KERO Wananchi Kibangu mtaa wa Kajima jimbo la Ubungo hatuna maji mwezi wa tatu sasa

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Fact
 
Tatizo ni kubwa sana
Back in 2006 nikiwa form four na wanangu tulipanga chumba maeneo ya ubungo kibangu aisee kulikuwa na shida ya maji usipime! Nashangaa imepita miaka karibia 20 tatizo bado lipo palepale, inasikitisha sana
 
[emoji91]
 
Wewe utakua afisa wa dawasa tu
 
Tunakuja huko
Shida ya maji maeneo ya Kibangu 1996- 2000 ilinifanya nichukie kibangu na jirani yake .. hata nilipoanza maisha sikufikiria kununua eneo kiwanja huko hata uchimbaji wa maji maeneo hayo sio mrahisi


Karibuni kigamboni..
 
Fact
 
Mkuu chimba kisima uuze maji, kwenye tatizo ndio penye fursa.
Maji mengi ya kisima dar siyo salama sababu ya uhovyo wa mipango miji.yaani viwanja vidogo na mashimo ya vyoo lukuki
 
Tuna miezi mitatu hatuna maji

Eneo ni kajima (Rivaside juu) mtaa wa Kibangu Ubungo

Maji hayatoki lakini watu wanauza maji na kuleta na magari na kuyauza kwa ndoo 500

Tumelalamika tumechoka inaonekana kuna mfumo wa watu kula hela na kujineemesha

Kipindi cha Magufuli maji yalikua yakitoka

Sio hivyo tu, wameleta matank ya kuuza maji na inadaiwa na miradi ya mheshimiwa fulani hivi

Naombeni mnisaidie namba ya Aweso tumechoka!!
 
Duh hata banana ukonga toka Nov mpaka sasa hakuna maji manager dawasa kinyerezi haeleweki kila siku anatoa ahadi hewa
 
Watu maji yanawatesa sana
Ila wakati wa uchaguz mitaa walikuwa wanaleta boza la maji
Dawasco wanawagawia watu maji...uchaguz umeisha maumivu pale pale

Ova
Ni mateso kwa kweli.
 
Kakindu Pongwe, Tanga mwezi wa pili unaenda wa Tatu huu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…