Wanafunzi Jenipher na Caren wa Iringa girls wanahitaji ushauri wenu,enyi GREAT THINKERS

Alafu post za kazi zinakuja kutoka diploma wanatakiwa watu 360 degree 5 ndo utajua hujui kwa tanzania option ya diploma ndo nzur kuliko hiyo ya advance kama unataka mwanao asiteseke sana kwenye ajira ila kama unaangalia kufika degree kwa haraka basi nenda tu advance
 
Shule ya A level ni shule iliyochangamka kwelikweli, sijui kwa nini watu wanaichukulia poa. Kiukweli nikiona CV ya mtu ambaye hana A level, huwa naona huyu mtu anakosa kitu flan hivi.
Na shule ya diploma ni shule ya kibabe hasa maana ukitoka hapo unakabidhiwa ofisi au idara kabisa sasa wewe na advance yako atakukabidhi nani ofisi
 
Embu nenda Sua pale au Dit au Must alafu uje useme tena walimu ni wabovu wanaofundisha diploma
 
Nitumie mawasiliano yao nichaague mmoja nimsomeshe 😋
 
Umenikumbusha story za kitambo mwe, siku za graduation hapo baada ya kula pilau tunasubiri gari ya kutoka zoo tupogkee wageni.. [emoji24]
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
toeni ushauri sio kuuliza maswali bora nini kati ya a level na kwenda chuo
 
Hii ni tabia ya watoto wa kike wa kisasa, wanapomaliza form 4, kitu kinachowajia kichwani ni kuwa na uhuru. Sasa na story za mitaani kwamba ukienda chuo unakuwa huru ila ukienda Advance unabanwa. Hili ndio swala linalowasumbua. Hapo wameshawaza kuvaa vitopu, skin jeans, kuweka nywele bleach na kumiliki iPhone ,,,, vyote hivyo wakiendelea na masomo.

Waendelee na form 5 hadi kieleweke, kwani wakifanyiwa masihara hao wanaelekea kuwa kama kina Mwajuma Nchokonoe.
 
M sisemi uongo ila elimu ya Advance kwa Tanzania hii tulofikia ni kupoteza muda tu
Unamaliza f6 vizuri huna ujuzi wowote ila mwenzako aloenda diploma tyr anaweza kuajiriwa kwa ujuzi wake

Mm kwa hali ilivo ya Tz simshauri mtu kwenda kusoma A level
 
Shortcut is a long way
Wakaze a.level degree moja kwa moja wimbi kubwa sana la vijana

wanaomaliza form four kwenda chuo wanafikiria kuajiriwa haraka wakati hali ni tofauti mtaani na ushindani ni mkubwa mnoo na matokeo yake wanalipwa chini ya kiwango stahiki maana muajiri hamlipi kama muajiriwa wake anamlipa kama mtu wa kujitolea hilo ni tatizo wasilolijua huku mtaani kingine

ni mawazo ya kuwa huru chuoni na kupoteza msingi muhimu wa elimu hasa a.level
 
Naona wewe unafananisha pass za Form six na pass za Form Four; Vitu viwili tofauti kabisa
Mfano; Form Six mtu akiwa na pass mark ya C tatu za PCB; hapo ana Division One na anaweza kwenda UDactari (MD) bila shida yoyote. Hizo pass za A kwa Form six zinapatikana kwenye Arts (History, Kiswahili nk)
Kwenye saiyansi (PCB/M) ni za kuotea na ndio sababu wana mfumo tofauti wa kurank division)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…