LGE2024 Wananchi hawajajitokeza kujiandikisha ktk daftari

LGE2024 Wananchi hawajajitokeza kujiandikisha ktk daftari

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024
Watanzania sio wajinga kiasi hicho hata uchaguzi mkuu watu hawatokua wengi, na hii yote ni kuvurugwa kwa chaguzi baadhi wazi wazi , hayo ndio matokeo na hali hiyo haitobadilika karibuni , watu wameona waendelee na shughuli zao kuliko kufanywa wajinga miaka yote, hata Mimi binafsi siwezi kwenda kupoteza muda wangu wakati najua hua Kura zinaibiwa , yaani nilianza kuchagua 85 hadi Leo niendelee kua mjinga haipo hiyo
 
Kawaida ya siku za mwanzomwanzo watu wana mazoea ya kutegea na mwishoni mwa zoezi tegemea msululu wa watu .
Labda ije threat...
Otherwise don't expect the difference..
 
Haya maneno yako ni mazuri sana hapa.
Natamani wananchi hao hao wasiishie kwenye kususia kujiandikisha kupiga kura. Wakiishia kufanya hivyo maana yake CCM tunayo tena miaka mitano zaidi na pengine zaidi ya hapo.

Kama ujinga umewaondoka wananchi; tutegemee hatua ya ziada itakayo fuata baada ya kukataa kujiandikisha. Hiyo hatua iwe ni ya kuikataa kweli kweli CCM; hata ikitumia mabavu kubaki madarakani, wakatae.
Ikitokea hivyo, hapo nami nitaelewa kuwa wananchi wametoka kwenye ujinga.
Wakiikataa CCM then chama mbadala kiwe kipi?
 
Kwani mwisho ni lini ? Sisi huwa tunasubiria mpaka zile dakika za majeruhi ndio tukafanye mambo
 
Upinzani walitaka kuwe na katiba mpya au angalau Tume huru ya uchaguzi kabla ya huo uchaguzi ili yale madhila ya 2020 yasijirudie, ila wamepigwa pini makusudi.
Kama mambo yote ni yale yale ya 2020 kutakuwa na jipya?
Utaniwia radhi sana mkuu 'antimatter', kwani kamwe sikubaliani kabisa na dhana hii.

Hakuna jambo ambalo wananchi wanaweza kushindwa kulifanya iwapo wana uewlewa wa wanacho kifanya.

Hayo yaliyo tokea 2020; na kama ndiyo hayo wanayo panga sasa hivi CCM kuyafanya, ni kwa sababu wananchi hawaja ongozwa na kupewa ufahamu mzuri wa mambo hayo yanayowanyima haki zao za kuwachagua viongozi wanao wataka wao.

Haihitaji Katiba mpya wala nini kwa wananchi kuzuia ukorofi wowote ule unao pangwa na CCM.
CCM sasa hivi wanajisikia vizuri sana kwamba wananchi hawakupewa mwamko wa kuyakataa yaliyo tokea 2020
 
Watanzania sio wajinga kiasi hicho hata uchaguzi mkuu watu hawatokua wengi, na hii yote ni kuvurugwa kwa chaguzi baadhi wazi wazi , hayo ndio matokeo na hali hiyo haitobadilika karibuni , watu wameona waendelee na shughuli zao kuliko kufanywa wajinga miaka yote, hata Mimi binafsi siwezi kwenda kupoteza muda wangu wakati najua hua Kura zinaibiwa , yaani nilianza kuchagua 85 hadi Leo niendelee kua mjinga haipo hiyo
Kwa hiyo mmeamua kususa?

 
Swali ni nani afanye huo uhamasishaji?

CHADEMA wanapo itisha maandamano kwa sababu halali kabisa wananchi wanashindwa kujitokeza kwa wingi kuunga mkono maandamano hayo.
Hapa tunaweza tusiwalaumu wananchi, kwa sababu ya vitisho vingi vinavyo fanywa na polisi.

