A) Ku speak out kwenye masuala ya udhalilishaji wa Kingono wengi huchelewa sababu ya kuumizwa sana hadi kushindwa kuliongelea, kuumizwa kiakili hivyo anakua anapata matibabu kutoka kwa wataalam wa Afya ya Akili, Kuona Aibu kuliongelea hilo suala... Kiufupi wengi hua kimya hata kwa Miaka 30 au anakufa nalo.
B) Alivyoona Tangazo la Royal Tour akaona aspeak up ili kuwatahadharisha wengine hasa Wakina Dada ambao wana safiri peke yao,
C) Hayo hua ni Maneno ya Mtu mwenye Hasira baada ya kufanyiwa jambo fulani basi hujumuisha vitu vingi na watu wengi bila kujali kwenye Wabaya na Wema wapo,
D) Hasira zake, hasa ukizingatia alitaka kufanyiwa kitendo hicho na Mwanaume na bado Wanaume hawakumpa ushirikiano wa Kisheria,
E) Kupata msaada wa kiSheria ukiwa ugenini sio jambo dogo, hapo ingebidi aishi hapo hapo ili kufatilia kesi yake je alikua amejipanga kwa gharama hizo?? lakini kuna ushahidi mwingi unao oenesha huyo dada alitaka kweli kufanyiwa jambo hilo lakini hakuna ushahidi unaoonesha huyo dada akiomba apatiwe kiasi hicho cha pesa ili kesi iishe, bado hatujui zaidi,
F) Ni Wapinzani wetu kwenye Soko la Utalii, hiyo ishu ingetokea Kenya hata sisi WaTz tungeungana na wengine kuwashambulia Kenyans,
G)Ni asilimia Moja pekee
H)Haita athirika kwa chochote zaidi itapata ahueni, kesi za madawa na Utapeli kwa Watalii wetu halisi zitapungua, kumbuka hiyo asilimia chache ya Nigerians wanaoenda Znz sio kwa Utalii bali kwa biashara za drugs, ukahaba na utapeli kwa Wazungu.