Wanafunzi 22 wa Kidato cha Sita katika Shule ya Sekondari Shinyanga kuzuiwa kufanya Mtihani wa Kidato cha Sita 2021

Mkuu Huu ni ushauri Wa mtu aliyekula makande ya ikungu lya mbeshi,unadhani waziri ni kama kaka mkuu,kwamba unaondoka Leo siku hiyohiyo unapata appointment ya kuonana naye?
Mwenzetu katoa ushauri katika uelewa wake,pengine saidia kuuboresha ushauri kaka ili tuwasaidie hawa watoto!
 
Hata hii leo nasikia iko vzr sn,tatizo linatajwa ni staff ya shule kufail katika eneo la usimamizi wa nidhamu kwa watoto
Tulikuwa na mwalimu wa nidhamu na akademiki ainaitwa Dungu m chawi wa makemia na bio huyo aliitunyoosha sana ..ukisikia Dungu anakuja unaingia uvunguni kimyaa kama paka
 
Kwa sasa staff imefel mno kwene nidhamu. Nasikia mwaka jana wanafunzi waliwahi kutoroka na kuandama kuelekea kwa RC usiku saa tisa na walimu bila taarifa. Yaan watoto wanatoroka shule nzima na hadi wanafika Kolandoto km 15 staff hawana taarifa.
Hahhaaa!!!
 
Nikikumbuka migomo😤🙌!
 
Kuna taarifa kuwa wanafunzi 22 wa kidato cha sita wa Shule ya Sekondari ya Shinyanga maarufu kama Shybush,wamefukuzwa shule na kuzuiwa kufanya mtihani wa kidato cha sita unaotarajiwa kuanza mapema mwezi ujao wa tano.

Taarifa zaidi zinadai kuwa sababu kubwa ni fujo iliyotokea shuleni hapo mwezi March ambapo wanafunzi waliharibu gari la Mwalimu,na hivyo kupelekea bodi ya shule hiyo kukutana na kuamua wanafunzi hao wachukuliwe hatua hiyo.
Sambamba na hao,pia wapo wengine zaidi ya 30 ambao walirejeshwa makwao na wataruhusiwa kufanya mitihani yao wakitokea makwao.

Binafsi niwaombe wataalamu wa sheria wanisaidie ufafanuzi wa juu ya "Waraka wa Elimu No. 13" uliotumiwa na bodi ya shule hiyo kuondoa haki ya vijana hao kufanya mtihani na kupelekea vilio na majonzi kwa wazazi na walezi.
Hao vijana waombe kufanyia mitihani yao kituo kingine hata kama ni private candidate centre kwa kutumia usajili wa shule yao. Sio sahihi kabisa hao vijana wasifanye mitihani yao, pia nafikiri wahusika wanafahamu vizuri psychology.
 
Kwa sasa staff imefel mno kwene nidhamu. Nasikia mwaka jana wanafunzi waliwahi kutoroka na kuandama kuelekea kwa RC usiku saa tisa na walimu bila taarifa. Yaan watoto wanatoroka shule nzima na hadi wanafika Kolandoto km 15 staff hawana taarifa.
Hahhaaa!!!
Hahaha Mkuu umenikumbusha tulikuwa tukifunga shule tulikuwa tunatembea kutoka hapo shuleni usiku saa moja asubuhi tupo mjini Shy na mabegi duh kama jeshini ..yaani tunakutana na fisi wanakimbia
 
Hao vijana waombe kufanyia mitihani yao kituo kingine hata kama ni private candidate centre kwa kutumia usajili wa shule yao. Sio sahihi kabisa hao vijana wasifanye mitihani yao, pia nafikiri wahusika wanafahamu vizuri psychology.
Pengine hii ndiyo idea inaweza kuwajenga na ikawasaidia mno ktk kipindi hiki kifupi kilichosalia. Sasa hii ruhusa inaombwa na kutolewa kwa nani? Saidia mawazo kaka ili tuwajuze wakimbie nalo hili
 
Kwa mazingira na ukubwa wa miundo mbinu ya. Shybush kwa sasa ilipaswa kuwa Chuo Kikuu huko kanda ya Ziwa
 
Pengine hii ndiyo idea inaweza kuwajenga na ikawasaidia mno ktk kipindi hiki kifupi kilichosalia. Sasa hii ruhusa inaombwa na kutolewa kwa nani? Saidia mawazo kaka ili tuwajuze wakimbie nalo hili
Baraza la mitihani, kwa sababu litakuwa limekwisha wapa namba zao za mitihani. Likishafanya hivyo lazima mwanafunzi afanye mitihani.
 
