Robert Heriel Mtibeli
Platinum Member
- Mar 24, 2018
- 40,153
- 93,069
Hamjambo!
Napenda wapigania haki. Hilo litabaki hivyo. Lakini nachukia ushabiki maandazi. Yaani uanaharakati wa kishabiki.
Siupendi kwa sababu unaulaghai na uongo mwingi sana. Na mtu mwongo kwa kweli hanivutii.
Ukiwa muongo uwe muongo mwenye Akili angalau.
Hawa wanaharakati uchwara hawana tofauti na machawa wa kiccm. Kina Lucas Mwashambwa na Tlaatlaah na magenge yao wote nawaona wapo sawa.
Mgomo wa madereva wa mabasi hauhusiani hata kidogo na mambo ya kisiasa. Lakini kuna wanaharakati uchwara wanahusisha siasa.
Maandamano ya hapo Mbeya hayapo kisiasa hata kidogo. Lakini kuna wanaharakati wanayahusisha na siasa. Ni tabia za ajabu na hovyo.
Hakuna tofauti yoyote na wale machawa ambao kila kitu kikifanikiwa hata kama hakihusiani na Siasa. Watamuingiza Rais Samia hapo kwamba ndio kafanya.
Kwa kweli sijajua kama ndio siasa zilivyo. Hilo sijajua. Na kama siasa ndio ziko hivyo basi mimi ni miongoni mwa watu ambao hatutaziweza.
Kujifyatua Akili mbele za watu na kuongopa waziwazi ni kipaji cha ajabu na hovyo sana.
Haya kuna wanaohamasisha watu kuandamana wiki ijayo October 29 mwaka huu kama sehemu ya kumbukumbu ya kilichotokea mwaka jana.
Sio tatizo. Tatizo ni pale unatumia uongo na matukio ya kilaghai ili kuipa nguvu na kuhamasisha watu katika siku hiyo.
Sipendi uhamasishaji wa kitapeli. Shawishi kiuadilifu.
Sema jamani watu tutoke siku fulani. Kuna moja, mbili, tatu. Hamasisha watu kwa kutumia Ukweli na Haki. Usidanganye.
Ule uongo wa kusema jeshi lipo upande wa wananchi mwaka jana uligharimu sana watu wengi. Uongo unaletaga majanga na Majuto.
Uongo unaleta mkumbo na watu kukurupuka.
Ukweli unaleta maamuzi ya kweli bila Maputo.
Tunapozungumzia uadilifu tunazungumzia haki, ukweli, wajibu na uwajibikaji.
Unapodanganya watu kuwapa moyo kiuongouongo huo ni uhuni. Hiyo ni dhulma.
Mfano unasema Fulani amekufa, au kapata stroke. Unaaminisha watu hivyo.
Ni bora hiyo taarifa iwe ya kweli.
Itawafurahisha wanaomchukia.
Lakini kudanganya unawaumiza mara mbili. Uongo unaumiza sana.
Wanaharakati uchwara muache kudhulumu hisia za watu wenu. Mnawafanyia uhuni we zenu.
Mnasema wanaonewa. Ni kweli wanaonewa lakini nanyi mnakuja kuwaonea zaidi.
Watu waambiwe Ukweli.
Kama huna taarifa ya uhakika na yakweli. Acha kuitoa. Acha utapeli. Acha uhuni.
Ukombozi hauletwi na watu matapeli, wahuni na waongo waongo. Hakunaga ukombozi wa namna hiyo. Watu waambiwe Ukweli.
Mtibeli napenda watu wakweli kwa sababu hao ndio watabadilisha sio tuu familia zao bali hata taifa lao.
Mimi bado nipo. Natazama.
TaikonMaster
Kwa sasa Dar es salaam