Wanafunzi 10 bora kitaifa matokeo darasa la saba 2021

Wanafunzi 10 bora kitaifa matokeo darasa la saba 2021

ingekuwa enzi za utawala wa marehemu, ili wamfurahishe mtukufu, katika hao kumi bora waliofaulu, wangechomeka mmoja kutoka katika wilaya inayopatikana mkoa wa geita
🤣🤣🤣 hizi comment zinaongeza siku za kuishi
 
Du hiyo Tuibok ni noma aisee katika marlfu a shule ,una nafasi zote hizo ??

Lakini pia ina idadi ya Wanafunzi wachache sana ni 25 tu.So ukilinganisha na Shule kama Liberman iliyokuwa na wanafunzi zaidi ya 100 na 95 % wana Daraja la kwanza.Twibhoko inabebwa na uchache wa wanafunzi.
 
Hii ya Tafuta wa kwanza kitaifa na wa mwisho ni kosa kubwa ambalo asilimia kubwa ya watu hawalioni hilo kosa.Janja janja zinakuwepo sana, wasimamizi kupewa Bahasha na kadhalika
Ni kweli hasa private lazima waibe mtihani Ili ikifaulisha ipate wateja wakutosha
 
Kipindi cha kuwabeba wanageita kimeisha kenge nyie !!!hakuna kubebwa tena !!! Endekeen kufuga fisi na chatu na kukwepa jando

Kwa taarifa yako Geita ina shule mbili katika top 10! Endelea kula malimao ukate kichefu chefu maana ndiyo kwanza una mimba ya miezi miwili,mpaka ufikishe miezi 9 utakuwa umechoka sana.Mwanahizaya mkubwa uso kuwa na haya!
 
Binafisi mimi sio muumini wa hizi sijui wa kwanza kitaifa, hii ya kushindanisha shule ni kosa kubwa sana linalo fanywa na taasisi ya elimu.

Ulitaka wafanyeje ili kupima ubora wa Wanafunzi na shule zao?Mbona sehemu nyingi Duniani wanafanya hivyo,unadhani ni vigezo vipi vimetumika kurank Vyuo vikuu bora Duniani kama siyo kuvishindanisha? Havard,Yale, Oxford and the likes ziliwezaje kuwa katika Top ten ya Vyuo vikuu Bora Duniani?
 
Hii ya Tafuta wa kwanza kitaifa na wa mwisho ni kosa kubwa ambalo asilimia kubwa ya watu hawalioni hilo kosa.Janja janja zinakuwepo sana, wasimamizi kupewa Bahasha na kadhalika

Inaelekea una mtoto matokeo yake si mazuri wewe,siyo kwa makasiriko uliyonayo leo [emoji3][emoji3]
 
Miaka yote akiwa Madarakani mbona NECTA hawajawahi kuchomeka huyo mwanafunzi kutoka hiyo Wilaya....Uongo useme wewe aibu naona mimi.

ugopa sana Mungu na teknolojia.
[emoji116][emoji116][emoji116][emoji116]
View attachment 1992759
IMG_20211031_021717.jpg
 
Twibhoki haipo kwenye top 10, Grayasara inaongoza lakini haina mwanafunzi hata mmoja kwenye top 10.......ngachoka mimi.
Twibhoki imeongoza kwenye shule zenye wanafunzi chini 40.afu pia naskia Twibhoki na Graiyaki ni ndugu..
 
Iwe inatangazwa shule iliyofanya vizuri kitaifa, na siyo mwanafunzi wa shule fulani aliyeongoza kitaifa. Nionavyo mimi shule ya kwanza kitaifa ni Tuibhok ya Mara kwa kwa kuwa ina wanafunzi wengi waliopata alama za juu.
 
Dar es Salaam. Baraza la Mitihani Tanzania (Necta), limemtaja mwanafunzi aliyehitimu shule ya msingi St Anne Marie iliyopo mkoani Dar es Salaam, Eluleki Evaristo Haule kuwa ndiye aliyeibuka kinara katika matokeo ya mtihani ya Darasa la Saba 2021.

Akitangaza matokeo hayo leo Jumamosi Oktoba 30, 2021 Katibu Mtendaji wa Necta, Dk Charles Msonde amesema watahiniwa bora kitaifa ni wale ambao wamepata alama nyingi zaidi kuliko wenzao kwenye masomo sita waliyotahiniwa.

Alimtaja aliyeshika nafasi ya pili kuwa ni Happy Joseph Deus kutoka shule ya msingi Twibhoki ya Mkoa wa Mara na nafasi ya tatu ikienda kwa John Chacha Charles kutoka Twibhoki.

Aliyeshika nafasi ya nne ni Joshua Mahende Jacob kutoka shule ya msingi Twibhoki iliyopo Mara pia, Eva Sebastian Chengula kutoka shule ya msingi Fountain of Joy ya Dar es Salaam ameshika nafasi ya tano, Joctan Samwel Matara kutoka Twibhoki ameshika nafasi ya sita.

Barnaba Jumanne Magoto kutoka shule ya msingi Twibhoki ipo Mara ameshika nafasi ya saba, Rahma Ombi Juma kutoka shule ya Mtuki Highland iliyopo Dar es Salaam ameshika nafasi ya nane na nafasi ya tisa ni Juliana John Shimbala kutoka St Joseph’s nafasi ya kumi ameishika Jackline Manfredy kutoka shule ya Masaka iliyopo Dar es Salaam.
Mkuu,
Hiyo Twibhoki ipo wilaya gani huko Mara?
Je, ni private au ya kata?
Ina boarding?
 
Back
Top Bottom