Mfano tu wa mada mezani,tuiweke hivi;
Mimi natokea mkoa X,kule kwetu mkoani kubandua tiles na kupanda miti au maua chumbani tunamolala ni kawaida,nimehamia mkoa ambao wewe una nyumba yako nakuja unanipangisha chumba na hapo jirani na kwako yupo mwenyeji wa kwetu tunaefanana tabia(kutoa tiles na kupanda mti au uwa ndani ya chumba),na wewe mwenye nyumba kwa kunijua kabisa kwamba mimi ni mkorofi linapokuja suala la kulinda itikadi yangu unanielekeza kabisa kwamba bwana huyo hapo jirani ni mwenzako nenda kapange kwake ndiye mtawezana!
Mimi nakwambia hapana hapa hapa kwako pananifaa(kumbuka umeshanipa mkataba wako unaosema siruhusiwi kuongeza au kupunguza chochote ndani ya chumba na nimesoma nikasema nimeelewa),mimi baada ya muda mfupi naenda serikali ya mtaa au JF kama hivi kukushtaki kwamba unaninyanyapaa hutaki kunipa uhuru wa kutoa tiles nipande uwa na mti ndani ya chumba nilichokwisha kukulipa kodi ili niishi itikadi yangu!
Unanionaje mkuu,hapo mimi nina akili timamu?maana mwenzangu ambaye ningewezana nae hata nipande mbuyu chumbani angenielewa ulishanionyesha na nikajua mpaka alipo lakini sikwenda leo ning'ang'ane kwako na mkataba kabla sijasain ulinipa nikausoma vizuri then leo yale uliyoyakataa mule nataka uyavunje kisa uielewe itikadi yangu,zipo jamii zinafanya mambo ya kijinga sana dunia hii inabidi zijitafakari hata kama wewe ni mmoja wao badilika.