GE2025 Wananchi wa Bumbuli wachinja ng'ombe kusherehea January Makamba kukatwa

GE2025 Wananchi wa Bumbuli wachinja ng'ombe kusherehea January Makamba kukatwa

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Watanzania wajinga sana! Sasa wanashangilia nini? Maana kama kumtoa si wao waliomtoa, na pia hajatolewa kwa sababu ya performance yake kuwa mbaya Bali kwa sababu tu ya yeye kutofautiana na wakuu wake. Angepitishwa na kamati bado angekuwa mbunge hata kama wananchi hawamtaki. Tupiganie reforms ili wabunge ambao hawasaidii waweze kutolea na wananchi wenyewe. Si mpaka kusubiri huko juu
 
Hapo ni kugeukia kilimo hizo degree zake za sociology sijui Kama atapata kazi
 
Waacheni wafu wazikane. Kama kweli hakubaliki wangeacha box la kura liamue.
 
Mwazahumua wedi wagosi wa JF?

Mwahumuaze wandee wose na va mame?

Na wale wengine bila Shaka mtakuwa wazima.

✍️Jimbo la BUMBULI wananchi wamefurahi January Makamba kukatwa mpaka wameamua kuchinja.
Tutaona mengi huu mwaka

Ndio kwanza intra-party nominations zimeanza.

View attachment 3423785
Mwisho wa uovii ni mbaya sanaaa na huyu shida ilianza kwa JPM yeye na Nape ,Nape akawa mjanja akaenda kuomba radhi yeye kwa sababu ya ujeuri akakausha
 
Mwisho wa uovii ni mbaya sanaaa na huyu shida ilianza kwa JPM yeye na Nape ,Nape akawa mjanja akaenda kuomba radhi yeye kwa sababu ya ujeuri akakausha
Alijua CCM ni ya makamba kumbeee inategemea upepo unaelekea wapi
 
Kamati maalum yaani task force ya wazee ilifanya kula mbuzi.

Vijana na wengine wao waangusha ng'ombe.

Kwisha kazi.
 
Kamati maalum yaani task force ya wazee ilifanya kula mbuzi.

Vijana na wengine wao waangusha ng'ombe.

Kwisha kazi.
Bora na wewe unisaidie maana Kiranga alitaka ushahidi
Mda huu tunachemsha kongoro kuizimua Siku mpyq ya kusaka kura za wajumbe sasa kwa wagombea pendwa
 
Bumbuli awamu hii ni ya kilua
Zile ngumi January na genge lake waliwashona chawa na kilua hazikuwa za bure
 
Mwazahumua wedi wagosi wa JF?

Mwahumuaze wandee wose na va mame?

Na wale wengine bila Shaka mtakuwa wazima.

✍️Jimbo la BUMBULI wananchi wamefurahi January Makamba kukatwa mpaka wameamua kuchinja.
Tutaona mengi huu mwaka

Ndio kwanza intra-party nominations zimeanza.

View attachment 3423785
Makamba hajakatwa makusudi kuna cheo ameandaliwa kwenye chama tena kikubwa sana
 
Tunasubiri kuangushwa kwa majitu mawili, lililokuepo na lililopo ili tufanye sherehe ya kitaifa, Ahadi zako hazichelewi Mungu wetu, tunaomba uliponye taifa ambalo sasa ni genge la wahuni.
 
Back
Top Bottom