Wanafunzi wa vyuo vikuu vya Sudan wahamishiwa vyuo vikuu vya Tanzania. Hongera kwa Serikali ya Tanzania

Wanafunzi wa vyuo vikuu vya Sudan wahamishiwa vyuo vikuu vya Tanzania. Hongera kwa Serikali ya Tanzania

Dada zetu Kwa Sasa tunaomba mtupishe kwanza ,tuko na shughuli ya Kitaifa ya Kupokea Wageni kutoka Sudan ❤️❤️



Screenshot_20230620-064531.jpg
 
Leo nimeamka ninaumwa, natarajia niende Muhimbili muda huu, kwani wanaanza kupima saa ngapi 🤣 🤣
 
Ushauri wangu wasiishie kuwaleta wa kada ya afya tu hata kada nyingine vyuo vyetu bado vina nafasi za kutosha
 
Hongera kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.Hasa Rais wetu mpendwa kwa kupokea Wanafunzi wa Udaktari toka nchini Sudan.
Rais anaingiaje hapa mkuu?, tupunguze kujipendekeza kusikokua na ulazima sana
 
Hongera kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.Hasa Rais wetu mpendwa kwa kupokea Wanafunzi wa Udaktari toka nchini Sudan.

Ikumbukwe nchi ya Sudan ipo katika vita vya wenyewe kwa wenyenye. Mungu akawape utulivu, wepesi na waendelee vema na masomo yao katika Chuo cha Kikuu cha tiba Muhimbili.

---
Wanafunzi 150 wa udaktari kutoka Chuo Kikuu cha Tiba, Sayansi na Teknolojia (UMST) cha Khartoum nchini Sudan wamehamishiwa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) ili kukamilisha mwaka wao wa mwisho wa masomo.

Akiongea wakati wa kuwakaribisha wanafunzi hao, Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Prof. Mohamed Janabi amesema kuwa hali ya mapigano ya wenyewe kwa wenyewe yanayoendelea nchini Sudani imesababisha kufungwa kwa Vyuo na baadhi ya shughuli kusimama hivyo Wataalamu hao kushindwa kuendelea na ratiba yao ya masomo ya kawaida.

“Wanafunzi hawa wapo mwaka wa tano wa shahada ya kwanza ya utabibu, ambapo katika mwaka huo, mafunzo hufanyika kwa vitendo zaidi, hivyo Madaktari hawa Wanafujzi watafanya mzunguko (Rotation) katika idara mbalimbali ikiwemo idara ya upasuaji chini ya usimamizi wa Madaktari bingwa ili kuhakikisha wanapata maarifa yanayotakiwa”

Amesema kuwa MNH itatoa fursa kwa Wataalamu hao kujifunza kama ambavyo inatoa kwa Wataalamu wengine wa ndani na nje ya Nchi na hata baada ya kumaliza masomo kama watapenda kufanya mafunzo tarajali (Intenship) MNH itawapa nafasi hiyo.

Kwa upande wake Ruba Anwar Salih ambaye ni Kiongozi wa kundi la Wanafunzi hao amesema kuwa wamefurahi kupata fursa ya kuendelea na masomo katika Hospitali kubwa na yenye wataalamu wa kutosha, ni imani yao kwamba watapata fursa nzuri ya kujifunza.

View attachment 2662913View attachment 2662914View attachment 2662915
Tupunguze kujipendekeza kusikokua na umuhimu, Sasa rais anahusikaje hapa?

Sent from my itel L5007 using JamiiForums mobile app
 
Kila nikiingia kijiweni kwa facebook, kwa twitter ,kwa Whatup habari ya town ni Swala wa Muhimbili!

Mshangao wa wengi ni kwanini "Warembo" wale wa KHARTOUM wamevuka mipaka yooote at last wameamua kuja kusettle kwa Mama Samia Suluhu Hassan?Kweli kwetu Tanzania ni pazuri!

Sisi ndio Tanzania Bwana!Nchi ya Amani!

"..Tanzania yetuuu ndio Nchi ya kusifika,watuu wote ulimwenguni ...wanajuaa,Tanzaniaa yetu ndioo Nchi ya furahaaaa..."

Am proud of my Tanzania!

FB_IMG_1687299012043.jpg
FB_IMG_1687300058919.jpg
Screenshot_20230621-013602.jpg
FB_IMG_1687278693595.jpg


Sent from my Infinix X6511B using JamiiForums mobile app
 
Dada zetu kutokea Sudan wametingisha mitandao kidogo. Tena na hivi ligi zimepoa poa, amsha amsha sasa hivi zipo kwa hao warembo.
Alafu kwenye kubeti sasa kuna michezo ya kuweka hela msimu huu kweli? Au ndo watu wakaushe mpaka ligi zitakaporudi?
 
Ila nyie watu mna hisia za udini kali loh Sudani iko Africa ukuraini iko ulaya.......loh
Yaani kwa ubwege wako hukusikia wa-Tz waliokuwa wanasoma Ukraine walirudi na hakuna aliyewapokea? Kwa hiyo kosa lao ni kusoma ulaya?
btw. kwa nini aliyetangaza kupokea hao wanafunzi ni Mohammed Janabi? Kwani naye ni mkuu wa chuo?
 
Back
Top Bottom