Wanafunzi 10 bora kitaifa matokeo darasa la saba 2021

Du hiyo Tuibok ni noma aisee katika marlfu a shule ,una nafasi zote hizo ??
 
Twibhoko ni private au ya serikali
Yawezekana itakuwa ya serikali mkuu, kama ni mtu binafsi basi kaipa jina la ukoo wake, shule kuwa na jina la namna hiyo si atakosa wateja?.

👉🏾 Although nakumbuka miaka ya 1980 kurudi nyuma shule za ukanda wa ziwa zilikuwa zinaupiga mwingi hasa na wanafunzi walikuwa wanapiga kitabu kwelikweli asee!.

Vyuo vingi vilikuwa na vijana kutoka Mara, Bukoba na Mwanza.
 
Aisee Twibhoki ni kiboko imetoa watoto weng ktk top ten ninataman kujua ni ya private au serikal
 
ingekuwa enzi za utawala wa marehemu, ili wamfurahishe mtukufu, katika hao kumi bora waliofaulu, wangechomeka mmoja kutoka katika wilaya inayopatikana mkoa wa geita
Infact we were heading to a point of no return (total darkness)...
 
ingekuwa enzi za utawala wa marehemu, ili wamfurahishe mtukufu, katika hao kumi bora waliofaulu, wangechomeka mmoja kutoka katika wilaya inayopatikana mkoa wa geita
Hahahaaaa
 
Yaani nyie watu ni zero kabisa inakuwaje kila mada ikitajwa lazima muibuke na jina la magufuli.
ingekuwa enzi za utawala wa marehemu, ili wamfurahishe mtukufu, katika hao kumi bora waliofaulu, wangechomeka mmoja kutoka katika wilaya inayopatikana mkoa wa geita
 
Dar es Salaam. Baraza la Mitihani Tanzania (Necta), limemtaja mwanafunzi aliyehitimu shule ya msingi St Anne Marie iliyopo mkoani Dar es Salaam, Eluleki Evaristo Haule kuwa ndiye aliyeibuka kinara katika matokeo ya mtihani ya Darasa la Saba 2021.

Akitangaza matokeo hayo leo Jumamosi Oktoba 30, 2021 Katibu Mtendaji wa Necta, Dk Charles Msonde amesema watahiniwa bora kitaifa ni wale ambao wamepata alama nyingi zaidi kuliko wenzao kwenye masomo sita waliyotahiniwa.

Alimtaja aliyeshika nafasi ya pili kuwa ni Happy Joseph Deus kutoka shule ya msingi Twibhoki ya Mkoa wa Mara na nafasi ya tatu ikienda kwa John Chacha Charles kutoka Twibhoki.

Aliyeshika nafasi ya nne ni Joshua Mahende Jacob kutoka shule ya msingi Twibhoki iliyopo Mara pia, Eva Sebastian Chengula kutoka shule ya msingi Fountain of Joy ya Dar es Salaam ameshika nafasi ya tano, Joctan Samwel Matara kutoka Twibhoki ameshika nafasi ya sita.

Barnaba Jumanne Magoto kutoka shule ya msingi Twibhoki ipo Mara ameshika nafasi ya saba, Rahma Ombi Juma kutoka shule ya Mtuki Highland iliyopo Dar es Salaam ameshika nafasi ya nane na nafasi ya tisa ni Juliana John Shimbala kutoka St Joseph’s nafasi ya kumi ameishika Jackline Manfredy kutoka shule ya Masaka iliyopo Dar es Salaam.
matokeo kwani yashatoka ya darasa la Saba Nchi nzima
 
Hongera kwake!. Kama kuna watu wako karibu na huyo T.O wa darasa la saba wampe guidance. Awekwe kwenye msingi mzuri
 
Dar es Salaam. Baraza la Mitihani Tanzania (Necta), limemtaja mwanafunzi aliyehitimu shule ya msingi St Anne Marie iliyopo mkoani Dar es Salaam, Eluleki Evaristo Haule kuwa ndiye aliyeibuka kinara katika matokeo ya mtihani ya Darasa la Saba 2021.

Akitangaza matokeo hayo leo Jumamosi Oktoba 30, 2021 Katibu Mtendaji wa Necta, Dk Charles Msonde amesema watahiniwa bora kitaifa ni wale ambao wamepata alama nyingi zaidi kuliko wenzao kwenye masomo sita waliyotahiniwa.

Alimtaja aliyeshika nafasi ya pili kuwa ni Happy Joseph Deus kutoka shule ya msingi Twibhoki ya Mkoa wa Mara na nafasi ya tatu ikienda kwa John Chacha Charles kutoka Twibhoki.

Aliyeshika nafasi ya nne ni Joshua Mahende Jacob kutoka shule ya msingi Twibhoki iliyopo Mara pia, Eva Sebastian Chengula kutoka shule ya msingi Fountain of Joy ya Dar es Salaam ameshika nafasi ya tano, Joctan Samwel Matara kutoka Twibhoki ameshika nafasi ya sita.

Barnaba Jumanne Magoto kutoka shule ya msingi Twibhoki ipo Mara ameshika nafasi ya saba, Rahma Ombi Juma kutoka shule ya Mtuki Highland iliyopo Dar es Salaam ameshika nafasi ya nane na nafasi ya tisa ni Juliana John Shimbala kutoka St Joseph’s nafasi ya kumi ameishika Jackline Manfredy kutoka shule ya Masaka iliyopo Dar es Salaam.
Subiri kidogo, hivi mbona kwenye list ya wanaofanya vizuri(top ten) level zote huwa ni majina ya ki kristo kuliko kiislam?!
 
Back
Top Bottom