Wanafunzi Jenipher na Caren wa Iringa girls wanahitaji ushauri wenu,enyi GREAT THINKERS

Wanafunzi Jenipher na Caren wa Iringa girls wanahitaji ushauri wenu,enyi GREAT THINKERS

Mwanangu alikuja na wazo kama hilo alipomaliza o level na nikamkatalia.

1. Kwanza nilimwambia mfumo wa kawaida wa nchi ni kusoma hadi form six ndipo uanze degree na kwa Kuwa lengo ni kupata degree ukimaliza diploma ya miaka 3 ni rahisi ukienda A Level kisha degree kuliko kupitia diploma

2. Pili chuo kuna uhuru ambao akienda kabla ya kufika 18 utamchanya na kumuharibia future kama asipokuwa makini

Alichukua ushauri wangu kwa sasa yuko 1st year Cardiff University UK. Wenzake walienda DIT Diploma ndio wako 3rd year na wakitoka hapo waanze degree. Wastage of time
Alafu post za kazi zinakuja kutoka diploma wanatakiwa watu 360 degree 5 ndo utajua hujui kwa tanzania option ya diploma ndo nzur kuliko hiyo ya advance kama unataka mwanao asiteseke sana kwenye ajira ila kama unaangalia kufika degree kwa haraka basi nenda tu advance
 
Shule ya A level ni shule iliyochangamka kwelikweli, sijui kwa nini watu wanaichukulia poa. Kiukweli nikiona CV ya mtu ambaye hana A level, huwa naona huyu mtu anakosa kitu flan hivi.
Na shule ya diploma ni shule ya kibabe hasa maana ukitoka hapo unakabidhiwa ofisi au idara kabisa sasa wewe na advance yako atakukabidhi nani ofisi
 
Commitment ya walimu A level nyingi nzuri iko vizuri ufundishaji na ufaulu

Diploma kuna walimu wabovu na wavivu acha kabisa ndio.maana hata huwezi jua chuo gani cha Diploma hufaulisha vizuri sababu vingi hamna kitu vinatoa wanafunzi average tu ambao hata sifa za kuingia chuo kikuu wengi hukosa sababu ya pass za chini
Embu nenda Sua pale au Dit au Must alafu uje useme tena walimu ni wabovu wanaofundisha diploma
 
Wanafunzi Jenipher na Caren wa Iringa girls wanahitaji ushauri wenu,

Wanafunzi Hawa walichaguliwa kujiunga kidato Cha 5 iringa girls mwaka huu,

Wameshareport lakini swala lao kubwa ni kwamba hawataki kusoma A level na hawakuijaza ktk machaguo ,waliopt chuo tu

Lakini wizara ikawatupa Iringa girls masomo ya sayansi.

Nikiwa kama Madam wao wa part-time, wamenifata na kuniambia kwamba hawataki kabisa A level wanataka waende chuo diploma 3 years,na wamejaribu kuongea na wazee wao wamesema Kama wanataka chuo wajisomeshe,

Sasa wamenifata kuniomba ushauri wafanye nn,maana wanaona kukaa huku A level ni kupoteza muda tu,

Hawa Watoto wanafikiria mpaka kutoroka shule,wapo dillema

NB: Jenipher baba ake ni komando JW

Caren mama ake ni Moja ya walinzi cruel ya Hangaya

MATOKEO YAO: Jenipher Ana Div I Pts 16

Caren Ana Div I-14

Ushauri kwenu wakuu GREAT THINKERS
Nitumie mawasiliano yao nichaague mmoja nimsomeshe 😋
 
Umenikumbusha story za kitambo mwe, siku za graduation hapo baada ya kula pilau tunasubiri gari ya kutoka zoo tupogkee wageni.. [emoji24]
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
toeni ushauri sio kuuliza maswali bora nini kati ya a level na kwenda chuo
 
Hii ni tabia ya watoto wa kike wa kisasa, wanapomaliza form 4, kitu kinachowajia kichwani ni kuwa na uhuru. Sasa na story za mitaani kwamba ukienda chuo unakuwa huru ila ukienda Advance unabanwa. Hili ndio swala linalowasumbua. Hapo wameshawaza kuvaa vitopu, skin jeans, kuweka nywele bleach na kumiliki iPhone ,,,, vyote hivyo wakiendelea na masomo.

