Atlast nimempata
JF-Expert Member
- Jun 3, 2011
- 585
- 1,166
Nina watoto wawili wanasoma shule za bweni za serikali kitaifa. Mmoja yuko kidato cha sita mwingine kidato cha kwanza. Wamesema wanaruhusiwa kulala kuanzia saa nne usiku na kuamka saa tisa na nusu hivi.
Hapo mtoto akiwahi kulala atakuwa amelala masaa matano na nusu au pungufu ya hapo kwasababu kuna muda wa kutembea kutoka madarasani hadi mabwenini na muda kujiandaa kulala, hivyo inaweza kuwa chini ya masaa 5 ya kulala. Mimi nilisoma shule za bweni hizohizo lakini tulikuwa tunaruhusiwa kulala saa nne na kuamka saa kumi na moja alfajiri, masaa saba.
Sasa hili la kulala masaa pungufu ya matano, kiafya hikoje? Kwa mtoto aliyeanza kidato cha kwanza na miaka 10-11 kama wengi wa watoto wa siku hizi wanaosoma wakiwa wadogo, lazima changamoto ya kiafya iwepo!