Wanafunzi wanauliwa na walimu kwa vipigo na wengine wanachora ramani za kutorokea USA; tazama huyu hapa anauliwa tena!

Wanafunzi wanauliwa na walimu kwa vipigo na wengine wanachora ramani za kutorokea USA; tazama huyu hapa anauliwa tena!

Ndomana nlipokuwa nasoma nlikuwa na historia ya kupiga walimu
Form 1 nliendaga sangu sec,
Kuna mahali pale shule wanapaita soweto ukilazwa pale
Kila mwalimu atakutandika..
Mm nlikuwa nawaambiaga tutakutanq uraiani
Kuna walimu pale mpk leo nawakumbuka majina wakina ndimbo,kasebele(alikuwa mfupi)
Mwakyulu wote hao nishawachapa sana nje

Ova
Umesoma Sangu?

Usikute hata msichoke umegonga gambe pale.

Mwakyulu alishafariki mwalimu wa kuvaa miwani.

Ww umesoma enzi za kina Kambasonic?

Nakaband au kina Jagwa? Manake hao ndio walikuwa wanapiga waalimu
 
Hapana mkuu, watukutu na watundu wapo sana hata kwa wanyama pia na wanafundishwa mpaka wanakaa sawa bila hata kupigwa
Kupigwa sio suluhu, hata Ulaya ni binadamu pia na wana watundu na hata wanyama wao kuna wabaya na wapole pia ila wana watu wa kuwafunza mpaka wanakaa sawa
Kwa sisi unaweza kumuona mtoto anachelewa kufika shule na jambo la kwanza mwalimu anamtandika fimbo za kutosha
Lakini hata siku moja hakai nae na kumuuliza kwanini anachelewa?

Labda nyumbani kuna ugomvi wa wazazi kila siku, labda baba mlevi akija hakuna kulala
Huenda ni yatima au anapigwa kila siku
Ila yote hayo hawajali
Hebu wewe fikikiria mtoto wa hivyo ana kosa gani
Kuhusu utumdu kuna wengi wana autism symptoms ila hamuelewi bali unapiga tu kumbe ni mgonjwa huyo

Umewahi kuwaza hilo mkuu au unaona ni mtukutu basi dawa ni fimbo tu mpaka afe?
Wengi waalimu na wazazi wanahitaji Elimu zaidi kuhusu haya

Kuna kipindi kinaitwa Dog whisperer na mwingine anaitwa Graeme Hull amesomea University of Hall hebu waangalie hao uone wanavyowabadili mbwa tabia zao
Ni mfano tu mkuu siwafananishi na watoto ila similarities zipo sana kwenye behaviors zao

Kuna pia unaweza kusoma kwanini watoto wanakuwa watukutu?
Shukuru Mungu wewe umepata watoto wapole wenye akili na usiombe ikutokee, Watu wanaombaga mpaka police mtoto akae sero, Mimi nimesoma mpwapwa Sekondari, kipindi Cha mwishoni miaka 90s walihamia wanafunzi wachache kutoka tambaza, kipindi hicho Tambaza ilifutwa sababu ya utukutu na watoto wote wakahamishiwa shule nyingine. Ndani ya miez miwili tu wakachoma nyumba ya mwalimu moto. Yan upate mtoto wa kiume mtundu utumie ushauri nasaha labda waache Kufundisha wadili na watukutu siku Nzima. Hao unaosema wanachelewa shule sababu za kifamilia wapo ni wachache sana na mtoto mwenye akili akiwa na shida hiyo anamuona mkuu na kujieleza.

Narudia mkuu, hujawahi kukutana na mtoto mtukutu wewe na usiombee. Hayo mambo ya kufananisha watoto wazungu na wakibongo lazma uangalie na utofauti mazingira.
 
Kilichoniuma zaidi kupiga watoto underage yaani mwalimu anapiga mtoto wa miaka 6 sijui 7 mpaka anaua
Anampiga mtoto mdogo ngumi ya tumboni pamoja na viboko sasa ni haki hiyo?
Tusiwape vichwa hawa waalimu
Kweli wapo watukutu sana na hao nimewaona mpaka wanafukuzwa na shule kabisa wale wanaitwa nunda yaani hasikii kitu ila Waalimu enzi zetu walikuwa ni wenye hekima pia
Mtoto anaadhibiwa sio kwa jazba na hasira za kibangi bangi hapana bali walikuwa wanawachapa na kuwapa adhabu
Lakini sasa imekuwa kila leo tunasikia mwalimu kamjeruhi mwanafunzi au kaua kabisa

Hebu niambie hata kama ulisoma zamani au miaka ya karibu je hakuna suluhu yoyote mpaka kuuwa kwa fimbo?
Naona adhabu ya fimbo ingefutwa maana sisi kama kuchapwa zilikuwa hazivuki 3 ila leo mpaka 20 tena waalimu kadhaa wanawapiga sio haki kabisa waitwe wazazi waambiwe matatizo yao

Mkuu hapa Ulaya kila baada ya mda kuna meeting ya wazazi, waalimu na wanafunzi
Tunaingia hall kubwa kuna vinywaji na bites kila mwanafunzi anaitwa anakaa na wazazi na kuambiwa maendeleo yake ya miezi kadhaa
Tunawajua waalimu wao na wao wanatujua personally
Hii inasaidia kujua maendeleo ya mtoto kila wakati hata akiwa mtoro utamjua haraka au kama ni mtundu unaambiwa
Ila sidhani Waalimu wa huko kama wanawajua wazazi wote wa wanafunzi wao wa darasa

Lakini kila nchi ina mambo yao
 
Kwa kesi ya mtoto wa miaka 7 kupigiwa Hadi kufa, kwasababu wahusika washakamatwa tuache police ifanye Kazi yake, tuje tuliongelee baada ya majibu kitoka

Hili la kumjua mtoto ni muhimu Sana, changamoto kubwa huku kwetu salary ya Mwl ni ndogo hivyo walimu wengi wanaiba muda wa mwajiri kufanya mambo mengine ya kumuingizia kipato hivyo wanakosa muda wa kuwa Karibu na mtoto na kumjua. Na Ndio maana fimbo inatumika Sana maana ni adhabu ya chap chap, adhabu nyingine zinahitaji usimamizi na zinakula Muda wa mwalimu.

