Wanafunzi wa vyuo vikuu Marekani wakaribishwa kusoma Iran na Yemen kama watafukuzwa kwa kuandamana

Wanafunzi wa vyuo vikuu Marekani wakaribishwa kusoma Iran na Yemen kama watafukuzwa kwa kuandamana

acha uongo Iran vitu vingi vyao vimetengenezwa undersupevision kutoka russia,china,south korea...kuna interview ya balozi wa Iran kipindi cha nyuma hapa nchini anasema wayahudi nchi kwao ndio wama hold biashara kubwa na kwenye sekta ya elimu pamoja na uchache wao,alikuwa akijibu swali kwanini wana uhasama na wayahudi.
HUNA EXPOSURE WE JAMAA NARUDIA TENA HUNA EXPOSURE.
Ninaifuatilia hiyo Iran kuliko unavyoifuatilia wewe.
Iran ina mifumo yake ya elimu ila ina recruit walimu ama maprofessa toka China na Russia.
Kiteknolojia ya silaha Russia ndio mshirika wake mkubwa wa kushare naye teknolojia na kielimu ya viwanda China ndio mshirika wake wa kushare naye teknolojia.
NA KWA SASA IRAN INAO UWEZO WA KUUNDA CHOCHOTE PASI NA MSAADA WOWOTE.
PIA UACHE UONGO SOUTH KOREA HANA URAFIKI NA IRAN BALI NI NORTH KOREA.
USITUDANGANYE HAPA.
 
sasa cha ajabu nini si mpambane kuliko kulialia au jino kwa jino,jihad,fatwa.. havijafua damu mbele ya wayahudi?Hao us na westerners demokrasia itawaponza unampuuziaje koboko aliyeingia ndani mwako!
Wanapambana ila muache kuegemea upande.
Wacheni kuweka vikwazo vya kipumbavu kwa watakaiosaidia Palestina mathalan Lebanon,Yemen na Iran.
Maana Israel anasaidiwa na USA na EU ila Palestina akisaidiwa mnaiwekea vikwazo nchi inayoisaidia Palestina.
MUNAOGOPA NINI PALESTINA IKIUNGWA MKONO!?
Pia acheni uoga ruhusuni Palestina amiliki maji/marine border,anga na jeshi.
MUNAOGOPA NINI WAO KUMILIKI SOVEREIGNTY!?
 
Vuguvugu linaloendelea nchini Marekani kwa wanafunzi wa vyuo vikuu kuandamana kuhusiana na vita vya Israel na Palestina limeingia hatua nyengine baada ya viongozi wa Iran na Yemen chini ya Houth kutoa nafasi kwa wanafunzi wa vyuo hivyo kama watafukuzwa kwa kutekeleza wajibu wao wa kidemokrasia.

Maamuzi hayo yamekuja wakati polisi nchini Marekani wakiendelea kuwakamata wanafunzi hao na kutishia kuwafungulia mashtaka huku vyuo wanavyosoma navyo vikitishia kuwafukuza kutoka vyuo hivyo.
Democrasia inaminywa huko USA.
 
Vipi kuhusu demokrasia na uhuru wa kufanya maaamuzi binafsi kama vile wadada kuvaa vipensi au suruali za jeans? Ahahahahaha!!!
Demokrasia wewe unaitizama kwa upana gani ama kwa maana gani!?
USA unayoisifia ndio baba wa demokrasia duniani katika maandamano alipiga wazungu wenzake virungu hadi wanawake walifanyiwa assault na kutolewa damu,je hiyo ndio demokrasia!?

Uhuru upo ila kila nchi/sehemu ina sheria zake,hivyo fuata sheria za sehemu unazoenda.
Kwani USA si wana sheria zao ikiwemo kutokuruhusu WANAWAKE KUVAA NIQAB WAINGIAPO VYUONI!?
Je hapo si utakua umenyima uhuru wadada wanaopenda kuvaa NIQAB!?
Ila ni sheria na watu wanafuata.
 
waende wakajifunze unyama wajute.
Unyama upo USA na western nations au nikukumbushe unyama uliopo huko!?
Sema tukukumbushe.
-Usisahau USA ni miongoni mwa mataifa yanayoongoza kwa mauaji ya askari kwa watu weusi.
-Usisahau USA iliwahi kufanya mauaji ya kimbali ya watu weusi.
-Usisahau USA bado kuna neo-slavery na ili kulituliza hilo wameamua kwa wale watakaofanyiwa neo-slavery watalipwa fidia na kupewa green card.
-Usisahau USA bado kuna ubaguzi wa rangi ambao mwingi hauripotiwi.
-Usisahau USA ni miongoni mwa mataifa yenye domestic na sexual violence tena hapo kwenye sexual violence hadi watu mashuhuri huhusishwa.

Unataka kutuambia nini wewe!?
Hii dunia yenyewe imechafuliwa na USA kwa kufadhili mapinduzi katika serikali za watu kisa kulinda maslahi yake kwa hayo mataifa.
Sisi sio watoto aisee tunaijua hii dunia iendavyo.
 
Exposure huna ndicho nachosema.
Au unataka ushahidi zaidi!?
Nikutajie shule za WaYemeni hapa Tanzania na mifumo yao ya elimu ukafuatilie zilivyo?
Pia nikutajie teknolojia waliyo nayo Yemeni na Iran na kipi wanaweza kufanya!?
Iran/Persia imevumbua vitu vingi ikiwemo SULPHURIC ACID uliyotumia katika titration form 3 chemistry.
Geopolitical issues ndio zimezidogosha hizi nchi maana external sovereignty yao imechafuliwa kwa vikwazo vya kiuchumi na vita.
Tanzania hata behewa huwezi kujenga wenzako Iran na Yemeni wanao uwezo wa kukuundia ENGINE YA TRENI.
Em sema tena.
 
