Mkuu siamini kabisa kuwa unaniuliza swali hili na kutaka kweli nilijibu.
Kwani hiyo CCM kama chama sasa hivi ina kitu gani cha ziada zaidi ya hao wengine unaoona wewe hawawezi kuwa mbadala!
Labda nijaribu kukupa jibu kwa swali lako hili kwa njia nyingine inayoweza kuwa rahisi kwako kuelewa.
Sasa hivi, hata kile chama cha "ubwabwa" cha Mzee Rungwe ni bora zaidi kuliko CCM. Hapana, usidharau ninayo kueleza. Ni hivi: chama cha mzee Rungwe kikiingia madarakani sisi wananchi tutaweza kupata fursa ya kukiondoa kama tutaona hakifai. CCM, badala yake, wao ndio wametuweka mateka, na kutufanyia kila aina ya uchafu. Hatuwezi kuwaondoa kwa njia za amani. Kinacho subiriwa tu sasa ni mpaka hapo tutakapo kuwa na ujasiri wa kuwaondoa kwa nguvu, na kumwaga damu za waTanzania.
Sasa nikuulize wewe, huu ndio unafuu wa CCM ambao unaona hakuna chama kingine kinachoweza kuwa mbadala wake?
Ninahisi kuwa umeniuliza hili swali kwa vile wewe ni mnufaika wa CCM kwa njia moja au nyingine. Ninakuomba, unapo nijibu tena, kama utafanya hivyo, jitahidi kuweka mapenzi yako kwa chama chako; jitahidi kuelekeza mapenzi hayo kwa nchi yetu Tanzania.