Wanafunzi wengi waliomaliza vyuo vikuu hawana reasoning and cognitive skills

Ukubali, ukatae, nyie vijana wa siku hz mna urlewa mdogo sana wa mambo
Huoni kama mleta uzi ndio kafanya segregation mapema mno ....Angechukua madaraja tofauti kabisa then anawapimahata kila daraja watano watano .


Ndio maana kuna interview ,wapo vijana wajanja sana ila mitihani wanambwelq kutwa .
 
Elimu ya kukariri ni shida sana, uje sasa kuonana nao kwenya mwendo kasi....ze ze zeee nyingi ila kichwani hawana lolote
 
Ukubali, ukatae, nyie vijana wa siku hz mna urlewa mdogo sana wa mambo
Uelewa na mambo unachangizwa na vitu vingi sana mkuu mosi ni juhudi ya mtu binafsi.

Tuambia hapa enyi wenye uelewa mkubwa mmeleta mageuzi gani kwenye Sayansi na teknolijia,siasa, uchumi pamoja kijamii
 
Mtu unamuuliza hii habari yaserikali imetoa fedha za kujanga madarasa kwa kutumia force account hii si monetary policy hihii?
Kujenga madarasa kwa kutumia force account sio monetary policy. Haihusiani na monetary policy hata kwa mbali.

Monetary Policy ni hatua za kuimarisha uchumi kwa kuthibiti kiasi cha pesa kinachoingia kwenye uchumi haswa kwa kurekebisha viwango vya riba na masharti ya viwango vya amana za mabenki.

Has nothing to do with whether serikali imenunua simenti na kuchimba matundu ya vyoo kwa kutumia wazabuni walioshindanishwa au kampuni teule ya swaiba wa waziri (force account).

Hukuwa na competency ya kuwa-assess na kuwa-judge hao vijana.
 
Mkuu umeongea jambo la maana, ila kumbuka kwamba kuna wenye akili( hiyo uliyoiita reason skill..hawa huwa hawana alama za juu darasani) halafu kuna wale wenye uwezo mkubwa wa kukariri lakini wana uwezo mdogo wa kufanya reasoning..hawa ndiyo vipanga na wanaonekana wenye akili sana.
Kundi hili ndilo ulilokuwa umeletewa kwenye huo usaili wako.
 
Top performers.....apa ndo mlipo zingua, nisawa na kuchagua mke kwa kuangalia take na sura
 

Umeongea kitu kikubwa, nilishawahi feli somo flani chuo kwa sababu tu sikucopy na kupaste vitini vya lecturer flani kwenye mtihani wake. Ila wale waliocopy na kupaste wanapata A clean,

Uzuri semester iliyofuata alikuwa na somo jingine, sikutaka kujipa tabu. Nilisoma notes zake hadi nukta bila kuongeza chochote, mwisho wa siku nikanyoosha banda 😁😁

Sasa hapo mtu awe serious kusoma madini ya nje ya nini, ndio chanzo cha watu kukosa analytical skills sababu wamelemazwa na copy pasting japo good lecturers bado wapo wengi tu
 
Huwezi kumtoa kijana chronic moja kwa moja ukampa ajira ukategemea atafanya vizuri. Ndio maana kuna internships. Ajifunze kazi kwa vitendo ndio aende kwenye ajira. Sisi ofisini kwetu kila mwaka wanaleta trainee kutoka kwao wanakaa miezi sita kujifunza kazi ndio wanaenda kutafuta kazi kwingine. Waajiri pia wanatakiwa kuwekeza kwenye professional training ili kuwapa ujuzi wa kazi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…