Naamini wahusika wamo humu wamesoma huu uzi na ufumbuzi UTAPATIKANA vijana wafanye Mitihani ..Jamii forum imebeba watu wengi sana muhimu na MAKINI
 
Naona kifahamu sababu za kufanya fujo na kuharibu mali ya mtumishi
Sababu zinazotajwa ni baadhi ya walimu kuwa nyuma ya uchochezi wa hizo vurugu ingawa sidhan kuzithibitisha ni rahisi sn.
Kwan inashangaza kusikia wanafunzi wanakaa vikao na kumobilize tukio walimu wapo na wanaona bila kujali kufatilia.
 
Baraza la mitihani, kwa sababu litakuwa limekwisha wapa namba zao za mitihani. Likishafanya hivyo lazima mwanafunzi afanye mitihani.
Sasa ndiyo weshafukuzwa na nasikia hata RC amebariki uamuzi wa bodi ya shule,wataufanyaje huo mtihani. Tuwaelekeze wakimbilie wapi ili wasaidike?
 
Sasa ndiyo weshafukuzwa na nasikia hata RC amebariki uamuzi wa bodi ya shule,wataufanyaje huo mtihani. Tuwaelekeze wakimbilie wapi ili wasaidike
Naamini wahusika wamo humu wamesoma huu uzi na ufumbuzi UTAPATIKANA vijana wafanye Mitihani ..Jamii forum imebeba watu wengi sana muhimu na MAKINI
Pengine uwe ndiyo msaada pekee jamani. Unajua ukiwawazia vijana wenyewe unaona km wanafanya ujinga ule kwa sabb tu ya peer pressure ambayo always haimpi mhusika nafas ya kuwazia matokeo baada ya tukio wanaloshiriki. Lakini madhara zaidi utayakuta kwa wazazi wa watoto hawa. Wengne wamejichimba mfukoni kuwaandaa kwa gharama kubwa kupitia shule binafsi,leo mtoto kafikia hatua ambayo mzazi anawazia aanze kupumua,ghafla analetewa taarifa ya mtoto kufukuzwa shule na mbaya zaidi hadi aondolewe ktk mfumo rasmi wa elimu!!
NADHANI WAHUSIKA WAONE SABABU YA KUSAIDIA HILI SUALA JAMANI.
 
Sasa ndiyo weshafukuzwa na nasikia hata RC amebariki uamuzi wa bodi ya shule,wataufanyaje huo mtihani. Tuwaelekeze wakimbilie wapi ili wasaidike?
Kama hawajafanya jinai wananafasi ya kufanya mtihani,lakini pia Kama RC amebariki itakuwa ngumu kwa kuwa board ya rufaa ipo chini yake kwa maana makosa yaliyofanywa na wanafunzi yanastahiki kufukuzwa.
Screenshot_20210422-064849_1619063734101.jpg
 
Kama hawajafanya jinai wananafasi ya kufanya mtihani,lakini pia Kama RC amebariki itakuwa ngumu kwa kuwa board ya rufaa ipo chini yake kwa maana makosa yaliyofanywa na wanafunzi yanastahiki kufukuzwa.View attachment 1760079
NIMEIELEWA HII KAKA AHSANTE!
Sasa kwa mkao wa hili suala hawa waende wapi na kwa nani kwa haraka wasaidike?
 
Kama hawajafanya jinai wananafasi ya kufanya mtihani,lakini pia Kama RC amebariki itakuwa ngumu kwa kuwa board ya rufaa ipo chini yake kwa maana makosa yaliyofanywa na wanafunzi yanastahiki kufukuzwa.View attachment 1760079
Unajua hata uamuzi wa bodi na ambao umebarikiwa na RC ni wa hasira tu,eti kwa vile mwaka jana waliandamana na hawa form six wakiwepo (walikuwa form five),basi watoe fundisho kwa watoto wote.
Binafsi naona hapo wameshughulika na matunda ya juu tu,badala ya kutafuta chanzo sahihi cha migogoro shuleni kila mara.
 
Back
Top Bottom