Wanafunzi Law School mnayo nafasi ya kujipigania

Wanafunzi Law School mnayo nafasi ya kujipigania

hiyo ni kile kizazi mnaita cha Z, hawana akili na wana mambo mengi ya kupuuzi. Hizo shule mlizotika mlilishwa na vijiko km vitoto vichanga siyo elimu ya juu dogo. Mmeibiwa mitihani na kila aina ya magendo mkafaulu, law school hakuna magendo.
mwambie tena , hamna jinsi utafeli na upewe marks za bure , pale ndio sieving point kama hawezi faulu , kazi zipo nyingine za kufanya
 
sina mchango kivipi mwenzangu na mimi , nina law firm dar , ofisi dodoma na nairobi , i speak pure facts the law isnt for everyone , na wengi wa wanaochangia pale sio actual practising lawyers , mi mwenyewe nlirudi pale LST after years of practice na in one of the units nilifeli , ila sikufelishwa , in that unit ethics kiukweli sikuwa na relevant content, nlipass zingine zote na the one i failed nlifanya resit and passed , pale hamna cha tunajuana , students need to be keen pale , wengi nliokuwa nao classes ni kufanya mahusiano, movie etc , yaani tuache mbwembwe za hapa nje ww mwenyewe nenda in one of the those classes , ukitoka pale hutowai watetea tena wanafunzi , uliona wapi students wa law wanafunzwa practice na library in anyday haina wanafunzi wasiozidi 10 , utapass vp , tuwe wakweli sometimes

Uliyaona haya kwenye rejea nilizokupa ndugu?

Kwa hisani ya mkuu MALCOM LUMUMBA:

Anaandika mdau:

Binafsi naomba nisema yafuatayo kuhusu shule ya sheria Tanzania:

Mosi, kutokana na uhitaji wa elimu ya kusoma kwa vitendo (Post-Graduate Diploma in Legal Practice) haikutakiwa kuwe na shule moja nchi nzima tena ambayo iko kwenye mji kama Dar es salaam. Walau hizi shule zingekuwepo kikanda ili kuwaepusha na kadhia wale wanafunzi wanaotoka mikoa ya mbali kuja kurudia mitihani Dar es Salaam. Mtoto anasafiri kutoka Tarime, hana hata mkopo halafu anakuja Dar es salaam kufanya mtihani akiwa na 50/50 kwamba hilo somo analorirudia atafuaulu au lah.

Pili, mbinu ya kumpima mwanafunzi (Mode of Assessment) siyo rafiki kabisa na haizingatia utaalamu wa kisaikolojia kwamba wanafunzi wana uelewa tofauti. Mtoto anasoma mwaka mzima halafu anapewa mitihani 24 ndani ya mwaka ambayo kama akifeli hata mmoja basi anaweza kupoteza zaidi hata ya miaka 2 anarudia tu kozi hiyo hiyo. Kikawaida tulitegemea kwenye elimu ya vitendo wanafunzi wapimwe kupitia kazi nyingine muhimu ambazo lazima ziwe na alama, kama PRESENTATIONS, GROUP ASSIGNMENTS, CLINICS + WORKSHOPS and INTERNSHIP WITH MARKS.

Sasa wanaitwa DIPLOMA IN LEGAL PRACTICE huku wakichukua ada ya zaidi ya milioni moja, ilhali vipimo vyote vinatolewa kupitia mitihani. Hii siyo sahihi, kwasababu hata mahakamani kwenyewe wanasheria huwa hatuviziani ila tunapewa muda wa kujiandaa. Sasa mtoto anakaa INTERNSHIP miezi zaidi ya sita huku akija kukaguliwa kihunihuni tu mara moja, bila kupewa alama yoyote ile ya muhimu. Kwanini hawa wanafunzi wasipangiwe hata miezi miwili-miwili kufanya kazi la lazima zenye alamu mahakama za mwanza, mabaraza ya ardhi, mabalaza ya usuluhishi, dawati la jinsia ???

Jingine, ambalo nimeliona ni jambo la kipumbavu kufanywa na watu wanaojiita wasomi ni kitendo cha kutoa matokeo ya mitihani yote ya mwaka mzima ndani ya siku moja, baada ya mwaka mzima na miezi mitatu kupita. Kwanini matokeo ya ICA (Individual Continous Assessment), WPE (WRITTEN PRACTICAL EXAMINATION) na FINALS NON-CORE hayatolewi mapema, ili mwanafunzi ajue mbivu na mbichi na aweze kujipanga vizuri kwenye mitihani ya mwisho ??? Pia wawekewe utaratibu maalamu kabisa wa kuyarudia haya masomo wakati hata wako shule, hasa wiki moja baada ya kumaliza WPE ???

