Swali ni nani afanye huo uhamasishaji?
CHADEMA wanapo itisha maandamano kwa sababu halali kabisa wananchi wanashindwa kujitokeza kwa wingi kuunga mkono maandamano hayo.
Hapa tunaweza tusiwalaumu wananchi, kwa sababu ya vitisho vingi vinavyo fanywa na polisi.
Sasa wakati huu wa kujiandisha kuwa wapiga kura, ingetegemewa kwamba CHADEMA na asasi mbalimbali wangefanya juhudi kubwa kuwa elewesha wananchi kwamba hii ndiyo nafasi yao nzuri ya kutumia haki yao na uhuru wao kwa kupiga kura na kuwapata viongozi wanao taka wawaongoze.
Hata kama CCM wakipanga kufanya mizengwe katika uchaguzi; polisi hawataweza kuwaelekezea wananchi mitutu ya bunduki wakati wakienda kupiga kura kwa wingi wao.
Kwa nini fursa hii wananchi hawaambiwi kuwa ipo na wanaweza kuitumia?
Bila shaka mkuu 'Proved' utakuwa umenielewa ni nani hasa wa kulaumiwa.
Kusema kweli inanishangaza sana kwa nini mambo yana kwenda hivi sasa hivi kama yalivyo. Nilitegemea hivi vyama vya upinzani vingekuwa kwenye kazi kubwa sana wakati huu; lakini ni kinyume kabisa, CCM ndio wanao onekana kufanya wanayo taka yafanyike. Ni ajabu sana.