Jr sema hawez kuelezea hili anaogopa wanakijani watamvamiaa[emoji23]
Mmh Kila kitu mnawaza uchawi
Akili ndogo kabisa
Uzembe was mtu mnawaza tofauti
Vifo vipo Mungu aliwwka kifo sio Kila kifo NI ushirikina
 
Kwakuwa limeshatokea liwe funzo kwa wengine ,watoto ni wa kukaa nyumbani tu ,watoto pia hawatakiwi kupelekwa sijui kwenye maswiming pool ,sijui pikiniki kwenye kuona wanyama ,sijui maetmbezi ya bla bla ni hatari.....Mimi issue za kwenda study tour huwa sikubali waende kama kuwapeleka niwapeleke mimi ambaye uangalizi utakuwa 100%.(watoto hawajitambui kwahiyo wazazi inabidi waplay part kubwa kuwalinda na sio kuwategemea hao mamatron waliovurugwa na maisha)

Kwa maendeleo ya technology ya sasa ,hivyo vitu vyote anaviona akiwa sebuleni..Kama anataka kuona wanyama muwekee Discovery channel etc watoto ni wa kutulia nyumbani na kujijenga kiakili kumsumbua sumbua na mizunguko ni kumvuruga akili mapema.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…