KERO Wananchi Kibangu mtaa wa Kajima jimbo la Ubungo hatuna maji mwezi wa tatu sasa

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Mkuu chimba kisima uuze maji, kwenye tatizo ndio penye fursa.

Wachaga wazee wa fursa wangeshachukua hilo dili fasta, ukiona hivyo huenda maji yake yana chumvi sana au ni gharama sana kuyapata hayo maji, kuna sehemu nilienda Malamba mawili kuchimba kisima mpaka upate maji ni almost 8 milion, na hapo huenda ukapata ya chumvi.
Sasa shida yote ya nini.

Nilichoona kule mtu ananunua tenki kubwa anaagiza gari inaleta maji anawauzia watu.
 
Umeongea ukweli halisi, afu Mamlaka za Maji hazijari wala nn.
Mxxxxiiiiieeew.
 
Bonyokwa ipi? Halafu haipo Ubungo. Maji tunapata
 

Toka lini umekuwa mshauri wa wapi watu waishi?acha watu waishi watakapo. Maji si issue hata kidogo.
 
Dar ni mji wa hovyo, tunaita jiji lakini haina hadhi hiyo;
1. Uhaba wa maji sehemu nyingi
2. Uchafu uliokithiri
3. Makazi holela sehemu nyingi.

I have never noticed tatizo la maji Dar es salaam , naongelea personal experience!
 
Dar ni mji wa hovyo, tunaita jiji lakini haina hadhi hiyo;
1. Uhaba wa maji sehemu nyingi
2. Uchafu uliokithiri
3. Makazi holela sehemu nyingi.
Uko sahihi kabisa.
 
Bado hujasema! Likizo hii nakuja hukohuko kibangu kuenjoy life
 
Yule profesa tamaa mbele analifahamu hilo?
 
Maji yapo mto Ruvu, tatizo Serikali imeshindwa kutatua tatizo la miundombinu ya maji.
 
Juma Aweso yuko pale sababu ya vitu viwili tu sitavitaja ila kiukweli hamna kitu pale.
Ngoja nivitaje,ndumba na dini
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…