Shukuru Mungu wewe umepata watoto wapole wenye akili na usiombe ikutokee, Watu wanaombaga mpaka police mtoto akae sero, Mimi nimesoma mpwapwa Sekondari, kipindi Cha mwishoni miaka 90s walihamia wanafunzi wachache kutoka tambaza, kipindi hicho Tambaza ilifutwa sababu ya utukutu na watoto wote wakahamishiwa shule nyingine. Ndani ya miez miwili tu wakachoma nyumba ya mwalimu moto. Yan upate mtoto wa kiume mtundu utumie ushauri nasaha labda waache Kufundisha wadili na watukutu siku Nzima. Hao unaosema wanachelewa shule sababu za kifamilia wapo ni wachache sana na mtoto mwenye akili akiwa na shida hiyo anamuona mkuu na kujieleza.
Narudia mkuu, hujawahi kukutana na mtoto mtukutu wewe na usiombee. Hayo mambo ya kufananisha watoto wazungu na wakibongo lazma uangalie na utofauti mazingira.
Kilichoniuma zaidi kupiga watoto underage yaani mwalimu anapiga mtoto wa miaka 6 sijui 7 mpaka anaua
Anampiga mtoto mdogo ngumi ya tumboni pamoja na viboko sasa ni haki hiyo?
Tusiwape vichwa hawa waalimu
Kweli wapo watukutu sana na hao nimewaona mpaka wanafukuzwa na shule kabisa wale wanaitwa nunda yaani hasikii kitu ila Waalimu enzi zetu walikuwa ni wenye hekima pia
Mtoto anaadhibiwa sio kwa jazba na hasira za kibangi bangi hapana bali walikuwa wanawachapa na kuwapa adhabu
Lakini sasa imekuwa kila leo tunasikia mwalimu kamjeruhi mwanafunzi au kaua kabisa
Hebu niambie hata kama ulisoma zamani au miaka ya karibu je hakuna suluhu yoyote mpaka kuuwa kwa fimbo?
Naona adhabu ya fimbo ingefutwa maana sisi kama kuchapwa zilikuwa hazivuki 3 ila leo mpaka 20 tena waalimu kadhaa wanawapiga sio haki kabisa waitwe wazazi waambiwe matatizo yao
Mkuu hapa Ulaya kila baada ya mda kuna meeting ya wazazi, waalimu na wanafunzi
Tunaingia hall kubwa kuna vinywaji na bites kila mwanafunzi anaitwa anakaa na wazazi na kuambiwa maendeleo yake ya miezi kadhaa
Tunawajua waalimu wao na wao wanatujua personally
Hii inasaidia kujua maendeleo ya mtoto kila wakati hata akiwa mtoro utamjua haraka au kama ni mtundu unaambiwa
Ila sidhani Waalimu wa huko kama wanawajua wazazi wote wa wanafunzi wao wa darasa
Lakini kila nchi ina mambo yao