Wanajeshi wa Tanzania takribani 2000 walifyekwa na majeshi ya Idd Amin; huo ndio ulikuwa mwanzo wa vita ya Kagera

Unajua maana ya askari 2000 hicho ni kikosi ama vikosi viwili. Tony Avirgan ameandika katika War in Uganda kuwa tulipoteza askari wengi sana mwanzoni mwa mapigano, lakini hakuna takwimu ya wanajeshi 2000 kufariki pale Lukaya. Msiendekeze sana BBC.
 
Nivyema kuwa makini sana tunalosikiliza taarifa za habari za vyombo vya magharibi, kunambinu kali sana za kuweza kudemoralize kundi la watu fulani wanalolitarget kwa manufaa yao fulani, na mipango yao huwa ni endelevu, ni kweli katika vita vifo havikwepeki, lakini kila unalolisikia changanya na zakwako au fanya tafiti
 
Askari 2000? Yaani askari wote walioko Arusha na Tanga jumlisha na walioko Dar na Pwani. Hizo ndio Battalion mbili. Hakuna Jeshi litasimama ukitokea msiba mzito namna hiyo. Hapo ina maana kila kitu kilinyang'anywa na majeshi ya Amini na tayari waliukalia mji wa Bukoba, Arusha na Dar. Kweli za kuambiwa changanya na zako.
 
Yeah...you are right man
 
Vita ni hatari ukienda kwa wazee wa Bukoba watakwambia jinsi damu ilivyonuka. babu yangu alienda ila hasimulii hadi alewe anakwambia Mganda alikuwa na ENEMY ALARMING MACHINE/WATCH yaani kila askari wa Uganda alikuwa na hiyo saa akiwa karibu na adui tu inatoa alarm. Yeye ikawa kajificha na alarm inapiga ila hawamuoni ile wanageuka tu kurudi aisee alichofanya huyu babu hatari hata kusimulia ila sikia tu kwa wenzio vita noma.
 
Mkuu hata mimi uwa napata ukakasi kuamini aliyosema mwalimu kwamba "tumepoteza vijana 395 na raia wasiopungua 1500" kwa nature ya ile vita watu wengi na askari walipotea, ukiangalia strength ya tanzania kulikuwa na askari "troops" wasiopungua 150'000~250'000, (hapa chukua na UNLA ya Mseveni plus wale askari kutoka Mozambique, China na Cuba) wakt waganda awakuwa na zaidi ya askari 70'000 ukijumlisha na Libya zaidi ya 500, na bado vita ilipiganwa zaidi ya miezi 10 mpk ushindi kupatika


Hapa nahisi yafuatayo......

1. Uenda idadi hii 395 ni idadi ya askari waliokufa vitani na sio idadi ya wale mgambo,JKT,UNLA,polisi na washirika kwani mwanzon zile platoons zaidi ya 10 zilizotaka kuvuka mto kupitia mitumbwi zilimiminiwa mizinga na kupotea kabisa kiasi cha kamanda wake kuondolewa mstari wa mbele na daraja kuvunjwa rasmi

2. Hii vita ilkuwa ngumu kweli kweli kutoka na kupiganwa kipindi cha masika na ile misitu minene na mapoli ya Uganda kiasi cha kupoteza askari wengi sana

3. Vita hii wakati mwingine ulihitajika uzalendo kwan kizana waganda walikuwa mbali kivifaa kuna wakati vita ilichachamaa esp katika utekaji wa mbalala na entebbe kiasi cha askari frontline ku retreat bila mpangilio wengin walkimbia mpk bukoba mjini mpk kupelekea msuguri kuonelea askari wote wavuke daraja kisha livunjwe ili wasipate pa kupitia na kazi ya kujijenga upya kuchukua wiki tatu

5. Uenda kuna stori inafichwa makusudi na kwa mtu ambaye ana ubongo ili ni muhimu zaidi na ufanywa makusudi
 
We jamaa utakua sio mtz unadhalilidha jeshi elfu 2000 watu mchanga? Jwtz unalijua au unaropoka tu nonsense!
Watu 2000 wana wa nchi waliuawa kikatili na jeshi la Uganda kwa msaada wa Gaddafi.

Halafu leo watu wanamsifia Gaddafi eti mzalendo, kiongozi bora wa Africa.

Inatia kichefuchefu.

Hamna mtu asiyefanya makosa na hivyo hata Gadaffi alikuwa na makosa yake. katika kumtathmini kiongozi lazma ulinganishe mazuri na mabaya yake na kwa kuzingatia hilo hamna kiongozi kama Gadaffi barani Afrika na itachukua muda mrefu kupata kiongozi kama Gadaffi. he's the true African hero
 
Nadhani data au takwimu halisi za wanajeshi waliopteza maisha wakati wa vita ya Kagera ipo pale Ngome....na haitusaidii sana kwa sasa zaidi ya kuadhimisha siku ya mashujaa na kuangalia familia zao.

Kama hupendi historia basi usilaumu wanaoipindisha. Ni wajibu wako kutnza historia walau kuandika tukio moja kwa siku kwenye diary yako.
 
Unajua maana ya askari 2000 hicho ni kikosi ama vikosi viwili. Tony Avirgan ameandika katika War in Uganda kuwa tulipoteza askari wengi sana mwanzoni mwa mapigano, lakini hakuna takwimu ya wanajeshi 2000 kufariki pale Lukaya. Msiendekeze sana BBC.

Idadi ya askari waliouawa hwezi kuambiwa milele. Tony asingeweza kupewa idadi ile na siyo mtu wa kupewa.
 
Idadi ya askari waliouawa hwezi kuambiwa milele. Tony asingeweza kupewa idadi ile na siyo mtu wa kupewa.
Mwaka juzi Al Shabab waliua askari zaidi ya 200 wa KDF kwa ambush ambayo haikuzidi one hour. Hadi leo Kenya hawajathubutu kuwatangazia wananchi rasmi hii idadi.
 
Respond the matters with the facts na sio porojo. Ukweli wa vita hii waulizie watu wa Kagera, especially Wilaya ya Missenyi ndo watawapa ukweli wa vita hii. sio kwamba kila kitu kilikuwa disclosed na ushindi haukuja da way wanavyouongelea.
 
Hawakuwa wanajeshi waliopata mafunzo,waliopelekwa kwanza,walikuwa wanamgambo na wananchi waliopewa crush program ya mapambano,kwa muda mfupi,ndio wakapelekwa mstari wa mbele,ungekuwa msomaji mzuri wa historia,hili jambo limeelezwa vzr kwenye filamu ya vita ya Kagera,mpaka majarida mbalimbali yanayopatikana hata kwenye maktaba ya Taifa,mimi nalifahamu hili tangu mwaka 1996,
Usishinde kwenye whatsaap tu,kasome vitabu,
 
Hawakuwa wanajeshi waliopata mafunzo,waliopelekwa kwanza,walikuwa wanamgambo na wananchi waliopewa crush program ya mapambano,kwa muda mfupi,ndio wakapelekwa mstari wa mbele,ungekuwa msomaji mzuri wa historia,hili jambo limeelezwa vzr kwenye filamu ya vita ya Kagera,mpaka majarida mbalimbali yanayopatikana hata kwenye maktaba ya Taifa,mimi nalifahamu hili tangu mwaka 1996,
Usishinde kwenye whatsaap tu,kasome vitabu,
 
Ila what is true ni kwamba tulifyekwa in that first round. Kwa nini just tusiseme tu ukweli?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…