Lingine muhimu ni kwamba LST, kuna mitihani ya WPE (Written Practical Examination) ambayo kwingineko duniani mwanafunzi huifanya kwa kufanya tafiti pamoja na majadiliano na wanafunzi wenzake, kisha baadae huenda kufanya huo mtihani. Ilhali sasa pale LST, wanafunzi wanafungiwa masaa manne (4) wakisoma mavitabu, bila kuruhusiwa kuzungumza halafu wanapewa saa moja kupumzika, ili warudi kufanya mtihani huohuo kwa masaa matatu. (It's just emotional debilitating)

Tatu, hili la kulazimisha kila anayesoma sheria awe wakili nadhani ni jambo la kishenzi ambalo lilifanywa kwa mihemko bila kufikiriwa. Miaka yote huko nyuma watu tuliajiriwa kama STATE ATTORNEYS bila hata kuwa wanasheria. Tulitakiwa tu tufanye INTERNSHIP miezi tisa kwa ATTORNEY GENERAL halafu tunaenda kufanya BAR-EXAMINATION kule Arusha. Kinachoshangaza ni kwamba wengi ambao hawakupita Law School wako vizuri kuliko hata hawa watoto wenu wa Mawasiliano nyuma kule.

Kubwa zaidi, wanasheria tuko kwenye nyanja kuu mbili ambazo ni LEGAL PRACTITIONER (ADVOCATES) na JURIST (LEGAL SCHOLARS/LEGAL RESEARCHERS). Hawa ni watu wawili tofauti na wanafanya kazi tofauti kabisa, sasa ukitaka kuwalazimisha wawe kitu kimoja utakuwa unapuyanga mno. Leo hii ushauri wa sheria wa JURIST unaweza kuwa una uzito kuliko hata ORDINARY LEGAL PRACTITIONER, kutokana na tafiti na ufahamu. Sasa kwenye nchi fulani ya kusadikika, wenyewe kwasababu hawana SPECIALIZATION basi wanalazimisha kila mtu awe wakili, kwamba hata JURIST haweza kutoa ushauri kama hana muhuri. Just Lackadaissical and Nonsensical....

Nne, mtaala wa shule ya sheria ni wa kizamani sana na hauwezi kumfanya mwanafunzi awe vizuri kwenye soko la kimataifa. Kuna baadhi ya masomo tulitegemea yafundishwe pale LST, lakini hayapo kwenye mtaala. Mfano, INTERNATIONAL COMMERCIAL ARBITRATION, INVESTMENT LAW, BASICS OF INTERNATIONAL ECONOMICS LAW/ INTERNATIONAL TRADE AND FINANCE LAW. Nchi haina wataalamu wa haya masomo, sisi tunakomaa kufundisha PROPABATE & ADMINISTRATION OF ESTATES, COMMERCIAL LAW, LEGAL ETHICS, HUMAN RIGHTS and ACCOUNTS FOR LAWYERS masomo ambayo vyuo vingi vinayafundisha na vinaweza kuyafundisha vizuri.

Kesi kubwa kama zila za makinikia, DOWANS, ESCROW n.k zinahitaji mwanasheria walau awe anajua masomo ya INTERNATIONAL COMMERCIAL ARBITRATION, ambapo anatakiwa aifahamu mikataba mikubwa BIT (Bilateral Investment Treaties), pamoja na taasisi muhumu kama ICSID, PIC, ICC. Lakini sisi tunakomaa kuwafelisha watoto masomo kama ACCOUNTS. Sijui hii nchi haina watu wenye akili kabisa. Mambo ya ajabu yanafanyika na hakuna hata anayestuka.

Tano, mradi wa LST tangu mwaka 2006 marehemu Prof. Mukoyogo aliupinga kweli kwasababu aliona hauna maana zaidi ya kuwatengenezea ulaji baadhi ya wataalamu wa pale University of Dar es Salaam. Hivi kweli, tuna uhakika kwamba haya masomo ya LST hayawezi kufundishwa vizuri kwenye vyuo ambavyo wanafunzi wanasoma wakiwa wanatafuta Shahada ya kwanza kweli ???