Sasa hivi misaada ya ulaya imekuja na sharti la shule salama, wakilazimisha watoto wasichapwe, iboreshwe tu huruma ya ushauri nasaha na Mfumo mzuri wa kukusanya maoni ya wanafunzi . Changamoto kubwa ya kwanza hakuna mwalimu mwenye huo muda wa kukaa na mtoto kumshauri wakati anapaswa kuandaa kipindi, kufundisha na Kisha akatafute kipato kingine. Mwalimu unakuita inabid apande daladala kwenye Kazini,anywe Chai na kula chakula Cha mchana akiwa shuleni na maji ya kunywa hapo ni kama 10,000 Kila siku inatumika, hapo Familia haijala wala Kodi haijalipwa Sasa mshahara wa laki 5 Au sita hauwez kutosha lazma mtu ajiongeze. Huko Mbele ni tofauti
 
Daa aisee nimesikitika sana
Kama ni hivyo inabidi waalimu waongezewe mishahara kwa kweli ingawa hata kuchapa haumwongezei kitu mwalimu bali uadui tu
Huku mwalimu London mshahara unaanza na £30,000 mpaka 47,000 na ni wengi wanakidhi mahitaji yote ya wanafunzi mpaka special needs wanapewa one on one

Nimekuelewa mkuu Asante
 
Nmesikiliza tena. Inaonekana ni Tanzania maeneo ya kusini, kuzunguka ziwa Nyasa au Malawi. Hiyo english wanapenda sana kuitumia wanyasa. Kama nimesikia na maneno kidogo ya kiswahili. Neno ''mia moja'' ''mwache kwanza'' ni kama nimeyasikia.
Angalau sasa mwelekeo umepatikana. Dkt. Gwajima D tunakuomba uwasiliane na polisi wa Ruvuma wafuatilie hili jambo kwa ukaribu ili huyu binti anayeadhibiwa kinyama apate haki yake.
 
Inasikitisha sana. Tumekuwa tukisikia walimu wakihusika kuwaua wanafunzi kwa vipigo na baadhi yao wameishafungwa gerezani na kuhukumiwa kunyongwa hadi kufa lakini huku mtaani nako hali si shwari.

Tazama mabaladhuli haya yanavyomuadhibu huyu binti bila huruma huku watu wazima wakishuhudia na kucheka wakichukua video wakatupie mtandaoni. Nchi hii kweli imefikia ufedhuli wa kiasi hiki? Mbona kuna baadhi ya watu wapo uraiani lakini wanaishi kama vile wapo jehanamu?
View attachment 2938392
Haya majitu yanamuonea binti mdogo asiyekuwa na hatia kwa kumfunga kamba na kumuadhibu kwa kiasi hiki kama vile nchi hii haina utawala wa sheria? Naomba vyombo vya sheria vichukue hatua kuwashughulikia wapuuzi hawa. Yaani wanamchapa binti kiasi hiki hadi wanammaliza nguvu za kike? Na utashangaa akiolewa asipate watoto yatakuwa yanakesha kwa Mwamposa kumuombea apate watoto wakati yenyewe ndiyo yamempa adhabu kali hadi yameua mayai yanayozalisha watoto.

Halafu tazama hilo shabiki la Utopolo jinsi linavyomchapa utadhani linaua nyoka! Majitu ya Yanga yana roho mbaya zaidi ya shetami. Hizi zote ni hasira za kufungwa na Azam. Yaani kufungwa yafungwe kiwanjani halafu hasira yanaenda kumalizia kwa binti wa watu asiyekuwa na hatia?

Tafadhali sana Dkt. Gwajima D naomba uchukue hatua haya mashenzi yakamaatwe yatiwe adabu. Hayawezi kuifanya nchi hii kama shamba la wanyama lisilokuwa na utawala wa sheria. Mambo ya kishenzi kama haya hayakubaliki duniani wala mbinguni. Haya majitu yakikamatwa yaadhibiwe zaidi ya yalivyomuadhibu huyu binti asiyekuwa na hatia. Naomba wanaoifahamu lugha hii inayoongewa na hawa wanaizaya watusaidie kutambua ni lugha ya kabila gani ili kuisaidia polisi kufanya upelelezi na kuwatia nguvuni wahalifu hawa wasiokuwa na chembe ya huruma.
Ila hii video ni ya miaka mingi kidogo. Halafu pia lugha ni ya nchi fulani hivi.
 
Hiyo Lugha ni ya Kinailoti na hapa Tanzania tuna Kabila moja au mawili tu ya Kinailoti Jaluo ni mojawapo.
 
Hiyo Lugha ni ya Kinailoti na hapa Tanzania tuna Kabila moja au mawili tu ya Kinailoti Jaluo ni mojawapo.
Hicho si kijaluo hata kidogo, yaani hata matamshi hayaendani kabisa kabisa.
 
Back
Top Bottom