Miss Zomboko
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 4,599
- 9,532
Wanajeshi wa Urusi wamesonga ndani zaidi katika mji wa Mariupol ulioathirika zaidi na vita vinavyoendelea nchini Ukraine ambapo inaarifiwa kuwa mapigano makali yamepelekea kufungwa kwa kampuni moja kuu ya chuma cha pua huku serikali ya eneo hilo ikitoa wito wa msaada zaidi kutoka mataifa ya Magharibi.
Mkanda wa vidio uliokuwa na ujumbe kwa viongozi wa nchi za Magharibi uliothibitishwa na shirika la habari la Associated Press, umemuonyesha wa afisa mmoja wa polisi wa Mariupol akisema kwamba watoto na wazee wanafariki kutokana na mashambulizi ya Urusi katika mji huo.
Kutekwa kwa mji wa Mariupol itakuwa ni hatua kubwa ambayo imepigwa na wanajeshi wa Urusi katika vita hivyo, ukizingatia kwamba wamekuwa na wakati mgumu kupenya katika miji mikuu, wiki tatu baada ya kuanza uvamizi huo.
Gazeti la New York Times limemnukuu mwanajeshi mmoja wa Ukraine akisema shambulizi la roketi limesababisha vifo vya hadi wanamaji 40 katika mji wa kusini wa Mykolaiv hapo jana.