Jambo jingine ni kwamba wataalamu wengi wa pale LST wameamua kufanya biashara ya vitabu. Wanatunga mitihani ambayo majibu yake utayapata kama tu umenunua vitabu vyao. Hili nilishawahi kuambiwa nikathibitisha mwenyewe kwenye baadhi ya vitabu. Hii ni tabia ya kishezi ambayo inaumiza na kukwamisha wengine huku wengine wakipata ukwasi mkubwa. Mwanafunzi anataoa pesa nyingi za Ada lakini hivyo vitabu havipo maktaba, utavipata mpaka umfuate mwandishi mwenyewe na umlipe 50,000. Kwanini msiweke vitabu vingi kule maktaba wanafunzi wakavisoma ???

Sita, hivi inawezekanaje mwanafunzi ambaye amefauli vizuri shahada yake afeli vibaya kwa kiwango cha DISCONTINUE pale LST ??? Ina maana huyu mwanafunzi hafahamu kitu chochote kabisa ??? Lakini, kubwa zaidi ni hili la wanafunzi 600 kuanza pamoja, lakini wanaofaulu ni watu 30, huku nusu ingine ikiwa inafanya SUPPLEMENTARY au DISCONTINUED. Sijui kwanini hili haliwastui Majaji na Wizara. Watu hufeli, lakini siyo kwa kiwango hicho ambacho kinafanyika pale Law School.

Pia, pale pana rushwa sana ya ngono, kukomoana na kubadilishiana matokeo. Kuna jamaa niliwahi kuwa naye mahakamani aliwahi niambia kwamba kuna rafiki zake wanafundisha pale walimuahidi kwamba watamfaulisha, na kweli alifauri vizuri hadi tukashangaa. Alikuwa na maswali hata kabla mitihani haijaanza. Nikasema HIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIII...

TANZANIA HAKUNA KITU KINACHOFANYA KAZI VIZURI KUSEMA TUNAWEZA JIVUNIA
 
Yaani miswada ijadiliwe na wabunge hata wa drs la saba ila kuitafsiri ikiwa sheria ndo ufaulu uwe mgumu hivi?

Hapa ndipo ccm kupitia waingereza wanapotuweza. Wametuaminisha kuwa elimu ni tabu sana kuipata na sio nyepesi. Waingereza walifanya hivi kurahisisha kututawala. Elimu ni ufahamu unaorithishwa kwa binadamu ili kurahisisha maisha katika sekta fulani.
mkuu miswada ya bunge ni kama hoja vile , ila wale wabunge hupitisha mambo broadly , pale bungeni wapo legal assistants na mawakili , wanachukua ile hoja ya wabunge na wanaiandika in form of sheria sasa , plus legislative drafting na issues hizo za wabunge ni ina form asilimia ndogo sana ya law , sheria bwana ni wide sana , na sio ngumu inahitaji bidii tu , sema hawa vijana wanataka utelezi , akitoka LST umpeleke mahakama yyte internationally hajitambui . ningetamani waliofeli wawekwe kwa debate na waliopita uone tofauti ,ndo uelewe
 
  • Kicheko
Reactions: Tsh
Wewe ukiacha kuwa dogo basi madogo hawapo tena:

"Ni muhimu kutambua Tanzania ni jamii ya watu waliojaa wivu, choyo, husuda, fitna, ujinga, upumbavu na ujuaji uliopitiliza."

Kama wewe mliangaziwa vilivyo kwenye mada.

Kazi yako ya laana wewe, acha kuitamka tamka huku unatia aibu:

Prof. Shivji na maoni yake kuhusu kadhia ya Law School
wacha chuki , kama hukupita , fanya mengine ,sheria waachie hao 23 waliopita , walitia jitihada mno wakafaulu , wataka utelezi tu mpaka in the field of law , nenda tena LST , kafanye ushenzi , uvivu ,mahusuiano ya kizembe na huo ujuaji , utapata F ilyosimama , uwe faliure tu , kama hujakaa ukatafakari why you failed pale , au ukachukua ya maswali urudi kwa those instructors ujue wapi ulikosea hizo ripoti za sijui kina nani hazitakusaidia , tia bidii
 
Wewe unazijua kuliko hawa?

Kwa hisani ya mdau aikambe:

Anaandika mdau (11 Oct 2022):

Nimeona mada za kuchambua taarifa ya kufeli kwa wanafunzi Law School of Tanzania.