Sasa wakati huu wa kujiandisha kuwa wapiga kura, ingetegemewa kwamba CHADEMA na asasi mbalimbali wangefanya juhudi kubwa kuwa elewesha wananchi kwamba hii ndiyo nafasi yao nzuri ya kutumia haki yao na uhuru wao kwa kupiga kura na kuwapata viongozi wanao taka wawaongoze.
Hata kama CCM wakipanga kufanya mizengwe katika uchaguzi; polisi hawataweza kuwaelekezea wananchi mitutu ya bunduki wakati wakienda kupiga kura kwa wingi wao.

Kwa nini fursa hii wananchi hawaambiwi kuwa ipo na wanaweza kuitumia?
Bila shaka mkuu 'Proved' utakuwa umenielewa ni nani hasa wa kulaumiwa.

Kusema kweli inanishangaza sana kwa nini mambo yana kwenda hivi sasa hivi kama yalivyo. Nilitegemea hivi vyama vya upinzani vingekuwa kwenye kazi kubwa sana wakati huu; lakini ni kinyume kabisa, CCM ndio wanao onekana kufanya wanayo taka yafanyike. Ni ajabu sana.
Hv kabisa mtu unaweza kwenda kupanga folen kupiga kura wakati najua kiongozi wangu akishapitishwa na chama keshashinda tayari kura wakapge chadema na Act
 
Wakiikataa CCM then chama mbadala kiwe kipi?
Mkuu siamini kabisa kuwa unaniuliza swali hili na kutaka kweli nilijibu.
Kwani hiyo CCM kama chama sasa hivi ina kitu gani cha ziada zaidi ya hao wengine unaoona wewe hawawezi kuwa mbadala!

Labda nijaribu kukupa jibu kwa swali lako hili kwa njia nyingine inayoweza kuwa rahisi kwako kuelewa.

Sasa hivi, hata kile chama cha "ubwabwa" cha Mzee Rungwe ni bora zaidi kuliko CCM. Hapana, usidharau ninayo kueleza. Ni hivi: chama cha mzee Rungwe kikiingia madarakani sisi wananchi tutaweza kupata fursa ya kukiondoa kama tutaona hakifai. CCM, badala yake, wao ndio wametuweka mateka, na kutufanyia kila aina ya uchafu. Hatuwezi kuwaondoa kwa njia za amani. Kinacho subiriwa tu sasa ni mpaka hapo tutakapo kuwa na ujasiri wa kuwaondoa kwa nguvu, na kumwaga damu za waTanzania.
Sasa nikuulize wewe, huu ndio unafuu wa CCM ambao unaona hakuna chama kingine kinachoweza kuwa mbadala wake?
Ninahisi kuwa umeniuliza hili swali kwa vile wewe ni mnufaika wa CCM kwa njia moja au nyingine. Ninakuomba, unapo nijibu tena, kama utafanya hivyo, jitahidi kuweka mapenzi yako kwa chama chako; jitahidi kuelekeza mapenzi hayo kwa nchi yetu Tanzania.
 
Hv kabisa mtu unaweza kwenda kupanga folen kupiga kura wakati najua kiongozi wangu akishapitishwa na chama keshashinda tayari kura wakapge chadema na Act
Jibu rahisi sana ni HAPANA.

Lakini ninakuomba unisome na kunielewa ninacho zungumzia hapa.
Kupiga kura kwa wingi sana kuwakataa CCM siyo mwisho wa zoezi; pamoja na kwamba wingi wa kura zilizo wakataa ni kizingiti muhimu kinachoweza kuwazuia hata wasithubutu kutangaza mtu ambaye hakushinda

Wingi wa kura hizo zilizo wakata ndiyo ushahidi mzuri wa kuwalazimisha, hata kwa nguvu kuachia madaraka. Lakini unapo susia hata kupiga kura, moja kwa moja umekwisha kubali CCM waendelee kuwepo madarakani bila ya kutokwa jasho.
Hili ni tatizo kubwa sana litakalo endelea kutuumiza chini ya CCM.

Lakini kutokana na jinsi ulivyo andika hapa, ni dhahiri wewe ni mnufaika wa huko kususia kupiga kura. Hapa unafanya gheresha tu!
 
