Wananchi Mara waandamana kuunga mkono juhudi zinazofanywa na Rais Magufuli

Pamoja na kuwa tuna baadhi ya mambo tunatenda ya 'kipuuzi' kama Taifa lkn hili la watu kujitoa ufahamu kwamba Rais atawale zaidi ya muda uliowekwa kikatiba ni ' Upuuzi' wa kiwango cha juu wa jamii yetu
 
Naunga mkono hoja, Magufuli aongezewe muda
Kwa Kasi hii ya Magufuli, kuna haja Kufanya Uchaguzi wa Rais 2020 ...

P.
 
Hilo limeshaonekana zamani sana na watu tushalisema sana!!

JPM ameanza kubadili katiba ya CCM... mwaka 2020 hana mpinzani ndani ya CCM!!!

Kitakachofuata ni kubadili katiba ya JMT! Unfortunately, sioni tena CHADEMA wakiwa na ushawishi wa kutosha kuhamasisha Watanzania tukutae ujinga kama huo!!!!
 
Kumi? Mitano hii ikiisha hapati mingine
 
Magufuli Mungu akutunze nakupenda sana ila siipendi ccm
 
Hilo mbona tumeshalisema sana...

Kuna kila dalili huo ndio mpango wa Magufuli kupitia vibaraka wake!!!

Watu aina ya Magufuli huwa wanakuwa na vibaraka mazuzu nje na ndani ya mfumo ambao kwa makusudi, huwa wanakuja kwa kauli kwamba "wananchi" wanataka aongezewe muda!!!

Dikteta Paul Kagame ndivyo alifanya miaka michache iliyopita! Kagame amekuwa de facto president kwa miaka 6, akaja kuwa president kwa miaka 17 na anataka mingine!!!

Watu aina ya Kagame na Magufuli ni wale wanaodhani hakuna anayejua kuongoza zaidi yao!! Sasa sijui ni ju'ha gani anayeweza kufungasha kwenda kutafuta maisha Rwanda kwa sababu Super President Paul Kagame ameifanya Rwanda kuwa ya Neema!!

NI kwavile tu watu walikuwa wanamchukia JK ndo wakawa wanataka kuaminishana kwamba Rwanda imepiga maendeleo kweli kweli wakati hadi leo Rwanda haijaifikia kiuchumi Tanzania na Kagame kukaa miaka 23 madarakani na kutaka mingine zaidi!

Na ndivyo tunataka kuaminishwa kwamba JPM akikaa madarakani miaka mingi ndo basi tena Tanzania itakuwa kama Ulaya ingawaje historia inaonesha hakuna kiongozi aliyekaa madarakani muda mrefu Sub Saharan Africa akaiacha nchi ikiwa bora! Hata JK Nyerere ambae kila mtu anakubali alikuwa kiongozi bora, nae aliiacha Tanzania ikiwa hoe hae!!

Na Watanzania tusipokuwa tayari kumwaga damu kuzuia uhuni kama huo, there's a big chance katiba ikabadilishwa!!!

Tayari wameshabadili katiba ya CCM... mwaka 2020 JPM hana mpinzani kupitia CCM!!
 
JAMANI.TUNAOMBA WASIJE WAKATUCHAFULIA NCHI YETU.HUU UJINGA ALIUFANYA NKURUNZINZA.NA WAO WALIANZA HIVI HIVI.NA SISI TUNAOSEMA URAIS NI MIAKA 5 BAADAE UCHAGUZI TENA TUKIANDAMANA ITAKUWAJE?
TAFADHARINI JAMANI HATUTAKI FUJO NA ***** ***** KATIKA NCHI.
VIONGOZI LIKATAZENI HILI JAMBO MAPEMA.
MARUFUKU.
 
ENDELEENI KUKUSANYA KUNI.
MOTO UNAKUJA.
MAANA MNAONA BURUNDI WANAISHI KWA RAHA MUSTAREHE.
 
Haijawahi kutokea kwa rais yeyote wa Tanzania akaongoza chini ya miaka 2 halafu watu wakatamani aongoze zaidi ya muda uliowekwa kikatiba. Madaraka hulevya sana, huyu aliyekuwa analalamika kuwa kazi ya urais ni ngumu anatamani hata angekuwa anaongoza kwa miaka 2, mwangalieni vizuri ikifika 2022-24. Katiba lazima itabadilishwa ili aendelee.
 
Kwa jinsi alivyombabe wala sitashangaa. Angekuwa muungwana angekuwa ameshajitokeza hadharani na kusisitiza kuwa Katiba haitabadilishwa kwa ajili yake. Anajiona yeye ndo Masia wa maendeleo ya Tanzania, hivyo tutegemee lolote.
 
Natamani wapinzani wampe shinikizo la kuheshimu Katiba akimaliza muda wake. Hasa Dr. Mashinji, hii ndo kazi yake. Amtake rais atoe kauli ya kuheshimu ukomo wa madaraka wakati ukifika. Tusiruhusu kauli hizi za kuongeza muda zizoeleke masikion mwa watu. Hata Kagame ilikuwa hivyo hivyo, watu walikuwa na wasiwasi nae miaka 5 kabla ya wakati wake kuisha na sasa yupo anagombea.

Kama Magu atafanya kazi ya urais kwa miaka 10 halafu akose mtu wa kuendeleza maono yake ktk serikali nzima, basi atakuwa hafai hata kidogo kutuongoza. Akishindwa kabisa kututafutia mrithi wake, ni heri atupe hata Bashite kuliko kuendelea na uongozi kwa kubadilisha katiba.
 
Kitu kama hicho hakiwezi kutokea,wapambe tu ndo wanajipendekeza kuandaa maandamano ya kuomba aongoze zaidi ya muda uliowekwa kikatiba,yeye hawezi kukubali
 
Acha ramli chonganishi!!!Mbowe kabadili katiba kinyemela kuwa Mwenyekiti wa maisha hujafungua thread

Ni kweli usemayo hata mm nakubali Mbowe kachemka. Ila huko cdm kama hukubaliani na hilo unaweza kuhama chama au kuanzisha cha kwako kama Zito. Je kwenye nchi? Kweli unaweza fananisha katiba ya nchi na ya cdm? You can't be serious.
 
Anawatisha wastaafu kwa kashfa zao as zamani na kuunda tuvikundi twa mazezeta kuandamana
Kuwa aongezewe muda.Sijui wastaafu wameogopa?tutaona.ONly time will tell.
Wastaafu ndo kina Nani? Au una maanisha wazee walioachwa "wapumzike"?
 

Mambo ya kubadili katiba ili kiomgozi asiwe na UKOMO wa madaraka ni bema wakawaachia CHADEMA. Ingawa kiukweli wananchi wengi kwa sasa wanahofu kama Rais atakayefuata hataturudisha Kwenye nchi ya MADILI, UFISADI na kuchekacheka hata kwenye issue serious.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…