Binafsi na mimi nimepitia Law School, na haya ndiyo ninayoyafahamu kuhusiana na hiki chuo.

1. Law School kiuhalisia, siyo sehemu ya mafunzo kwa vitendo kama mnavyosikia redioni.

2. Somo la field lipo, ila marks zake hazihusiki kwenye kubaini ufaulu. Yaani alama za somo la field hazina maana kwenye GPA calculation maana hazitambuliki.

3. Wanafunzi wa Law School hufundishwa kwa nadharia darasani, na kuingia semina kama ilivyo vyuo vikuu.

4. Mwalimu mmoja hutoa mhadhara kwa wanafunzi wote 600+ na akimaliza anaingia mwingine hadi siku inaisha.

5. Mada zinazofundishwa Law School ni zilezile mwanafunzi alifundishwa vyuoni ngazi ya degree na hakuna tofauti.

6. Muda wa mitihani haupo fair. Kwenye mtihani mmoja, kunakuwa na maswali ya kuandaa hati za mashtaka na madai nyingi mno kiasi kwamba muda wa kuandaa hati hizo hautoshi. Kwa wasijua, hati za kisheria uandaaji wake unahitaji kurejea vifungu vya sheria mbalimbali ambazo unakuwa unazo mezani(Acts).

7. Wahadhiri wa Law School huamini kwamba wanafunzi wao watafeli na mtu akifaulu wanashangaa sana. Yaani wapo kama miungu watu. Pale Law School hata secretary anamdharau mwanafunzi na anataka umuinamie kumsujudu.

8. Mahakimu, na waajiriwa wengine wenye uzoefu kwenye sheria wakienda kujiendeleza Law School nao hufeli pia.

9. Kuna wakati mahakimu walishauriwa wasijiendeleze Law School maana ni fedhea hakimu mzoefu unafeli Law School. Badala yake waliaambiwa watapewa utambulisho maalum kwamba wamefuzu vigezo vya sheria kwa vitendo.

10. Suplementary yaani mitihani ya kurudia haina kikomo Law School. Unaweza hata ukakaa na sup. hata miaka 40.

11. Law School ukikata rufaa ya matokeo haipatiwi majibu na unaweza ukaanza apya kusoma na kumaliza bila kupata majibu ya rufaa.

12. Law School unasoma masomo yote uliyofundishwa kwenye shahada ya sheria kwa miaka minne, lakini ukifika Law School unafundishwa kwa miezi 6 na unapewa mitihani. Halafu miezi mingine 6 unaenda field.
Stupid system.
 
wacha chuki , kama hukupita , fanya mengine ,sheria waachie hao 23 waliopita , walitia jitihada mno wakafaulu , wataka utelezi tu mpaka in the field of law , nenda tena LST , kafanye ushenzi , uvivu ,mahusuiano ya kizembe na huo ujuaji , utapata F ilyosimama , uwe faliure tu , kama hujakaa ukatafakari why you failed pale , au ukachukua ya maswali urudi kwa those instructors ujue wapi ulikosea hizo ripoti za sijui kina nani hazitakusaidia , tia bidii

Unaanza kurukia treni kwa mbele sasa. Kwani unafahamu hayo.yalianzia wapi ndugu?

Nilikupa rejea uliziona?

Nyingine iko hapa wewe si umesema una firm?

Kwa hisani ya mdau aikambe:

Anaandika mdau:

Nimeona mada za kuchambua taarifa ya kufeli kwa wanafunzi Law School of Tanzania.

Binafsi na mimi nimepitia Law School, na haya ndiyo ninayoyafahamu kuhusiana na hiki chuo.

1. Law School kiuhalisia, siyo sehemu ya mafunzo kwa vitendo kama mnavyosikia redioni.

2. Somo la field lipo, ila marks zake hazihusiki kwenye kubaini ufaulu. Yaani alama za somo la field hazina maana kwenye GPA calculation maana hazitambuliki.

