LGE2024 Wananchi hawajajitokeza kujiandikisha ktk daftari

LGE2024 Wananchi hawajajitokeza kujiandikisha ktk daftari

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024
Walimu wanatia huruma katika hivyo vituo.
Serikali ijitafakari.

Mwisho.
IMG-20241012-WA0000.jpg
 
Kawaida ya siku za mwanzomwanzo watu wana mazoea ya kutegea na mwishoni mwa zoezi tegemea msululu wa watu .
Siyo kweli. Jana wakati kunapita tangazo, nikawasikia watu wanasonya na kusema eti nchi hii uchaguzi hauna maana. Gari la matangazo likawa limeamsha mjadala mrefu, wakaanza kuongelea bandari, viongozi kuwekewa kinga ya kutoshtakiwa, deni la Taifa, Zanzibar inavyopendelewa, walimu walivyochangishwa hela kwa nguvu kwaajili ya kuipa CCM. Watu wenyewe kwa kuwatizama, huwezi kufikiria wanayajua hayo yote!! Kumbe kwenye kundi, mmoja ana ndugu yake ni mwalimu. Akaeleza jinsi mkurugenzi wa halmashauri ivyowalazimisha watumishi wote wa halmashauri kuwa wanatakiwa kuwa na kadi za CCM, na kuwa ni lazima waichangie CCM maana ndiyo iliyowaajiri. Huyo ndugu yake alipokosa kuchangia, aliitwa na kuonywa, na kulazimishwa kuchangia laki 1.
 
CCM tunajiandikisha kama kawa, kwa raha zetu,

Wasiyojiandikisha ndiyo atakuja kuwa wa kwanza kulalamika kudhulumiwa kura.

Kondoo wanajulikana.
Ccm hamtegemei kura. Hakuna atakayekuja kulalamika kuibiwa kura wakati tumeshapuuza huo ujinga uitwao uchaguzi. Watakaolalamika ni wale watakaoendelea kushiriki huo ushenzi.
 
Mjinga tu ndio hupanga mstari ili kutoa, wajinga wanapanga stari kutoa sadaka, kupiga kura nk.

Ila haya ni mambo mpokeaji alipaswa akufate Ghetto tena kinyumenyume.

Sikia, Juz tupo kwa Graduu mgeni rasmi akakata Cake kwa niaba ya CCM na akasema Mi5 tena, Watu wote Aaaaaah... Naoma akaingiwa hofu akavunga kama si yeye🤣
 
Nani apoteze muda wa kupiga kura wakati CCM wana majina ya washindi wao mfukoni?

Lissu amewahi kusema kuwa kushiriki uchaguzi kwa sheria hizi ni Ujinga

Ni mpaka hatua madhubuti za kuufanya uchaguzi uwe huru na haki ndo watu watauchukulia serious, otherwise wacha CCM waendelee kujidanganya kwa chaguzi feki mpaka siku watakapokutana na violent revolution
 
Mkuu, 'Gulwa', huu siyo "wizi wa kishamba". Imepangwa maksudi iwe hivyo; na nyinyi mnao susa ndio mtaji mkubwa kwao.
Wizi wa kijanja hufanyika bila kujulikana, wa kishamba hata wajinga wanauona
 
Jibu rahisi sana ni HAPANA.

Lakini ninakuomba unisome na kunielewa ninacho zungumzia hapa.
Kupiga kura kwa wingi sana kuwakataa CCM siyo mwisho wa zoezi; pamoja na kwamba wingi wa kura zilizo wakataa ni kizingiti muhimu kinachoweza kuwazuia hata wasithubutu kutangaza mtu ambaye hakushinda

Wingi wa kura hizo zilizo wakata ndiyo ushahidi mzuri wa kuwalazimisha, hata kwa nguvu kuachia madaraka. Lakini unapo susia hata kupiga kura, moja kwa moja umekwisha kubali CCM waendelee kuwepo madarakani bila ya kutokwa jasho.
Hili ni tatizo kubwa sana litakalo endelea kutuumiza chini ya CCM.

Lakini kutokana na jinsi ulivyo andika hapa, ni dhahiri wewe ni mnufaika wa huko kususia kupiga kura. Hapa unafanya gheresha tu!
Mkuu nashukuru elim uliyonipa natumai pia nawengne wataielewa ila kusudio langu lilikua kuonyesha wanaoenda kujiandikisha niwalio na uhakika wa ushindi kwan wengi tumekatishwa tamaa kujiandikisha alafu kupga kura natukashinda na tusitangazwe washindi ccm hawajawah kuwa na aibu nikwambie kabisaa kunakitua wapga kura walikua 320 upinzan wakapata kura 180 ccm kura 220 ukizijumlisha nathan kura znafka 400 hzo mia nakitu zmetoka wap na mtendaj akatangaza matokeo ni halal
 
NYIE KAJIANDIKISHENI...
Mnalazimisha wote tujiandikishe ili mwisho wa siku muibe Kula nyingi 😂😅 hizo hizo chache za watu wenu zinawatosha mtazi duplicate machine si mnazo... Kama washindi wanajulikana yanini kujichosha?
 
Wanachama wa ccm wanajua wapige kura ama wasipige watashinda, wanachama wa upinzani wanajua hata wakipiga kura kuwachagua viongozi wao wa upinzani hawawezi kutangazwa kushinda. Sasa nani ataenda kupiga kura? Yani kwa nini ukapige kura wakati matokeo unayajua yatakuaje... Ni kupoteza muda tu
 
Mkuu nashukuru elim uliyonipa natumai pia nawengne wataielewa ila kusudio langu lilikua kuonyesha wanaoenda kujiandikisha niwalio na uhakika wa ushindi kwan wengi tumekatishwa tamaa kujiandikisha alafu kupga kura natukashinda na tusitangazwe washindi ccm hawajawah kuwa na aibu nikwambie kabisaa kunakitua wapga kura walikua 320 upinzan wakapata kura 180 ccm kura 220 ukizijumlisha nathan kura znafka 400 hzo mia nakitu zmetoka wap na mtendaj akatangaza matokeo ni halal
Sasa kwa wananchi ambao wame elimika vizuri na hawataki HAKI zao zivurugwe; hapo kwenye kituo hicho ulicho tolea mfano uchaguzi huo na matokeo yake yasinge kubalika, kwa sababu wananchi wenyewe wasinge ruhusu. CCM inatumia mwanya huo wa wananchi kutojua HAKI zao ni zipi, na kukosa uongozi mbadala huko huko mitaani; jambo ambalo vyama vya upinzani walipaswa kuwa mstari wa mbele kujiandaa kufanya kazi hiyo, tokea miaka mitano iliyo pita.
Hebu nieleze wewe, kwa mfano katika kituo hicho ulicho tolea mfano, pangekuwepo na watu angalao watano tu ambao wangekataa matokeo hayo yaliyo tangazwa; na hali ikawa hivyo hivyo katika vituo vingi pote Tanzania... Bado CCM wange ng'ang'ania ushindi wa kulazimisha?
 
Watu hatuna imani na wasimamizi wa uchaguzi, tumeamua kuwaachia ccm waendelee wenyewe na wizi wao wa kishamba
Halafu iweje baada ya hapo. Nani kati yenu," mnaosusa na hao wezi washamba" ataonekana "mshamba" baada ya uchaguzi?
 
Back
Top Bottom