Demokrasia wewe unaitizama kwa upana gani ama kwa maana gani!?
USA unayoisifia ndio baba wa demokrasia duniani katika maandamano alipiga wazungu wenzake virungu hadi wanawake walifanyiwa assault na kutolewa damu,je hiyo ndio demokrasia!?

Uhuru upo ila kila nchi/sehemu ina sheria zake,hivyo fuata sheria za sehemu unazoenda.
Kwani USA si wana sheria zao ikiwemo kutokuruhusu WANAWAKE KUVAA NIQAB WAINGIAPO VYUONI!?
Je hapo si utakua umenyima uhuru wadada wanaopenda kuvaa NIQAB!?
Ila ni sheria na watu wanafuata.
Hujajibu swali langu. Iran itakubali mabinti wavae vipensi chuoni na mtaani?
 
basi tu natamani dunia ingekua na usawa. tukaishi bila kujikweza na kubaguana lakini HAITAWEZEKANA. mwanadamu ni kiumbe wa hovyo mharibifu.
 
Silaha anazotengeneza Iran US hawana ndio maana wanaihofia Iran siku zote, ni kutokana na taaluma mkuu kule Marekani sana sana utapewa elimu ya mwanaume kuolewa na kupata haki zenu za msingi kama hizo
Unaota ndoto za mchana.
 
Iran ni taifa la wasomi kijana.
Ifuatilie Iran vizuri,hata hivyo vifaa tiba vingine hususan vya upasuaji viligunduliwa na Iran.
Iran ni taifa lenye mifumo bora ya elimu.
Ila uhasama na figisu za wamagharibi taifa la Iran limedogoshwa.
Bullshit ...
 
Sasa mbona US wako busy sana kutaka kujua silaha alizotengeneza Iran na wanaihofia, na munasema waarabu hawana elimu, elimu iko Ulaya na Marekani
Umeulizwa swali badala ya kujibu unaleta bla bla ...
 
Bullshit ...
Toa hoja kupinga hoja sio mipasho ya Khadija Kopa!
Can you defend what you claim about me talking bullshit!?
Iran ina teknolojia ya ;
-Kuunda magari kuanzia injini.
-Kujenga reli aina yeyote kasoro broadway na Maglev.
-Kuunda injini za treni.
-Kujenga miundombinu mikubwa mathalan mabwawa makubwa na madaraja makubwa ya aina yeyote.
-Kuunda silaha aina zote.

Unakumbuka kitu kinaitwa PERSIAN CARPETS?
Kipindi hiko Afrika mlikua hata kushona nguo hamjui.

Lete facts sio ushostito wa kusema "bullshit".
 
Vyuo vya ulaya na US vilitishia dunia zamani lakini katika dunia ya leo ukienda Apollo hosp. Kule india wataalam wa moyo, upasuaji wa ubongo wabobez waliopo pale wengi wamesoma india, china, Thailand, Singapore n.k Mfano mwingi ni Iran unasoma pale hadi unatengeneza hypersonic missile hata guided missile sasa wewe mweusi nenda kasome huko ulikokariri halafu uone kama utatengeza hata compressor ya baiskeli
Naunga mkono hoja!tatizo marekani na nchi za magharibi walifaulu ku brainwash dunia kuwa kila kitu bora na kizuri vinatoka kwao kitu ambacho si kweli kuna mataifa mengi yameizipita hizo nchi kiuchumi,technology,kielimimu n.k mfano nchi kama urusi,china n.k zipo mbele sana sema hazina kiki kama nchi za magharibi
 
Unatakiwa ukumbuke kuwa Israel ndio ilianza.
Mnamo August wayahudi wakisaidiwa na IDF walivamia makazi na mashamba ya wapalestina na kuyavunja na kujimilikisha ili kufanya expansion.
Au umesahau kuwa EU imetoa sanctions kwa jewish settlers!?
Au mnadhani sisi wajinga hatujui kufuatilia habari!?
Pia mkumbushe kuwa hakuna taifa linaitwa Israel !bali kuna Palestine
hiyo Israel iliyopo sasa imeptikana kwa kuwaua wapalestina na kuchukua maeneo yao kibabe toka mwaka 1948 hiyo Israel ni wavamizi wa ardhi ya wapalestina ila Palestine ikijitahidi kurudisha ardhi yao wanaitwa magaidi.
 
Toa hoja kupinga hoja sio mipasho ya Khadija Kopa!
Can you defend what you claim about me talking bullshit!?
Iran ina teknolojia ya ;
-Kuunda magari kuanzia injini.
-Kujenga reli aina yeyote kasoro broadway na Maglev.
-Kuunda injini za treni.
-Kujenga miundombinu mikubwa mathalan mabwawa makubwa na madaraja makubwa ya aina yeyote.
-Kuunda silaha aina zote.

Unakumbuka kitu kinaitwa PERSIAN CARPETS?
Kipindi hiko Afrika mlikua hata kushona nguo hamjui.

Lete facts sio ushostito wa kusema "bullshit".
Kwa kumtaja Khadija Kopa na kutumia neno "shostito" umeshaonyesha ni mtu wa aina gani. Anyway, Katika vitu vyoote ulivyotaja ni kitu gani nchi za magharibi hazitengenezi? Pia lete ushahidi kwamba hivyo vitu viligunduliwa Iran. Halafu unaongea mambo ya ancient Iran, sio Iran hii ya kina Ayatollah. Iran ya sasa imezidiwa hata na Qatar tu.
 
Back
Top Bottom