3. Wanafunzi wa Law School hufundishwa kwa nadharia darasani, na kuingia semina kama ilivyo vyuo vikuu.

4. Mwalimu mmoja hutoa mhadhara kwa wanafunzi wote 600+ na akimaliza anaingia mwingine hadi siku inaisha.

5. Mada zinazofundishwa Law School ni zilezile mwanafunzi alifundishwa vyuoni ngazi ya degree na hakuna tofauti.

6. Muda wa mitihani haupo fair. Kwenye mtihani mmoja, kunakuwa na maswali ya kuandaa hati za mashtaka na madai nyingi mno kiasi kwamba muda wa kuandaa hati hizo hautoshi. Kwa wasijua, hati za kisheria uandaaji wake unahitaji kurejea vifungu vya sheria mbalimbali ambazo unakuwa unazo mezani(Acts).

7. Wahadhiri wa Law School huamini kwamba wanafunzi wao watafeli na mtu akifaulu wanashangaa sana. Yaani wapo kama miungu watu. Pale Law School hata secretary anamdharau mwanafunzi na anataka umuinamie kumsujudu.

8. Mahakimu, na waajiriwa wengine wenye uzoefu kwenye sheria wakienda kujiendeleza Law School nao hufeli pia.

9. Kuna wakati mahakimu walishauriwa wasijiendeleze Law School maana ni fedhea hakimu mzoefu unafeli Law School. Badala yake waliaambiwa watapewa utambulisho maalum kwamba wamefuzu vigezo vya sheria kwa vitendo.

10. Suplementary yaani mitihani ya kurudia haina kikomo Law School. Unaweza hata ukakaa na sup. hata miaka 40.

11. Law School ukikata rufaa ya matokeo haipatiwi majibu na unaweza ukaanza apya kusoma na kumaliza bila kupata majibu ya rufaa.

12. Law School unasoma masomo yote uliyofundishwa kwenye shahada ya sheria kwa miaka minne, lakini ukifika Law School unafundishwa kwa miezi 6 na unapewa mitihani. Halafu miezi mingine 6 unaenda field.
 
mkuu miswada ya bunge ni kama hoja vile , ila wale wabunge hupitisha mambo broadly , pale bungeni wapo legal assistants na mawakili , wanachukua ile hoja ya wabunge na wanaiandika in form of sheria sasa , plus legislative drafting na issues hizo za wabunge ni ina form asilimia ndogo sana ya law , sheria bwana ni wide sana , na sio ngumu inahitaji bidii tu , sema hawa vijana wanataka utelezi , akitoka LST umpeleke mahakama yyte internationally hajitambui . ningetamani waliofeli wawekwe kwa debate na waliopita uone tofauti ,ndo uelewe
Ok boss....
 
Sijui NI utawala wa NCHI? au hakuna wenye uwezo wa kuchambua mambo na kubaini kinachoendelea pale?

Hivi Watanzania tupo kama Nyumbu tunaangalia wenzetu wanaliwa tunadhani hayatuhusu.
Hivi tija ya hiyo SHULE inapimwa na Nani? Kwani kunaugumu gani kupitia mitihani ya waliofeli na waliofaulu!? Kama Kuna tatizo je,hakuna wa Kufuatilia Muundo wa hiyo SHULE pamoja na Walimu wake?

Tunazalisha watu wa hatari ambao UTENDAJI KAZI WAO utatutesa Kwa MIAKA mingi ijayo.
 
Wa kwanza kuliwa kichwa ni huyu hapa:

Waziri Ndumbaro awajibishwe kwa matokeo mabovu Law School
 
Hivi uongozi wa Law school nao wako comfortable kabisa wanaendelea na enrollment ya wanafunzi wengine regardless ya kufaulisha wanafunzi kwa 3%?
Je, wanayo kitengo cha research na quality assurance ya elimu wanayotoa hapo ili wawapatie wananchi ambao ni wadau wao?

Tunaposema kuwa wananfunzi wanatoka vyuo vyetu vikuu wakiwa hawana uwezo wa kutosha kuendelea na elimu inayotolewa hapo Law School, je kwanini wasichujwe kwa mitihani ndani ya mwezi mmoja baada ya wao kufanya usahili ili kuepuka kadhia hii inayotokea mwishoni?

Kweli Law school hawaoni kuwa na wao wanastahili lawama kutoka kwa wadau wa elimu kuhusiana na matokeo? Yaani wabakie na wananfunzi wasiyo na uwezo muda wote huo ili waje kuwachuja mwishoni!!!!

Kwa style hii Law school inaweza kujiuza na kuvutia wageni Kuja kupata elimu wanayotoa hapo? Watafiti fanyeni tafiti kuna shida hapo Law school (Uongozi wa chuo, walimu pamoja na wanafunzi).
 
Back
Top Bottom