Wanafunzi Dar na Dharau kwa Wakubwa Wao

Wanafunzi Dar na Dharau kwa Wakubwa Wao

Atuongoze kwakweli...ila kimtaamtaa mtoto akizingua nampa mabanzi alafu natoaga kabisa ruhusa kamwite mzazi wako
Kumbe wee mbabe eeh yna4! ngoja ukutane na mwanamke wa Kizaramo aje amekufungia kibwebwe kama hujalazwa hospitali kwa maneno yake tu ya kukuchamba kwa kumgusa tu mwanae, wee una neno moja yeye maneno hamsini😀😀😀
 
[emoji16] [emoji16] [emoji16] unadhani naogopa maneno...siogopi hata kidogo na wenye watoto wananifahamu vizuri tu
 
[emoji16] [emoji16] [emoji16] unadhani naogopa maneno...siogopi hata kidogo na wenye watoto wananifahamu vizuri tu
Ila wazazi tubadilike kwakweli, hivi hatuoni fahari kua na mtoto aliyejengeka katika misingi ya heshima kwa watu wote, adabu kwa wakubwa na nidhamu kwa mambo ayafanyayo?
 
Ila wazazi tubadilike kwakweli, hivi hatuoni fahari kua na mtoto aliyejengeka katika misingi ya heshima kwa watu wote, adabu kwa wakubwa na nidhamu kwa mambo ayafanyayo?
Na kweli tubadilike..tulee watoto katika misingi iliyo mema..zamani mtoto akiwa na njia zilizo njema mzazi unapata sifa. "Mtoto wa Fulani ana adabu kweli" tofauti na Siku hizi "lile Toto la mama zai halina adabu toto jeuri" mweh mzazi unapewa sifa mbaya sababu ya ulezi m'baya TUBADILIKE jamani
 
Halafu watu hua hawajui tu, hata hao watoto wenyewe wanapokua watu wazima hua wanakumbuka sana na kuwaenzi wale waliowapa malezi ya adabu na heshima hata kama ni aunt zao au bibi zao kuliko kule walipodekezwa na kuharibiwa kitabia hata kama ni kwa wazazi wao
 
Tatizo ni wazazi na pia makondakta huwa tunafikiri pesa ndo kila kitu. Tunampa mtoto pesa ya nauli na kumwambia nimekupa pesa ili ukae usisumbuke makonda wasikusumbue. Konda naye anamkuta mwanafunzi kakaa ktk kiti anamwambia umelipa 200 alafu unakaa nyanyuka ktk kiti pisha wakubwa. Mwanafunzi naye anapisha ktk kiti huku akijua kuwa amenyanyuliwa ktk kiti kwasababu amelipa 200.

Siku nyingine mwanafunzi akitoa 400 konda anapokea kwa tamaa zake huku anamuona amevaa sare za shule na anamruhusu kukaa hata wakubwa wakiwepo. Kwa mwenendo huu Kwanini mwanafunzi akiwa na pesa ya kulipa nauli ya 200 asimdharau mtu mzima?

Tunapaswa kuwafundisha watoto kuhusu thamani ya utu kuwa haipimwi kwa fedha. Anayestahili heshima hupewa hata akiwa fukara. Watoto wa jinsi hii watakapokuwa na mali ndo wanakuwa mafedhuli, wakatili, hawajali mtu yeyote. Wanajiona wapo juu tu kwakuwa wana fedha. Watoto wanapaswa kufundishwa kuwa pesa haiwezi kufanya kila kitu.

Katika hili wazazi tuna nafasi kubwa ya kuwaelekeza vijana. Nakupa pesa hii lakini heshimu wakubwa, kama umechoka unahitaji kukaa jibu kwa heshima "nimelipa nikae kwasababu nina shida samahani".

Na makonda nao wanapaswa kuwarudishia pesa zao wanafunzi pindi wanapotoa zaidi, wachukue pesa wanayostahili tu. Kwanza ni wizi kwanini konda unachukua pesa ya mwanafunzi zaidi ya ile anayotakiwa kutoa?
 
Back
Top Bottom