Wananchi tuna haki kufahamu alipo Makamu wa Rais Philip Mpango

Amen
 
"Nimesikia habari nzito kuhusu mwamba huyu lakini siwezi kuisema hapa kama ilivyokuwa vigumu kusema ya Magufuli" - Nukuu Mkuu TPaul, yawezekana unajua kitu fulani kinachofichwa kuhusiana na huyu mwamba. Japo kwa "codes" ebu jaribu kufunguka zaidi.

Ukisoma "between the lines" katika andiko lako, mbona linatisha!?
 
Wakati ukuta. Tusubiri tutangaziwa muda mfupi ujao. Hawawezi kuficha milele.
 
Tulimpoteza Magufuli kwa sababu kuumwa hadi kuzidiwa kulifanywa National Bigly Secret ambapo wananchi hatukujulishwa iwapo anaumwa ama amezidiwa zaidi ya kustuliwa na taarifa ya kifo chake mnamo 17 March 2021...
Wasijibebeshe mzigo bila sababu. Waseme tu hali ilivyo. Kwani kuugua itakuwa yeye ni mtu wa kwanza? Wanavyofanya mambo kwa kificho wanatufanya tusiwaelewe vizuri, au tuanze kuwatilia shaka na kuto waamini.
 
Sawa kabisa kama kuna tanzia la kitaifa tujulishwe!
 
Serikali ina utaratibu wake wa kufanya mambo yake, nadhani hata ukienda ikulu uatajibiwa hivyo.
Hili jibu linatosha.

Hata kwenye familia baba akiwa mgonjwa watoto hawawezi wakawa wa kwanza kuambiwa, na hata kama akianguka mbele ya watoto atabebwa na baadaye watoto wanaelezwa kwamba baba ni mzima kabisa na anawapa hi.
 
Uliambiwa yupo kwenye majukum, ni swala la utulivu tu, wasije kuja na habari zingine full stop,

Sie tushikilie kauli tajwa hapo iliyotolewa , vinginevyo hataeleweka mtu, kwa sababu hata kama anaumwa ni lini Tumeona kiongozi wake amemtembelea na kumjulia hali,

Kama Rais wa nchi kubwa kama USA anaumwa na ulimwengu wote unajua kwa nini kwenye nchi za kwetu, binafsi naamini ni mzima anaendelea na shughuli zake kama tulivyotangaziwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…