Wanafunzi Kukosa Viatu ni ishara ya wazi ya Umasikini wa nchi

Wanafunzi Kukosa Viatu ni ishara ya wazi ya Umasikini wa nchi

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Posts
128,308
Reaction score
245,426
Huko Rwangwa ambako Rais Samia yuko ziarani , na ambako kila mwananchi aliyehudhuria Mapokezi ya Rais ameonekana ameshika bango la kumpomba , Wanafunzi hawana viatu .

Ndiyo maana Chawa wa Mama wameamua kuomba hela wanakojua wenyewe na kugawa kwenye Kaya Masikini huku wakiongozana na mama mwenyewe kwenye ziara hiyo

Rwangwa ni Jimbo linaloongozwa na Mbunge ambaye ndiye Waziri Mkuu , huyu ni miongoni mwa Wabunge waliopita bila kupingwa .

Screenshot_2023-09-18-18-07-32-1.png

Screenshot_2023-09-18-18-07-27-1.png
 
Biblia inasema! Masikini mnao siku zote!

Hii inamaanisha, umasikini hautaisha, lakini shida ni kwamba, ccm imesababishia watu umasikini

Watanzania wamekuwa wakilima na kutoa majasho wao, ccm wao wanaenda kuvuna!

Watanzania wakila, wenye kushiba ni maccm, tushangae wazazi watoto wao kukosa viatu?

Nawashangaa vijana bado wakiendelea kushadadia ccm! Upuuz
 
Mbona huko Lindi na Mtwara ni kawaida wanafunzi kuwa pekupeku!
Halafu wapo wanaong'ang'ana kuwa wanaweza kumbe wanatufelisha.Ndio maana hata mbao za majivu za kujifunzia udongoni,bila hata ya mkeka achilia madawati ni msamiati mgumu bado kwa wanafunzi wengi achilia mbali wazazi wao waliosomea madarasani enzi ya mkoloni, mjerumani na mwingereza.
 
Rushwa, ubadhilifu, Ubinafsi na anasa za roho mbaya zinaliangamiza Taifa!
Baada ya maisha ya duniani,kuni bora kabisa motoni ni anayejiita kiongozi wa Afrika.🏃🏃🏃🤸🤸🤸🤔🤔🤔😂😂😂
 
Huko Rwangwa ambako Rais Samia yuko ziarani , na ambako kila mwananchi aliyehudhuria Mapokezi ya Rais ameonekana ameshika bango la kumpomba , Wanafunzi hawana viatu .

Ndio maana Chawa wa Mama wameamua kuomba hela wanakojua wenyewe na kugawa kwenye Kaya Masikini huku wakiongozana na mama mwenyewe kwenye ziara hiyo

Rwangwa ni Jimbo linaloongozwa na Mbunge ambaye ndiye Waziri Mkuu , huyu ni miongoni mwa Wabunge waliopita bila kupingwa .

View attachment 2753744
View attachment 2753745
IMG-20230918-WA0042.jpg
 
Back
Top Bottom