LGE2024 Wananchi Kata ya Zingiziwa Wagomea Uchaguzi Wakidai Kurudishiwa Ardhi Zao

LGE2024 Wananchi Kata ya Zingiziwa Wagomea Uchaguzi Wakidai Kurudishiwa Ardhi Zao

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

MeVSMe

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2024
Posts
270
Reaction score
425
Wana Jamiiforums mko salama?
Mimi naomba Wakazi wa Chanika Zingiziwa mtusaidie kuhusu suala hili, kwa mwenye kufahamu.

Juzi, nilitembelea Kata ya Zingiziwa, iliyopo Chanika na kuzungumza na wakazi kuhusu uchaguzi.

Nilijulishwa kuwa takriban Wananchi 10,000 wamekataa kujiandikisha na wameapa kutoshiriki kupiga kura,
wakishikilia kuwa hawatafanya hivyo hadi pale watakapopatiwa ardhi yao.

Wananchi hao wanadai kuwa na mgogoro wa muda mrefu kuhusu ardhi na mamlaka zinazohusika na hifadhi ya msitu wa Pugu, maarufu kama Kazimzumbwi.

Wanasema mamlaka hizi zimewanyang’anya ardhi yao na hata kuzuia kukanyaga maeneo hayo.

Wanadai mgogoro huu umedumu kwa zaidi ya miaka 10 na licha ya ahadi kadhaa kutoka serikalini kuwa wangepewa haki yao, hadi leo hakuna hatua iliyochukuliwa.

Uamuzi wao wa kugomea uchaguzi umechochewa zaidi na mkutano wa Septemba 10 mwaka huu, ambapo Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogoro, aliwaahidi kuwa mgogoro huo ungepatiwa ufumbuzi kabla ya uchaguzi wa serikali za mitaa.

Hata hivyo, hakuna hatua iliyochukuliwa hadi sasa, na mgogoro unaendelea huku ukihusisha uharibifu wa mazao na madai ya ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu.

Wananchi hawa, takriban 10,000, wanasema hawatashiriki kwenye mchakato wa uchaguzi mpaka haki yao ya kumiliki ardhi itakapotekelezwa.

Hizi ni baadhi ya nyaraka zinazohusiana na mvutano huo.

Screenshot_20241025-151252.jpg

Hii ni barua iliyoandikwa na wakulima(wakazi) maeneo tajwa


IMG-20241023-WA0005~2.jpg

Wadau wanaotokea chanika, huko zingiziwa, tuambizane zaidi Kwa wanaofahamu.
 

Attachments

  • IMG-20241023-WA0005.jpg
    IMG-20241023-WA0005.jpg
    50.5 KB · Views: 6
Back
Top Bottom