Yaani serikali inayoundwa na chama tawala ndio inasimamia uchaguzi, kuna uchaguzi hapo !!! nawaza tu
 
ujinga una mwisho wake, yaani leo mtengeneza jukwaa la kukaa na kupigia kura, wasimamizi na waendesha zoezi zima la kujiandikisha na kupiga kura linasimamiwa na viongozi wa chini wa chama cha mapinduzi, watendaji wa mitaa na kata, waalimu..wamepeana ajira za ulaji.
Pili, kwanini zoezi la kuhakiki lisingeunganishwa na hili la kujiandikisha kupiga kura?, yaani leo uniite mwananchi kujiandikisha alafu kesho uniite tena nije nihakiki taarifa..stupid!!..maisha yalivyo magumu hivi tunapambana tupate chochote tuishi ...nije unipotezee muda wangu wewe...sababu ya ujinga wako. Yaani serikali na tume ya uchaguzi hawana akili kiasi hicho kwamba wananchi hawana uvumilivu kupotezewa muda na mafisadi waliogawa zoezi moja lionekane ni mazoezi mawili tofauti!!?..tusichoshane..kama wanataka waendelee tu kuiba kura kama wanavyoibaga siku zote "Nape". Wasomi wengi hawana ajira na hata wakiomba za muda mfupi hawapati, so hawawezi kubali kupotezewa muda na wahuni
 
Watu hatuna imani na wasimamizi wa uchaguzi, tumeamua kuwaachia ccm waendelee wenyewe na wizi wao wa kishamba
Mkuu, 'Gulwa', huu siyo "wizi wa kishamba". Imepangwa maksudi iwe hivyo; na nyinyi mnao susa ndio mtaji mkubwa kwao.
 
Umuhimu wa vyama kuwa na ofisi ni wakati kama huu. Chama kisicho na ofisi hakiwezi kufanya kazi nje ya maandamano na mikutano ya hadhara . Sasa ni kuwaorganize watu waende kujiandikisha kwa makundi makundi kama maandamano kila sehemu lakini hakuna sehemu ya kuratibu mambo ya vyama. Taasisi za dini ziokoe Jahazi hasa Kanisa katoliki na Waislam nje ya Bakwata.

Lakini pia kuna upumbavu fulani unafanywa na Chadema na ACT kujiona kila kimoja kuwa kinaweza kuitoa CCM madarakani bila kushirikiana . Ni ndoto ya aliacha CCM kutolewa madarakani na Chadema peke yake au ACT peke yake .

Ili siasa za kuitoa CCM zibalance ni lazima ACT ilingane na Chadema katika kuachiana mitaa najilbo lakini huu ujinga wa kulia lia kwenye mitandao eti CCM wanahujumu wakati hakuna mikakati ya kuingia kwenye uchaguzi .
Hivi Chadema itapataje kura za kutosha kwenye ngome za CUF(ACT ) Au ACT kwenye ngome za Chadema.
CCM ni vyama vingi ndani ya Chama kimoja lakini linapokuja suala la UCHAGUZI WANAWEKA TOFAUTI ZAO PEMBENI lakini wapinzani wanabaki na chuki kubwa na kuitana wasaliti mara CCM B mara vyama vya mfukoni na kukebehiana bila kujua adui wao ni CCM tu na kuitoa ni lazima kushika ngome za pwani kuanzia Zanzibar(ACT) na bara (Chadema)

Ni ingekua kwenye hivi vyama Wanaovuruga uchaguzi wangenyooka na familia zao asubuhi na mapema siku ya pili baada ya uchaguzi.

Nilisahauri sana Chadema kuwa waachane na maandamano kama walikua hawana mbinu ya kuyafanya zaidi ya kusubiri huruma ya CCm na polisi jambo ambalo halipo
 
Ukiskia watu wamechafukwa mtaani huwezi amini

Leo jilani yangu ananiambia wakitaka nika vote wanipe hela ya kupotezea mda nimeshindwa kumwelewa alikuwa Ana maana gani

Nimejikuta na mwitikia tu eti eeeh?? Akqni jibu hivohivo.,

kikauzu Kama tuna ugomvi


Sasa kama viongozi wa vyama ndio wanaolia lia eti kuna hujuma akati hata kujiandikisha hawajajiandisha basi ni dhahiri kuwa CCM itaendelea kutawala na upinzani útkuavdhaifu
 
Back
Top Bottom