Hizi si video za kutengenezwa na akili mnemba bali ni halisi.. Na hawa si wananchi wa kuandaliwa ili wafurahie bali unaweza kuona walikuwa wamekaa na maumivu mengi kwa muda gani..
JM amekuwa kwenye nafasi za juu serikalini tangu enzi za JK, amekuwa na ushawishi wake na ndoto zake... Amekuwa na mitandao yake na watu wake
Kuanguka/kuangushwa kwake kwenye kura za maoni kinyang'anyiro cha ubunge sio fedheha kwake tuu bali ni wake up call kDa chama cake kujitafakari kama kitaweza kufanya hivyo
Imagine kama wapiga kura wake wamelipuka kwa shangwe jamaa kuanguka, vipi kwa watanganyika wengine!
Je ni wangapi huko kwingine waliopitishwa kwa mabavu na wapiga kura wao wanaugulia maumivu ya kimya?
Miezi michache iliyopita mkuu wake kazini alifunga safari na msafara mzima hadi Jimboni Bumbuli kwenda kumsamehe JM... Hii ilileta ukakasi mkubwa kwakuwa mwenye kosa ndio huenda kuomba msamaha na si kufuatwa! Kumbukeni ya Nape Nnauye!
Leo mtu uliyemfungia safari kwenda kumsamehe kaanguka wananchi wamelipuka kwa shangwe mpaka kuchinja ng'ombe hata wewe tambua hauko salama!
Wamesikika wananchi wakisema hatimaye DALALI WA BUMBULI kadondoka.. Maneno hayo pia ni wake up call kwa level ya kitaifa.. Ni muhimu sana kujitafakari.. Ni muhimu sana kusikiliza sauti za wananchi
Kaanguka JM lakini anguko lake linaweza kuathiri uimara wa mbuyu pakubwa sana.. Na kujikuta nao unaanguka kwa pigo moja tuu
Tunywe supu ya shangwe dalali kadondoka!
View attachment 3423797