KERO Wananchi Halmashauri ya Biharamulo tunalazimishwa kufanya usafi huku tukilipa fedha za usafi kila mwezi

KERO Wananchi Halmashauri ya Biharamulo tunalazimishwa kufanya usafi huku tukilipa fedha za usafi kila mwezi

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Halmashauri ya Wilaya ya Biharamulo imekuwa ikitoza ada ya usafi kwa kila kaya, ofisi na wafanyabiashara. Wananchi wamekuwa wakilipa fedha hizo kwa matarajio kwamba zitatumika kuboresha usafi wa mazingira katika maeneo mbalimbali ya umma, ikiwemo kusafisha mifereji ya maji na maeneo mengine yanayohitaji matengenezo.

Hata hivyo, kwa mshangao wa wananchi, hivi sasa Halmashauri imekuwa ikiwataka wananchi wenyewe kufanya usafi kwenye mifereji ya maji iliyopo kandokando ya barabara, licha ya maeneo hayo kuwa sehemu ya miundombinu ya umma.

Wananchi wanahoji kuwa, ikiwa Halmashauri inakusanya tozo maalum kwa ajili ya usafi wa mazingira, fedha hizo zinatumika kwa kazi gani ikiwa usafi wa maeneo ya umma bado unaachiwa wananchi kufanya kwa nguvu zao wenyewe?

Tunaomba Halmashauri ya Wilaya ya Biharamulo kutoa ufafanuzi kuhusu matumizi ya fedha zinazokusanywa kupitia tozo za usafi na kuhakikisha kuwa jukumu la kusimamia usafi wa maeneo ya umma linafanyika ipasavyo.

Wananchi wako tayari kushirikiana katika masuala ya usafi wa mazingira, lakini ni muhimu kuwepo kwa uwazi na uwajibikaji katika matumizi ya fedha zinazokusanywa kwa ajili ya huduma hizo.
 
Back
Top Bottom