GE2025 Wananchi wa Bumbuli wachinja ng'ombe kusherehea January Makamba kukatwa

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
nimeishi halmashauri ya BUMBULI kwa muda wa miaka kadhaa sijawahi muona JANUARY zaidi kumuona kwenye TV siku ya ziara ya RAIS lushoto tena sikutaka kwenda maana nilikuwa sijawahi kwenda halmashauri nikajichanganya kwenda walipokuwa wanazindua jengo la halmashauri nilipanda bodaboda kutoka SONI hadi halmashauri aisee nilikula vumbi balaa maana jamaa hakuna ata barabara yoyote ya rami aliyotengeneza zaidi ya ile barabara ya MOMBO-LUSHOTO ,yaani bumbuli ukipiga picha ya drone utachoka nyumba zimechoka balaa na nyingi za udongo na masikini ni wengi aisee,uzuri wa lushoto kinachowaokoa wananchi hawateseki sana ni hali ya hewa na maji ya kutosha yanasaidia hawalali njaaa maana kilimo cha ndizi ,matunda,mbogamboga na mazao mengi yanakubali,
 
Mzee wake watampelekea kilo ngapi
 
miaka 15 mtu amekua mbunge, WAZIRI tena amekua karibu sana na Maraisi lakini wananchi wa jimbo la Bumbuli hawajui Lami ni kitu gani, Jimbo liko nyuma kimaendeleo utafikiri wako mwaka 1987.

Pumzika kaka January Ma-rope
BUMBULI kwekundu kama kigoma vile wakati wamebarikiwa hali ya hewa nzuri na maji ya kutosha kula huakika ,
 
Siku zote mwisho wa ubaya Huwa ni aibu
 
I
Ikiwa hii reform ya Uchaguzi huru haiwezekani inawezekana hiyo ya ya kuwatoa Wabunge 🤣🤣😅😅😄 !
 
Ajabu sana,akatwe January,angizwe Abdul,ccm ni ile ile. Maskini,wamejitoa ufahamu hao,wahahitaji uponyaji.🥲
 
Ni chuki tu za kupandikiza, wanategemea nini zaidi Kwa atakae kuja? Ajira ? Maisha nafuu ? Wacha tuone na mje mchinje japo bata Kwa hayo matumaini yenu, TUNASUBIRI HAYO MAAJABU.
 
Watumwa watu wajinga sana, yaani wanashangilia bwanyenye mpya.. hapo walioshinda ni wale wazee wa meza kuu wanajua kucheza na akili ya watumwa......
Huyo wanayempeleka naye hana jipya zaidi ya kuendeleza kile kile
The House Will Always Win...
 
Kwa taarifa tu ni kwamba, January Makamba amekuwa na nidhamu yenye mashaka Tangu 2012 aliitwa kwenye kikao Dodoma pamoja na akina Lowasa kwa Kosa la kuanza Kampeni mapema. Akakiri akasamehewa

2018 alimwomba Msamaha Mwenyekiti wa Chama chake kwa makosa ya kinidhamu akasamehewa na akapitishwa kugombea Ubunge 2020.

2024 akakamatwa na watu wa usalama akiongoza genge la kumstaafisha Boss wake nje na utaratibu na Chura wa Kizimkazi sio kama JPM hana msamaha

Kwa ufupi ni kwamba, January Makamba anaongoza Magenge na sio kambi.

Makamba ni Kibaraka/coordinator wa Magenge ya mafisadi, mauaji na MISSION TOWN hapa nchini yaliyo chini ya ROSTAM.
 
Watajua wenyewe Ila muhimu kwa wana nchi hayupo
 
Bora na wewe unisaidie maana Kiranga alitaka ushahidi
Mda huu tunachemsha kongoro kuizimua Siku mpyq ya kusaka kura za wajumbe sasa kwa wagombea pendwa
Tanzania nchi ya ajabu sana.

Huyu bwana ndiye tuliambiwa kapita bila kupingwa uchaguzi uliopita.
 
Tanzania nchi ya ajabu sana.

Huyu bwana ndiye tuliambiwa kapita bila kupingwa uchaguzi uliopita.
Mifumo yenu si unaijua lakini?
Hata hivyo sio haba amekula miaka ya kutosha
 
Mifumo yenu si unaijua lakini?
Hata hivyo sio haba amekula miaka ya kutosha
Wanasema anapimwa imani kama anaweza kukaa benchi bila malalamiko au kuhama chama.

Akipita mtihani atapewa pande kubwa mpaka mtashangaa wenyewe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…