Waendelee na form 5 hadi kieleweke, kwani wakifanyiwa masihara hao wanaelekea kuwa kama kina Mwajuma Nchokonoe.
 
Wanafunzi Jenipher na Caren wa Iringa girls wanahitaji ushauri wenu,

Wanafunzi Hawa walichaguliwa kujiunga kidato Cha 5 iringa girls mwaka huu,

Wameshareport lakini swala lao kubwa ni kwamba hawataki kusoma A level na hawakuijaza ktk machaguo ,waliopt chuo tu

Lakini wizara ikawatupa Iringa girls masomo ya sayansi.

Nikiwa kama Madam wao wa part-time, wamenifata na kuniambia kwamba hawataki kabisa A level wanataka waende chuo diploma 3 years,na wamejaribu kuongea na wazee wao wamesema Kama wanataka chuo wajisomeshe,

Sasa wamenifata kuniomba ushauri wafanye nn,maana wanaona kukaa huku A level ni kupoteza muda tu,

Hawa Watoto wanafikiria mpaka kutoroka shule,wapo dillema

NB: Jenipher baba ake ni komando JW

Caren mama ake ni Moja ya walinzi cruel ya Hangaya

MATOKEO YAO: Jenipher Ana Div I Pts 16

Caren Ana Div I-14

Ushauri kwenu wakuu GREAT THINKERS
M sisemi uongo ila elimu ya Advance kwa Tanzania hii tulofikia ni kupoteza muda tu
Unamaliza f6 vizuri huna ujuzi wowote ila mwenzako aloenda diploma tyr anaweza kuajiriwa kwa ujuzi wake

Mm kwa hali ilivo ya Tz simshauri mtu kwenda kusoma A level
 
Shortcut is a long way
Wakaze a.level degree moja kwa moja wimbi kubwa sana la vijana

wanaomaliza form four kwenda chuo wanafikiria kuajiriwa haraka wakati hali ni tofauti mtaani na ushindani ni mkubwa mnoo na matokeo yake wanalipwa chini ya kiwango stahiki maana muajiri hamlipi kama muajiriwa wake anamlipa kama mtu wa kujitolea hilo ni tatizo wasilolijua huku mtaani kingine

ni mawazo ya kuwa huru chuoni na kupoteza msingi muhimu wa elimu hasa a.level
 
Kitu huelewi, pita kimya. Nakupa mfano, mtoto kapata C ya Physics na kama kawaida Biology na Chemistry ana C au zaidi. Huyu kwenda PCB anapoteza muda maana ni ndoto za ndalia kuibuka na A ya Physics form Six ili aweze kuchukua MD. Sana sana akijitahidi atapata C au D au S. Hapo kama amekamia MD lazima arudi kuchukua CMT ambapo aliokuwa nao wakaenda Chuoni, watakuwa mwaka wa tatu wakati yeye akianza mwaka wa kwanza. Ili achukue MD atatumia miaka 5 na kama akikatisha form four atatumia miaka 3 tu. Amina68 nimekupa nondo
Naona wewe unafananisha pass za Form six na pass za Form Four; Vitu viwili tofauti kabisa
Mfano; Form Six mtu akiwa na pass mark ya C tatu za PCB; hapo ana Division One na anaweza kwenda UDactari (MD) bila shida yoyote. Hizo pass za A kwa Form six zinapatikana kwenye Arts (History, Kiswahili nk)
Kwenye saiyansi (PCB/M) ni za kuotea na ndio sababu wana mfumo tofauti wa kurank division)
 
Back
Top Bottom